Kwa nini mnichukie...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini mnichukie...!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Oct 8, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Oct 8, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Sisi binaadamu tunajipenda sana, katika kujipenda kwetu ndio maana tuko tayari kuwaona wengine wakiumia ili sisi tuone raha, yaani kuna watu wengine hufurahi sana kuwaona wengine wakiumia kihisia.

  Kwa kujipenda kwake binadamu anataka aone kuwa yeye peke yake ndiye anafanikiwa maishani, yeye peke yake ndiye anayepata sifa na yeye peke yake ndiye anayepewa heshima. Ili hayo yatimie ni lazima binadamu wengine wawe chini yake, kwa maana kwamba wasifanikiwe, kwani kufanikiwa kwao kutakuwa na maana ya kumzidi yeye.

  Wote tunajua maana ya chuki, ingawa kuna uwezekano mkubwa wengi wetu hatujui ni kwa kiasi gani chuki dhidi ya wengine hutuharibia maisha yetu na kutufanya kila siku kubaki katika hali duni tuliyomo.

  Hebu jaribu na wewe kufanya utafiti mdogo. Ni mtu au watu gani ambao wewe unawafahamu vizuri kuwa wana chuki dhidi ya watu wengine?

  Ninaposema chuki nina maana ya watu ambao wenzao wakipata wao hujisikia vibaya, wenzao wakifanikiwa wao huponda na kudharau mafanikio yao, wenzao wakijitahidi kupanda kimaendeleo wao huwashusha, wenzao wakisifiwa kwa jambo zuri wao hujitahidi kuwaharibia majina na tabia nyingine za namna hiyo.

  Hebu waangalie watu hao ambao wana tabia kama hizo, halafu uangalie au upime kiwango cha maendeleo yao, unaweza ukapima pia aina ya maisha wanayoishi. Bila shaka utagundua kwamba kwa kiwango kikubwa ni watu ambao wana maisha duni siku zote na ni watu ambao maisha yao yanaonekana yamejaa nuksi na hawana furaha katika maisha.

  Sisemi hata hivyo kwamba watu wote wasio na kitu wana chuki, au sisemi kuwa watu wote wenye uwezo hawana chuki, hapana. Kuna watu wenye chuki lakini ambao wana uwezo, ingawa uwezo huo kwa kawaida huzongwa na mikosi tele na kukosa amani ya nafsi.

  Kuna watu wasio na kitu ambao hawana chuki hata asilani, lakini hawa maisha yao siku zote yamejaa matumaini na furaha ya kweli. Chuki kwenye maisha ina kazi moja tu, nayo ni kuhakikisha kwamba anayeifuga hata siku moja hapandi juu kimafanikio, na anaishi kwenye fadhaa, wasiwasi na kukosa furaha siku zote.

  Chuki hupoteza muda wetu, hutuharibia mahusiano na watu, hutukosesha bahati na baraka, sasa kwa nini mtu usiamue kubadilika?

  Ukianza kuondoa chuki moyoni au rohoni mwako ni wazi utaanza kujisikia mwepesi zaidi kimwili na kiakili na ninachoweza kukuhakikishia ni kwamba utaanza kuona mabadiliko kwenye shughuli na mambo yako.
   
 2. N

  Nsuri JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 996
  Likes Received: 183
  Trophy Points: 60
  Mbona picha kama ya baba yangu????
   
