kwa nini nafurahi kikwete kuanguka jukwaani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kwa nini nafurahi kikwete kuanguka jukwaani?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mwikimbi, Aug 23, 2010.

 1. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  ni kawaida binadamu kutofurahia maanguko au mateso ya mtu mwingine waziwazi. lakini kwa nini hili la kikwete nachelea kumsikitikia?

  ninazo sababu zangu nyingi lakini baadhi tu ni hizi

  1. kiwete ni msanii alitukuka, yeye na wasanii wenzake wameeendelea kuwasanii watanzania kwa muda wa miaka mitano, wakati wananchi wanakufa njaa, hawana matibabu yeye anatumbua mapesa na mali asili zanchi hii na wateule wachache. kwa kuwa kuna wananchi wanaoanguka kwa njaa, kwa nini nijali kuhusu msanii kama kikwete kuanguka jukwaani, tena wakati anawaghilibu wananchi kwa kuwasomee litania ndefu ya mafanikio anayoyajua yeye na msanii mwenzake rostam aziz?

  2. bado ule wizi wa epa na kagoda unanisumbua akilini. wakati kikwete na wenzake walichota mabilioni wakahonga mpaka akawa rais, badala ya kuwakamamta wale walioiba wanajulikana waziwazi, rosta, lowasa, nimrod mkono, kingunge, yeye na vibaraka wenzake wakawasweka ndani wasiohusika kama wale wafanyakakzi wa BOT. sasa wananishi maisha ya dhiki hawana mbele wala nyuma. kwa nini sasa nisifurahi kidogo anguko lake ambalo ni adhabu toka kwa MUNGU?

  3. jakaya kikwete anataka kujenga usulatni wa ajabu hapa nchini, sasa yeye na wanawe ndo waamuzi wakubwa kabisa katika maisha na mustakabali wa nchi yangu, kama alivyokuwa sadam na wanawe wawili ndivyo alivyo kikwete, mkewe, na wanawe , kwa nini nisifurahie anguko la mtu kama huyu?

  4.JK, WATU WANAKUDANGANYA, UMEZUNGUKWA NA WEZI, MAFISADI, PALE JUKWAANI JANGWANI UNAPOANGUKA KILA WAKATI WA KAMPENI KUNA ZINDIKO KUBWA, SEPTEMBER 5TH, 1990, MTU WA HAKI, NA MTUMISHI WA MUNGU BABA MTAKATIFU YOHANE PAULO WA PILI, ALIHUTUBIA TAIFA, AKALIKABIDHI TAIFA HILI KWA MUNGU, ILI WAONGO, WAZANDIKI, WAHUNI, WASANII, WALA RUSHWA, WAFISADI, WAKARIBIAPO PALE WAPATE KUANGUKA!

  UTAANGUKA DAIMA
   
 2. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Mwanangu kuwa uyaone, aliniambia mama yangu Lukomo
   
 3. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Hee! Kwahiyo JK kaangushwa na papa! Nijuavyo mimi Taifa hili halina dini. Huyo papa kapata wapi mamlaka ya kukabidhi Taifa hili kwa huyo Mungu wako
   
 4. Mshirazi

  Mshirazi JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2010
  Joined: Dec 8, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo...SILAA akiukwaa URAHISI pale (jangwani) ndio itajengwa IKULU? au KANISA?? maana panaonekana ni mahala PATAKATIFU
   
 5. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #5
  Aug 23, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,936
  Likes Received: 12,206
  Trophy Points: 280
  Inaonekana nyote nyie na Mahesabu hamjamwelewa Mwikimbi.
   
 6. M

  Msee Lekasio Member

  #6
  Aug 23, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana jamfi!
  tusisahau kitu kyingine muhimu. Kikwete na kundi dhake wamedheta hongo nyingine mbaya sana ya kuwanunua wagombea wa upinsani. Kwa mfano wakiona mgombea wa Chadema ana ngufu kubwa sa kushinda wanampa hedha ili akosee kujasa idhe fomu ya ubunge kwa makusudi. Matokeo yake ni msimamisi wa uchagusi kumwengua.
   
