Kijakazi
JF-Expert Member
- Jun 26, 2007
- 5,645
- 6,477
Leo hii nimesoma kuwa raisi kikwete amefungua rasmi TBC tanzania broadcasting corporation, badala ya Television ya Taifa (TVT), swali langu humu ambalo labda kuna mtu anafahamu jibu lake ni kwamba ni KWA NINI JINA LA TVT AMBALO NI LA KISWAHILI NA KILA MTU TANZANIA ANAELEWA LINAMAANISHA NINI PUNDE ANAPOLISIKIA LIBADILISHWE NA KUPEWA JINA LA KIGENI AMBALO NAFIKIRI KAMA UKIFANYA UTAFITI NCHINI KWETU NINA UHAKIKA SI ZAIDI YA ASILIMIA 5 YA WATZ AMBAYO WATAELEWA MAANA YAKE... sasa ni nini tena kimembaki nchini mwetu cha kwetu kwa lugha yetu? manake hata majina ya mitaa na barabara yote yamebadilishwa kutoka kwa mf MT unyamwezi kwenda Unyamwezi street, BR bibi titi kwenda Bibi Titi road, sasa Je kuna ulazima gani ?? mimi siku zote nilikua na majivuno ya nchi yangu ndio pekee ktk Afrika ambapo tunatumia lugha yetu kwa kila kitu sasa kuna nini kimebaki cha kujivunia... naombeni msaada ktk hili labda kuna mtu ana mawazo yenye akili kuhusu sababu za kukifuta kisahili kisirisiri...