Kwa nini lakini?

Kijakazi

JF-Expert Member
Jun 26, 2007
6,407
8,899
Leo hii nimesoma kuwa raisi kikwete amefungua rasmi TBC tanzania broadcasting corporation, badala ya Television ya Taifa (TVT), swali langu humu ambalo labda kuna mtu anafahamu jibu lake ni kwamba ni KWA NINI JINA LA TVT AMBALO NI LA KISWAHILI NA KILA MTU TANZANIA ANAELEWA LINAMAANISHA NINI PUNDE ANAPOLISIKIA LIBADILISHWE NA KUPEWA JINA LA KIGENI AMBALO NAFIKIRI KAMA UKIFANYA UTAFITI NCHINI KWETU NINA UHAKIKA SI ZAIDI YA ASILIMIA 5 YA WATZ AMBAYO WATAELEWA MAANA YAKE... sasa ni nini tena kimembaki nchini mwetu cha kwetu kwa lugha yetu? manake hata majina ya mitaa na barabara yote yamebadilishwa kutoka kwa mf MT unyamwezi kwenda Unyamwezi street, BR bibi titi kwenda Bibi Titi road, sasa Je kuna ulazima gani ?? mimi siku zote nilikua na majivuno ya nchi yangu ndio pekee ktk Afrika ambapo tunatumia lugha yetu kwa kila kitu sasa kuna nini kimebaki cha kujivunia... naombeni msaada ktk hili labda kuna mtu ana mawazo yenye akili kuhusu sababu za kukifuta kisahili kisirisiri...
 
Kijakazi, ulikosea sana kufikiri hivyo......
 
Kijakazi hata hujakosea,kwa nini lakini na mimi nauliza.Au Bush katulazimisha kubadilisha jina.Ni nini madhara ya kutumia TVT na ije TBC ni nini kimeongezeka.
 
Leo hii nimesoma kuwa raisi kikwete amefungua rasmi TBC tanzania broadcasting corporation, badala ya Television ya Taifa (TVT), swali langu humu ambalo labda kuna mtu anafahamu jibu lake ni kwamba ni KWA NINI JINA LA TVT AMBALO NI LA KISWAHILI NA KILA MTU TANZANIA ANAELEWA LINAMAANISHA NINI PUNDE ANAPOLISIKIA LIBADILISHWE NA KUPEWA JINA LA KIGENI AMBALO NAFIKIRI KAMA UKIFANYA UTAFITI NCHINI KWETU NINA UHAKIKA SI ZAIDI YA ASILIMIA 5 YA WATZ AMBAYO WATAELEWA MAANA YAKE...

Huyo boss si alikuwa BBC kwa muda mrefu tu.
Mimi nadhani amecopy na kupaste alichofanya sana sana ni British ikabadilika na kuweka Tanzania... kamaliza kazi yake hapo mkurugenzi
 
Jamani sio ninyi tu hata mie nimeshangaa yaani tulizoea neno TVT na RTD sijui tutaanzaje kujing'atang'ata na hilo neo TBC1 na TBC taifa yaani maneno hata hayana ladha.Huyu Tido naye kichwani nadhani kateleza kitu yaani kwakuwa UK kuna BBC1 na BBC 2 na yeye kaamua kutupiga changa kidogo eti TBC 1 halafu TBC2 ndio ipi na TBC Taifa ndio ipi bota hata angesema basi TVT sasa itaitwa SUT,yaani shirika la utangazaji Tanzania.AU hata wangeacha TUT ilikuwa bomba tu
 
TBC ilikuwepo miaka ile, na lugha ya kiingereza bado ni rasmi katika shughuli za kiserikali ingawa lugha ya taifa ni kiswahili
 
Back
Top Bottom