 7. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #7
  Aug 23, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,506
  Likes Received: 1,230
  Trophy Points: 280
  Ari mpya Nguvu mpya Kasi mpya =ANGUKA NDio maana anaanguka anguka ila asiendelee kuanguka manake atazima
   
 8. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #8
  Aug 23, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Mimi Kikwete simpendi kama rais, lakini siwezi kusema nafurahia kumuona anaanguka jukwaani katika hali kama ile.Kusema hivyo ni kukosa ubinadamu kunakoelekea katika uchuro ulio karibu na ulozi kama si uchawi kabisa.

  Ingawa sipendi siasa za Kikwete, naona kufurahia ugonjwa wa mtu mwingine si ustaarabu na kunaonyesha udogo wa mawazo.

  Kama unakataa siasa za Kikwete, kataa siasa zake, huna ulazima wa kutaka kuona anaumia kimwili ili ukamilishe kukataa siasa zake. Ndiyo maana watu makini katika upinzani ngazi ya taifa wamemtumia salamu za pole. Upinzani wa kisiasa haumaanishi uhasama binafsi.

  Na hili ni jambo la msingi kabisa katika ubinadamu, hata ukitoa urais wa Kikwete.
   
 9. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #9
  Aug 23, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  Huoni kama ni 'ubinaadamu' yeye ndiye wa kwanza kuukosa? ....kwa kufuja fedha za wananchi eg EPA huku akiwaacha maelfu wakifa kwa maradhi au matatizo ambayo yangeweza kuondolewa na hizo fedha wanazofuja?
   
 10. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #10
  Aug 23, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  no comment ila mimi sipendi anguko badala yake sipendi kabisaa apate urais
   
 11. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #11
  Aug 23, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Two wrongs do not make a right, kama Kikwete kakosa ubinadamu - kitu ambacho wengine wanaweza kukipinga- haimaanishi hilo linakupa leseni na wewe ukose ubinadamu.

  Kikwete akijivua suruali hadharani na kuonyesha dhakari yake (ashakum si matusi, naonyesha ujinga wa kuiga mabaya tu) na wewe utataka kuvua suruali hadharani na kumuiga ? Ukitaka kukosa ubinadamu kama yeye (unavyodai wewe) utapata wapi moral high ground ya kumsema yeye ? Utawezaje kutuambia tuna haja ya kubadilisha uongozi mmoja unaokosa ubinadamu kwa kutaka kuleta uongozi mwingine unaoungwa mkono na wahuni wasiojali ubinadamu? Tofauti itakuwa wapi sasa ?

  Acheni hizi simplistic positions zilizojaa fanatic zeal kuliko informed thinking.
   
 12. Maverick

  Maverick JF-Expert Member

  #12
  Aug 23, 2010
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 308
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ...Bado sioni kuanguka kwa Kikwete kunahusiana vipi na hoja zilizotolewa......Yaliyotokea kwa JK yanaweza kutokea kwa binadamu yoyote......Tuweke ubinadamu mbele....
   
 13. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #13
  Aug 23, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  Two wrongs do not make right BUT ALSO one wrong and one right do not make right... siyo? Ohoo dear...ule wakati wa kugeuza shavu ulienda na karne iliyopita!!!!!
   
 14. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #14
  Aug 23, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  At least with one wrong and one right utanionyesha unaanza ku right the wrong, wewe unaposema unataka kutoa wrong kwa wrong possibly ili ulete wrong nyingine hunipi sababu ya kutaka kubadili hii wrong iliyopo.

  Nibadili ili iweje sasa? Nitoe wrong moja na kuingiza wrong nyingine?
   
 15. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #15
  Aug 23, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Non sense
   
 16. Ilumine

  Ilumine Senior Member

  #16
  Aug 23, 2010
  Joined: Dec 27, 2008
  Messages: 196
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo Avatar yako, mhhhh! ni vita tu inaashiria, tusichochee vita jamani, mnatuogopesha!:confused2: Tazama Pakistani wanavyokufa kwa mafuriko, China nako tena hali ni mbaya. Sasa, Bunduki na jambia unaendelea kushikilia, ona huruma kwa uhai, Uhai ni mali ya Mungu!
   
