Kwa nini kuleta watoto kuteseka, Una haraka gani?

pakamwam

JF-Expert Member
May 28, 2013
516
651
Nianze kwa kusema pesa ni sabuni ya roho. Usipokuwa na pesa hata roho yako inakuwa chafu.
Pia pesa ni jawabu la mambo mengi sana. Kamwe usidharau pesa wala kuibeza.

Uzi huu inajikuta sana kwenye utamaduni wetu. Jamani mimi nasikitika sana ninapoona mtu anatekeleza au kukataa mtoto. Hata kama mkeo atachukia mwambie ukweli tu. Hakuna laana mbaya kama kuacha damu yako mwenyewe iteseke wakati wewe unakula vizuri.

Pia kwa vijana, sio hekima sana kuharakia maisha. Oa na leta watoto wakati unaweza kuwapa maisha angalau yanaishika.
Mara nyingine watoto wanaharibiwa kutokana na mipango yetu mibovu. Kesi nyingi za watoto kulawitiwa itazikuya maeneo yenye misongamano mikubwa kama Buguruni, Manzese, Mwananyamala, n.k. haya maeneo yana watu wengi na unakuta mtu ana chumba kimoja na ndio kuweka mtoto na ndugu humo humo.
Tukitaka kushinda umasikini lazima tujifunze kuwalea watoto wetu vizuri na kwenye mazingira yenye staha.

Yakobo alioa pale alipokuwa na ukomavu wa kutosha na mali pia. Ndio maana aliweza kulipa mahali kwa leah na Rebeka. Hakulipiwa mahali.
Musa alipewa mke pale alipoweza kuwa na mali baada ya kuchunga kwa Yesse ambaye ndiye alikuwa mkwe wake. Ni vyema ukajipanga na kuandaa mazingira ya mtoto kuja na kufurahia.
Lakini pia unapoleta mtoto ni vyema ujiandae kiakili pia. Ipo mitazamo mingi sana hapa. Katika yote mimi nasema lete mtoto wakati umejiandaa na uko tayari kumpa malezi mazuri.

Umasikini huondolewa kwa kulea watoto vizuri na kuwaongoza vizuri
 
Ushauri mzuri, ila kama wazazi wetu wangefuata huu ushauri wengi wetu tusingezaliwa!
 
Back
Top Bottom