Kwa nini CCM isiondolewe madarakani 2015?

Landson Tz

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2011
Posts
304
Reaction score
238
Wananchi wengi (80%) ni maskini wa kutupwa ndani ya nchi yetu. Cha ajabu 99% ya viongozi wa CCM ni matajiri!!!
Miaka ya nyuma CCM kilijitambulisha kama chama cha wanyonge (wakulima na wafanyakazi) kikiongozwa na Mwl Nyerer (maskini)
Lakini sasa matajiri ndio wenye chama maskini wanatumika kwa kupewa virushwa vidogovidogo (visenti, kanga, tshirt, chumvi n.k)
Sasa maskini wanaendelea kufunguka kupitia mafundisho ya CHADEMA!
Sasa je? Kama 80% ya waTZ wataamua 2015 nani atawazuia kuiadhibu CCM ( chama cha matajiri) ????????????
 
Ni mtazamo wako huo. Hamna wa kuitoa CCM madarakani. Hiki ni chama mchanganyiko kada zote, imani zote, kanda zote, kuanzia masikini walala hoi mpaka matajiri wakubwa kabisa. Tofauti na vyama vingine ambavyo ni vya matabaka ya watu wa imani fulani au kanda fulani
 
Kwa kuingia Msituni tu sio kwa kupiga kura.
Hao 80% ya waTZ hawapitii humu JF ikikukera zaidi anza kukusanya.AK 47, SAR ndio muziki wake
 
ni mtazamo wako huo. Hamna wa kuitoa ccm madarakani. Hiki ni chama mchanganyiko kada zote, imani zote, kanda zote, kuanzia masikini walala hoi mpaka matajiri wakubwa kabisa. Tofauti na vyama vingine ambavyo ni vya matabaka ya watu wa imani fulani au kanda fulani
wewe usidanganye uma bana!wakuitoa ccm wapo kibao tu watanzania.
 
uwezo huo upo endapo kila mmoja mwenye kuchukizwa na utendaji wa serikali ya ccm ataamua kwa dhati kujenga chama kwa nguvu zote,atakuwa mstari wa mbele kuwakomboa kifikra jamii inayomzunguka,atasimamia ukweli,haki na usawa.na hawa 80% waelimishwe na kujuzwa haki zao na yale yasiyotimizwa waelezwe ni nani anazo na ili kurejeshwa watambue haki zao za kuchaguliwa na kuchagua viongozi wenye uwezo wa kusimamia mikakati yao ya maendeleo.
 
Inahitajiwa nguvu kubwa tena ya kisayansi kuhakikisha ushindi huo unapatikana na si kukaa tu kwa kubweteka.
 
Ni mtazamo wako huo. Hamna wa kuitoa CCM madarakani. Hiki ni chama mchanganyiko kada zote, imani zote, kanda zote, kuanzia masikini walala hoi mpaka matajiri wakubwa kabisa. Tofauti na vyama vingine ambavyo ni vya matabaka ya watu wa imani fulani au kanda fulani

Wewe unajipa moyo maana wanaonufaika na mfumo mbovu unaonufaisha wachache ni wachache sana bahati ya CCM kwa miaka mingi ilikuwa ni uoga na ujinga wa waTZ. Lakini sasa idadi kubwa ya waTZ wamefunguka na ndo maana CCM wamejaa uoga.

Katiba mpya ikiweka mfumo wa free and fair election magamba kwa heri.
 
Sijui kwa nini wasiondoke, ila najua kwa nini waondoke.
 
CCM inawezaka kabisa kuondolewa madarakani.Base ya CCM kubwa ni wazee,vijana hawaisupport kabisa.Ikitaka kuamini hilo,hakikisha vijana wote wanaingia kwenye daftari la wapiga kura,halafu kuwe na tume ambayo sio ya wachakachuzi.CCM inatumia nguvu nyingi kubishana na ukweli.Kwa mtu anayemcha MUNGU aliyehai,atakubali ukweli huu,CCM ya sasa sio ile ya akina Nyerere,imekuwa ni kikundi cha watu wachache waliojilimbikizia mali za uma na uongozi ili kulinda maslahi yao.Mwananchi mnyonge amewekwa pembeni,anajengewa barabara za mikopo ili apumbazike,hasa wazee, angali mapato ya ndani yakikwapuliwa na wajanja.
 
Hiyo tume ya vibabu vistaafu itasoma shule safari hii.
 
Ni mtazamo wako huo. Hamna wa kuitoa CCM madarakani. Hiki ni chama mchanganyiko kada zote, imani zote, kanda zote, kuanzia masikini walala hoi mpaka matajiri wakubwa kabisa. Tofauti na vyama vingine ambavyo ni vya matabaka ya watu wa imani fulani au kanda fulani
Wewe ndio utaitoa CCM madarakani, Wewe, Ritz na Nduka (Sijui yuko wapi siku hizi)
 
Watatoka tu hawana ujanja wana Chadema ni kujipanga tu
 
CCM inawezaka kabisa kuondolewa madarakani.Base ya CCM kubwa ni wazee,vijana hawaisupport kabisa.Ikitaka kuamini hilo,hakikisha vijana wote wanaingia kwenye daftari la wapiga kura,halafu kuwe na tume ambayo sio ya wachakachuzi.CCM inatumia nguvu nyingi kubishana na ukweli.Kwa mtu anayemcha MUNGU aliyehai,atakubali ukweli huu,CCM ya sasa sio ile ya akina Nyerere,imekuwa ni kikundi cha watu wachache waliojilimbikizia mali za uma na uongozi ili kulinda maslahi yao.Mwananchi mnyonge amewekwa pembeni,anajengewa barabara za mikopo ili apumbazike,hasa wazee, angali mapato ya ndani yakikwapuliwa na wajanja.
CCM bado inafanya vizuri ndo maana haijaondolewa madarakani. Na kwa sasa jinsi vyama vya upinzani vinavyozidu kupiga mayowe na kuibua ufisadi ndivyo inavyoendelea kukua na inazidi kuimarika na kulenda maendeleo zaidi.
Sidhani kama ni busara kuondoa ccm sas hivi madarakani.
 
Kaka umesha ingiza siku kwa nape
 
waTZ wenyewe pamoja na wanaCCM (grass root) wajumuike kutokomeza CCM ambayo sasa ipo kwa ajili ya Mafisadi na baada ya kusimika umaskini wa kutupa kwa asilimia kubwa ya waTZ.
 
Back
Top Bottom