Kwa nini kimya hivyo utafikiri tuna msiba? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini kimya hivyo utafikiri tuna msiba?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Eliphaz the Temanite, Sep 6, 2010.

 1. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #1
  Sep 6, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  CCM wanatumia nguvu nyingi sana kujitangaza! Wamezagaa kila mahali kwenye mitandao!
  Cha ajabu ni kwamba CHADEMA sijui hata kinachoendelea, siamini kwamba CHADEMA hakuna uwezo wa kufanya hivyo! A small digital camera can do a lot. Mnashindwa kuwapatia vijana camera mbila,tatu wakafuatana na mgombea jioni waka-upload pictures hata hata hapa JF. Mbaya zaidi hata kwenye mtandao wa Chama ni kimya utafikiri hakuna campaign.
  Kuna Blogs kibao zinab support kazi inayofanywa na CHADEMA lakini hamwapi!

  Jamani jamani PUBLICIZE your campaigns. Tunahitaji kwenda uso kwa uso na kiki chama cha Majambazi! Wekeni habari pics, viioja na vituko propaganda na kila aina ya mbinu ilimradi tu CCM wang'atuke!
  Flood the internet!!!!!!!!!!
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Eliphaz,
  Nakubaliana na wewe kabisa. We need to do more.
   
 3. Njaa

  Njaa JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2010
  Joined: Dec 6, 2009
  Messages: 970
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 60
  What is your initiatives????
   
 4. Kulikoni Ughaibuni

  Kulikoni Ughaibuni JF-Expert Member

  #4
  Sep 6, 2010
  Joined: Dec 12, 2007
  Messages: 234
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 60
  Mkuu nakubaliana nawe 100% na sina cha kuongeza.Tatizo ni kwamba hata ukiomba utumiwe habari kwa ajili ya kusambaza ujumbe,hakuna majibu.Nadhani pamoja na kazi nzuri wanayofanya Chadema katika duru za siasa,kuna mapungufu makubwa kwenye idara ya uenezi (PR).


  Anyway,tunaendelea kutoa sapoti hivyo hivyo but wanapaswa kujirekebisha.
   
 5. D

  Dopas JF-Expert Member

  #5
  Sep 6, 2010
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nakubaliana nawe mkuu. Nimeudhiwa sana na picha za wapinzani anazoleta Michuzi, ebu wewe linganisha na anazowaletea JK na CCM kwa ujumla. Hivyo kweli Chadema hatuna wapiga picha kabisa wa kufuata msafara wa wagombea wetu: Urais, ubunge na hata udiwani?
   
 6. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #6
  Sep 6, 2010
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  PR machine ya Chadema ni kama mfu.Hivi hawajui kuwa picha moja inaweza kuwakilisha maneno elfu na ushee?Sasa ziara za kampeni za Slaa huko mikoani hatuonyeshwi picha wala video za "nyomi".Hao Tanzania Daima mtandaoni wanasuasua na updates.
   
 7. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #7
  Sep 6, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Tatizo watu wanaendekeza umbeya na mambo ya kipuuzi tu, kampeni kwanza bana....inakuwaje mabango ya CCM yapo mpaka misituni mpaka kwenye blogi za "wakubwa",yanafikaje...mbona wapinzani kimya tunaendekeza mipasho na mambo ya kijinga tu...sijuwi kaowa, kakamatiwa, kafumaniwa, upuuuzi mtupu....nimevunjwa moyo na kampeni za mwaka huu..wenzetu bara mnaturudisha nyuma...mnacheza ngoma ya siasa kama wanavyopiga CCM bana, hamshituki kama hawa watu wanawapotezea mda na Oktoba hiyo apo imefika, mkitanabahi mshachelewa. Ajabu kuna watu miili mikubwa humu akili chache, wamen'gan'ngania tu "wajibuni tu"...aagh!
   
 8. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #8
  Sep 6, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Nilishawahi kuuliza hili suala huko nyuma lakini hakuna aliyejibu. Siku chadema walipofungua kampeni pale jangwani kulikuwa hakuna update yoyote kwenye tovuti yao. It was as if nothing happned. Nimeangalia tena hivi punde na habari mpya ni ile ya 12 Julai 2010 - Sabodo aichangia CHADEMA milioni mia moja. Hakuna picha, no video. Mpaka Michuzi aweke ndio wengine tu-copy. Michuzi asipoweka, na hapa kweupe. It is a shame. Jamani Chadema jaribu kuwafuata wapiga kura huko waliko. Chadema isitegemee wapigakura watawatafuta. Hakuna mtu aliye na muda huyo.
   
