Kwa nini sheria za mitandaoni inabidi ziangaliwe upya

NullPointer

JF-Expert Member
Feb 7, 2011
3,461
2,273
Hizi sheria za mitandaoni zilikuwepo toka zamani lakini zimeanza kubanwa awamu hii ya tano. Kuna sababu kwa nini nchi nyingi duniani hawana hizi sheria, na nchi zenye hizi sheria wamezilimit, Tanzania kama nchi ambayo haijaendelea haina uwezo wa kuisimamia hii sheria na kuhakikisha kua hakuna mtu kaonewa. Sababu kubwa ni kua hatujaendelea kiteknolojia, hata watu wanaotoa hukumu na wanaokua consulted wanajua kutumia simu tu ila nothing more.

Hadi leo kitu kinachomfunga mtu ni screenshot ya alichokipost, hawana uwezo wa kupata post yoyote ile kama mtu mwenyewe kaifuta, sasa kwa nini kutumia screenshot ni ujinga? Screenshot mtu yeyote yule anaweza akai~forge na ikaonekana kama original ndani ya sekunde 30. Mtu akitaka kukusakizia kesi mfano facebook au page yoyote, kama anatumia chrome au firefox, akiright click anaenda developer tools -> inspect page -> anatafuta post yako, anaiedit hapohapo inabadilika, anachukua screenshot anaisambaza kila kona, kesho yake utaona polisi wanakugongea mlango. Ukisema sio wewe lazima utaambiwa tu kua umeifuta, pamoja na kua ukweli sio wewe uliyepost.

Mfano mwingine JF kuna kum~quote mtu, ukiclick quote, unauwezo wa kubadilisha maneno aliyopost kwenye quote yako, hiyo haitohitaji hata screenshot, kama wakitumia post yako wakiamini kua ile original aliyepost kai~edit kufuta ile part mbaya (kitu ambacho hata mtoto mdogo anajua its crazy) umekwisha.

Sasa tunabaki na Whatsapp, kwa kua mtu hawezi badilisha then kwa nini wasitumie yenyewe kama evidence, ila tatizo linakuja hapa, mtu yeyote yule anaweza akachukuliwa simu na mtu anayemchukia akapost kwenye groups zote ujinga kumsakizia kesi, una uhakika gani kua mwenye hiyo account ndo aliyepost? Ukimkamata akatupa simu mbali akasema iliibiwa na sio yeye aliyepost je? Utatumia evidence ipi kua yeye ndiye aliyepost? na hata kama simu anayo, akisema sio yeye aliyepost maana simu inaweza guswa na mtu yeyote yule, kama kweli ni innocent lazima atafungwa kwa kua atashindwa kuprove kua sio yeye aliyepost.

Sheria kama hizi wakiwa wanatunga labda wawe wanajaribu kuuliza watu wanaohusika na hiyo field yenyewe ili wajaribu kupima pande zote mbili, mambo ya online ni magumu sana kuprove, najua kwa bongo wengi wanafikiria kwa kutumia mihemko sio akili wanaamini wanachokiona mbele yao ambacho ni screenshot. Watu wengi sana wataumia kwa hii kitu, wengine wasio na hatia.

Kama una counter-argument ningependa kuisikia.
 
Back
Top Bottom