 17. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #17
  Aug 23, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Aisee! Ukiona unaongoza nchi ya watu wenye akili kama hii, basi ujue huna wananchi humo, maana ni likely kwamba wote wamepotea hawana uwezo wa kuchambua wala kutafakari mambo kwa undani. Kama JK anafurahia kuwa na watu kama huyu mahesabu basi lazima na yeye akili yake itakuwa na mshikeli.

  Kwa hiyo wewe mahesabu, shida zote hizi za watanzania zinazotokana na uongozi mbovu wa CCM wala huzioni? Inflation ya kutisha iliyopo nchini huioni? Kushuka kwa thamani ya hela ya Tanzania kunakoendelea hivi sasa huoni? Huduma mbovu zilizopo mahospitalini kwa wagonjwa na vifo vya watoto na akina mama wajawazito wala huzioni? Kutumia bilioni moja na zaidi kujenga nyumba moja tu ya gavana kwako ni sahihi despite umaskini mkubwa unaowazunguka wananchi? Kutumia bilioni zaidi ya 200 za wananchi walipa kodi maskini kwa ajili ya safari za Rais kwako wewe ni sawa tu?

  Nina wasiwasi na uwezo wa akili wa Watanzania, pia nina wasiwasi kama kweli kunaweza kutokea mageuzi ya maisha ya mtanzania kama watanzania wenyewe tulionao ndiyo kama hawa!
   
 18. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #18
  Aug 23, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  Tatizo wewe ni mtu wa theories kwa sana.... sio kila mahali uta-apply hiyo... Akianguka tena na tena na tena na tena na tena na tena atasikia aibu na kuwaachia wenye uwezo watawale. Hata kama hatuna uhakika anayekuja ni mzuri zaidi lakini bado ni one step ahead! Ndio maana jamaa kasema kila anapopiga chali ni one step ahead....na unaposonga kila hatua unayosonga mbele ni furaha...
   
 19. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #19
  Aug 23, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Wewe unafurahia mtu kuanguka kwa ugonjwa, mtu anakupinga unasema hiyo ni theory?

  Wewe unataka aachie madaraka kwa sababu ya kuanguka? Asipoanguka tena ? Wewe una strategy gani zaidi ya kutegemea kudra za mtu kuanguka mwenyewe? Is this the best upinzani can do? Kusubiri mtu aanguke ? Unajuaje kama akianguka tena na tena ataachia wenye uwezo watawale? Akiwaachia wazembe wengine utasemaje? Utaombea nao waanguke ?

  Huna uhakika kwamba atakayekuja ni mzuri lakini bado unaona ni one step ahead? Unajuaje kama si one step back ?

  Hivi kama hupendi siasa za Kikwete huwezi kumpinga Kikwete kisiasa na kuonyesha udhaifu wa hoja zake bila kumtakia aanguke kimwili?

  Hivi kumuangusha Kikwete kisiasa wapinzani hawana njia nyingine zaidi ya kuombea aanguke kimwili ?

  Mimi nataka kuona upinzani unaokuja kwa fikra mpya, unaoleta matumaini, unaotupeleka kwenye uongozi unaojiheshimu na na wenye nidhamu kwa dhamana ya uongozi wa wananchi.

  Nafurahi kuona viongozi wa upinzani wameweka ubinadamu mbele ya siasa. Alipoumia Slaa Kikwete alimtumia pole, Kikwete kaanguka Slaa amemtumia pole. Angalau kuna ubinadamu.

  Hawa fanatics wanaokuja hapa kutaka kumla nyama binadamu mwenzao hawana support ya official positions za upinzani ninazozijua. There is a reasopn for this, the reason being these positions do not make sense humanely or even politically - they backfire terribly, Tanzanians do not like a ruthlessly inhumane politics-, ndiyo maana hata kama - I am not saying they actually do this, note hata kama- upinzani unataka kumuona Kikwete anaanguka na kufa jukwaani viongozi wao, kwa kujua responsibility ya ku project image ya ubinadamu, hawawezi kusema hivyo kamwe .

  But I guess some people will never get that through their heads.
   
 20. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #20
  Aug 23, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  safi sana mkuu hahaaaa haaaaa
  ukiona unaingiwa na ubinadamu wa kumuonea huruma mwenziyo ni dhahiri kuwa wewe unamjua Mungu,
  maana nje ya kumjua Mungu hakuna mwanadamu mwenye huruma kwa mwenizie
   
Loading...