 9. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #9
  Sep 6, 2010
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Sasa unataka watu wanapoeneza propaganda za uongo wasijibiwe?What if kama uongo huo ukiachwa pasipo kujibiwa uka-assume status ya truth?

  Siasa zetu ni kama futiboli,kuna wakati inalazimu kuiga formation ya timu pinzani kusaka ushindi.Na busara zinatuusia kuwa sometimes offence is the best form of defence.
   
 10. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #10
  Sep 6, 2010
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 315
  Trophy Points: 180
  Hao CHADEMA ndio sisi. We want our country back. CHADEMA wanaongoza lakini hatuwezi kukaa pembeni tukasubiri wapigane na hayo manyang'au wenyewe.

  Tupige sisi picha na kuzileta huku. Wako wengi wameelewa hilo na wanafanya hivyo. Tuungane nao mkono. Kila anayeweza kuwarushia CCM ngumi afanye hivyo. Tusisubiri CHADEMA pekee ndio warushe makonzi.

  CCM wamehodhi nguvu za serikali siku nyingi, na wanazitumia vibaya kujieneza. Wako watu kibao wanaoogopa CCM kuanguka, kwani biashara zao zinategemea kukingiwa kifua na CCM. Wako poachers, wafanya biashara wa madawa ya kulevya, wakwepa ushuru, na hata wabakaji ambao wanapigana kufa na kupona CCM isianguke. Maana ikianguka wataishia kwa pilato.


  It can be done, play your part. KANU na UNIP zilionekana tishio lakini mwishowe wananchi wa Kenya na Zambia wakazibwaga chini. Zamu yetu ni sasa. Si kesho, ni leo.

  Tafadhali tuache kabisa kusubiri mtu mwingine atubebe. Sisi wenyewe tufanye hayo tunayotaka CHADEMA ifanye. Tupate tu mwongozo toka kwao. Na wao ni sisi. Amen.
   
 11. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #11
  Sep 6, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Sasa wapiga kura watafanyaje wakati wenyewe hawataki kijieneza? Kama ni vigumu kupata informaion za chadema hata kwenye tovuti yao, tutakinadije chama? Publicity ina-matter sana kwenye haya maswala. It can be done, play your part. But how? Wakina nani wanaotakiwa watoe information wanafanya nini na wako wapi? Chadema or wananchi.

  Pia tofautisha upinzani uliokuwa Kenya na ulioko Tanzania. Kenya walikuwa very active and managed to convince the public. Hapa TZ chadema wanajua kabisa kuwa wananchi ni waoga but they doing nothing kuwaondoa woga.
   
 12. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #12
  Sep 6, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana sana na wewe, lakini kumbuka kuwa upigaji wa picha na habari ni 'profession' kwahiyo si kila mtu anaweza kuleta picha ya maana kutoka katika digital camera. Point hapa ni kuwa lazima kitengo cha propaganda cha Chadema kifanye kazi kwa kutumia watu wenye uelewa.Kama walivyosema wengi, kitengo hiki ni butu. PR ni muhimu sana kwa kipindi hiki. Blog na media zipo nyingi sana na wala hazihitaji malipo ni kupeleka news zinatoka. Watu wengi hawapo katika mikutano huko vijijini kwahiyo si vyema kusema '' kila mtu' alete pics au habari. Kutokana na ubutu wa baadhi ya vitengo ndio maana kila hoja anajibu Slaa. Hivi nani anaongoza kitengo cha propaganda and mass mobilization!!!! Kama yupo hapa 'JF' kama walivyo viongozi wengi ajitokeze ''anonymous' ili tumpe michango yetu moja kwa moja.
   
 13. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #13
  Sep 6, 2010
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 315
  Trophy Points: 180
  Jitokezeni kuwa volunteers wa CHADEMA. Kuna aliyejitokeza akakataliwa kusaidia?

  Kuna haja ya mliopo Dar na kweinginepo Tanzania kujitokeza kwenye ofisi za CHADEMA na kujitolea. Kila mtu apeleke kipaji chake. Wataalamu wa It watasaidia kuimarisha website ya CHADEMA. Wabunifu wengine watasaidia kuunda mabandiko na kuyaweka kunakotakiwa.

  CHADEMA haina fedha za wafanyabiashara wakubwa wa madawa ya kulevya na poachers wa wanyamapori wetu kama CCM. Inahitaji nguvu ya wananchi.

  Ask not what CHADEMA can do for your nation. Ask instead how you could join forces with CHADEMA to save your nation from the clutches of CCM.

  Ndugu zangu hawa CCM ni kizazi cha nyoka. Tusiposhirikiana kwa kila hali wataendelea kuitokomeza nchi yetu.
   
 14. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #14
  Sep 6, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Ni kweli tutajitahidi kuipublicize lakini Chadema PR people wake up..!
   