 3. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  No man is a true believer unless he desires for his brother that which he desires for himself.
  Prophet Muhammad (pbuh)

  :poa
   
 4. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,175
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  shikamoo Mtambuzi!
  yani unalosema ni maneno kuntu kuliko maelezo!
  chuki huzidi kutudunisha na kuumiza miioyo yetu halafu la kuchekesha zaid utakuta mtu anamchuki mwingine huku yule mwingine hata hajui maskini kuwa anachukiwa na maisah yanasonga mbele!
  CHUKI NICHUKIE ROHO YANGU NIACHIE!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Root

  Root JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,263
  Likes Received: 12,985
  Trophy Points: 280
  Siku za mwisho watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe,wenye chuki,wenye kupenda pesa etc
  Haya yalisema na Yesu kabla hajafa

  Sent from my BlackBerry 9860 using JnamiiForums
   
 6. Gunda66

  Gunda66 JF-Expert Member

  #6
  Oct 8, 2012
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 508
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Asante kwa kunifungua macho Mtambuzi,, yaan nimepima juu ya mafanikio ya watu ambao wanachuki kali dhidi ya wengine na kiukweli hawana maendeleo hata kama huwa wanalipwa pesa nyingi,,
  hii yote ni kutokana na kuwa pesa zao pia huwa hawafanyii mambo ya maendeleo ila hufanya show off ili wapate attention kwa wa2 wengine na waonekane wao ni bora zaidi,,
  Asante kwa somo la Leo,,
   
 7. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #7
  Oct 8, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  nilijua ni wassira hahahahaaha
   
 8. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #8
  Oct 8, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  nalilia uzima mieeeee! rizki MUNGU atanipa!
   
 9. Paloma

  Paloma JF-Expert Member

  #9
  Oct 8, 2012
  Joined: Jan 22, 2008
  Messages: 5,341
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Machiavelli bana, alisema yote hayo...
   
 10. piper

  piper JF-Expert Member

  #10
  Oct 8, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 3,260
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  True to the best of my knowledge, chuki hupelekea kuwa na vinyongo ambapo mwisho wa siku husababisha tupate magonjwa yawezayo kuzuilika.
   
 11. T

  Tetra JF-Expert Member

  #11
  Oct 8, 2012
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 1,523
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Tunawahitaji sana watu wenye CHUKI zisizokuwa na msingi.Maana ndio wanaofanya wanaojitambua watumie vema vipawa vitatu vya AKILI,,UWEZO na UTASHI ili kusonga mbele.Katika Afrika watu hawa ndio bado kikwazo,ila nchi za wenzetu vikwazo ni mazingira,hali ya hewa n.k ILI tufike waliko wenzetu tunahitaji kundi kubwa la WALIOJITAMBUA ili wawapuuze WASIOJITAMBUA.
   
 12. Anthony Lawrence

  Anthony Lawrence JF-Expert Member

  #12
  Oct 8, 2012
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 1,544
  Likes Received: 318
  Trophy Points: 180
  Asante kwa darasa Mkuu
   
 13. promiseme

  promiseme JF-Expert Member

  #13
  Oct 8, 2012
  Joined: Mar 15, 2010
  Messages: 2,715
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 135
  Unko umenigusa ndipoooooooooo!!! wapo kwenye ulimwengu haooooo............
   
 14. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #14
  Oct 8, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  :A S 465::A S 465: Hasa hasa chuki ikichanganyikana na wivu :A S 465::A S 465:
   
 15. S

  Stinker Member

  #15
  Oct 8, 2012
  Joined: Sep 9, 2012
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Am so blessed with your post......Asante mtambuzi
   
 16. Z

  Zero One Two JF-Expert Member

  #16
  Oct 9, 2012
  Joined: Sep 16, 2007
  Messages: 9,390
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Chuki ni dhambi kuu ifikishayo motoni kwa waaminio Mungu, ila kwenye Satanic bible wanafundisha kitu tofauti, wana sema huwezi penda kila mtumaana ukifanya ivyo unakua umeloose power of selection
   
 17. Philipo Kidwanga

  Philipo Kidwanga Verified User

  #17
  Oct 9, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 2,063
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mtambuzi bana una akili sana wewe,yaani chuki huathiri hata siha ya mwili maana muda mwingi mtu huwa na jakamoyo na wengine ndipo wanapokuwa wachawi kabisa chuki ni giza la kujitakia.
   
Loading...