Si unaju mbuga za serengeti, mlima kilimanjaro na kisiwa cha zanzibar vimepata watalii wengi sana tangia marekani alipovitangaza duniani kupitia CNN? Hii yote ni kwa sababu ya ujasiri wa raisi Kikwete. Huwezi kuwa na unemployment rate 89% halafu ukakaa nchini bila kuhangaika kule na huku kuwatafutia watu wako uwapendao kazi. Nyumbani mkiwa na ziki kali(ngama), baba anawajibu wa kutembelea marafiki na jamaa kutafuta msaada, sasa kwa kikwete kuona uhaba wa ajira ulivyo mkali hapa tanzania, je afanyeje?
Soko la ajira zuli analo bepari, ndio maana museveni kapeleka majeshi Iraq kunsaidia mmarekani. Ndio maana pakistani inawachinja magaidi kwa niaba ya marekani na ulaya. Ndio maana Jordan kaweka urafiki wa kibalozi na Israel. Unapohangaikia kitu kiitwacho unemployment lazima uwe mjanja kama nyoka na mpole kama njiwa. wewe bepari gani atakusaidia shida zako kama unakwenda ulaya na marekani huku umevaa Chou-EN-Lai ! au manguo yale ya kikomunist ya korea kaskazini?
Umuhimu wa raiasi yeyote yule duniani upo kwenye kufight unemployment maana kazi ni uhai. Kikwete ndie raiasi wa kwanza tanzania kutamka wazi kuwa atacreate jobs kwa raia zake na sio kuwaita wazururaji . machinga complex ni mfano mmojawapo wa kuwawekea economic prosperity raia zake. Tembelea mikoa ya Ruvuma, Mtwara, Lindi na Rukwa, halafu uone kitu kiitwach unemployment kilivyo na kero na kuwafanya watu wengi kufa kabla ya mika 45.
Nyie watu mnao mlaumu kikwete na safari zake, ndie mliokuwa mnashangilia Kifo cha mabepari Tanzania. Hamkujua kabisaa kuwa kifo cha mabepari ni hatari sana katika jamii kwa watu kupoteza kazi na kurudi kuishi maisha ya Ngama.Mihogo, machenga, kipolo cha wali sio vitafunio vya chai, bali maisha ya ngama ndio yanapelekea watu kuishi hivyo kwa sababu ya kutokuwa na ajira.
Kikwete mungu akubariki raiaisi wetu.Ndie wewe shujaa, mwerevu akeshae mwepesi katika kuliona shida la kuwa na idadi kubwa ya wapiga kura wasio na kazi. tembea pia na katika Israel ambako kuna manepari wengi sana wanao outsource kazi nchi za asia na ulaya mashariki.