 15. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #15
  Sep 6, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Jambo ni dogo sana! Biashara ni kujitangaza! CHADEMA walipaswa kulijua hilo kabla hata hatujaanza campaign! Haihitaji pesa nyingi kuwa na digital Cameras wakawa wana upload pictures. Sijui kinachokosekana huko CHADEMA, may be walikuwa hawana hili wazo! Kama tumeshindwa kununua magazeti ya Bongo tunadirisha lingine hapa amabalo nonexclusive.

  Tunataka kuona mashambulizi huko kwenye viwanja vya vita!

  Halafu wazo lisingize kuwa kuweka pics tu, watengeneze short video clips zinazobainisha failed promises za CCM moja baada ya nyingine wazipost kwenye youtube! Wafanyakazi Tanzania wote wana internet siku hizi na habari zinasambaa kwa kasi sana kwa njia. Lengo ni kuwavua nguo kabisa CCM na failed promises zao!
   
 16. Mwanamosi

  Mwanamosi Member

  #16
  Sep 6, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NO PR...no business!!!! kama hujitangazi nani atakujua? nani atakununua? kweli PR wa Chadema kama wapo wafanye kazi yao...nasema kama wapo makusudi kwani najua wapo ila kama ni hivyo basi wameshindwa majukumu yao...nawachallenge kuwa wameshindwa kazi na waache wengine wafanye kazi hiyo, ni jukumu lao kuni-prove me wrong kwa kufanya tunachojua PR wanafanya.
   
 17. Mtu66

  Mtu66 Senior Member

  #17
  Sep 6, 2010
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni kweli kabisa
  Ila Nampongeza sana
  Utakapojua Hujui Ndipo Utakapojua
  Kwa juhudi zake
   
 18. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #18
  Sep 6, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Thanks kwa link! Though nguvu zaidi inahitajika kuitangaza kampeni ya Dr Slaa! Tunaomba basi hata kwenye page yake ya Facebook awe anaweka pics mara kwa mara halafu from there zinaweza sambaaa kwa urahisi!

  Kitu kimoja kinanishangaza CHADEMA wana-mabomu mengi kuhusu serikali ya CCM jamani hatuwezi kuiga hata wenzetu wanavyofanya kampeni just a short video clip unakiweka youtube! Can you imagine ujumbe huo utawafikia wangapi! It is easy and effective!
  Chonde Chonde expose them!
   
 19. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #19
  Sep 6, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapo umenena. "Ask not what CHADEMA can do for your nation. Ask instead how you could join forces with CHADEMA to save your nation from the clutches of CCM." Lakini kama Chadema yenyewe hajienezi unafikiri watu watajiunga tuu hivi hivi? Instead of asking how I could join forces with CHADEMA to save your nation, kama mpiga kura i would first ask whether chadema wants me to join forces with them to save your nation. But no where to find such information.
   
 20. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #20
  Sep 6, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Kabisa mkuu. Kwenye tovuti ya CHADEMA kuna link inasema tuunge mkoni. Ukienda kwenye hiyo link unakuta njia mbalimbali za kuiunga mkono Chadema. Mojawapo ya njia za kujiunga ni Kuwa mwanachama wa CHADEMA na kipigie kura CHADEMA. Kuna wengine hawataki kujiunga na vyama. They simply want a change by helping a person or an institution ambayo inaonyesha iko genuine kuleta mabadiliko.

  Njia nyingine ni Tuchangie kwa hali na mali. Chama ni wanachama na uhai wa chama unategemea wanachama. Kumbuka kuna watu wanaotaka kuwa wanachama lakini wakisikia mchango wanagota. Chukulia mfano wa community ndogo ambayo inabidi utoe fee kabla ya kuwa mwanachama. Kabla ya kujiunga, people will fist ask what will I get from the community, not what will I do for the community. Hiyo ni reality.

  Jiandikishe na Upige Kura.
  Sawa but how far Chadema wamehakikisha kuwa wanajieneza ipasavyo ili watu wawe no moyo wa kujiandiksiha? kama nilivyosema huko nyuma hakuna information za kutosha kuhusu Chadema. Yaani ni vigumu kupata information. Inawezekana hii ni kwa sababu ya media zetu zilivyo, but Chadema needs to find a way to get around this.

  Kuna njia nyingine zimeelezwa pale lakini sikuona ya kujitolea. Nina hakika wako watu wengi sana wanaopenda kujitolea kulingana na fani zao. Hata wale ambao hawana fani. Ushindi wa akina Obama na Cameron walitegemea sana volunteers. Tusiwazarau hawa watu. Some just want to help, not to actively involve in politics. Give them a chance.
   
Loading...