Kwa nini ccm isiniruhusu nigombee udiwani, ubunge & urais kwa pamoja?

May 21, 2011
33
11
Kwa mujibu wa Katiba ya sasa ya Tanzania (ILIYOTUNGWA NA CCM) ya 1977 na sheria za uchaguzi mTanzania anaruhusiwa kugombea ama udiwani, au ubunge, au udiwani na ubunge kwa pamoja au urais. Mtanzania hawezi kugombea udiwani, ubunge na urais kwa wakati mmoja kama ilivyo kwa Kenya, Marekani na nchi nyingine nyingi zenye demokrasia ya kweli. Swali ni je, kwa nini tusigombee nafasi hizo kwa pamoja?

Suala hili ni muhimu sana hasa wakati huu wa mjadala wa Katiba mpya. Mawazo finyu ya CCM ni kuwa, kama ilivyo kwa mgombea binafsi ,hili litadhoofisha chama chetu kwani viongozi wa vyama pinzani kama Dr SLAA na LIPUMBA watapata mwanya wa kuingia bungeni, yaani CCM inawaadhibu wapinzani wanaothubutu kugombea urais na kuipinga CCM kwa kuwanyima nafasi ya kuingia bungeni. Jambo hili linaminya demokrasia nchini kwani kama Lipumba, SLAA, MTAMWEGA nk wangeruhusiwa kugombea urais na ubunge na udiwani kwa pamoja; sasa hivi tungekuwa nao bungeni wakichangia kwa nguvu zote kuijenga Tanzania yetu. Lakini wapi, hawako bungeni.

Swali jingine ni je, kutatokea nini iwapo mgombea atashinda udiwani, ubunge na urais? Jibu ni kuwa yeye mwenyewe atachagua kupitia TUME YA UCHAGUZI ni ktk nafasi gani, je ni ktk urais au udiwani au ubunge, angependa kuwatumikia waTanzania. Kama akichagua urais basi, ubunge na udiwani vitakuwa wazi na taratibu za kuziba nafasi hizo kwa mujibu wa SHERIA NA KATIBA zitafuata. WAMAREKANI wanafanya hivyo, kwa nini nasi tusifanye hivyo? Obama na Biden walishinda urais na umakamu wa rais, pia wote walishinda na useneta. Nafasi zao za useneta zilizibwa kwa mujibu wa sheria zao. Kwa nn nasi tusifanye kama wao, mbona kwenye umakamu wa rais tunafanya kama wao?
 
Unachekesha kweli.
Kwani huyu wa ccm akikosa urais anakuwa nani? si kama agombea wa upinzani?
Halasi si kila kitu lazima uige marekani. Tanzania ni nchi huru yenye taratibu zake na watu wake wanajitosheleza kimawazo. Binafsi sioni umuhimu wa hii thread yako hapa.Unatujazia serve tu.
 
Sometimes we put bogus articles... as you know not only CCM won't let U even if they are called Chama Cha Mafisadi; all over the world you cannot be able to be a candidate on more than one elected position...

Freedom in general may be defined as the absence of obstacles to the realization of desires and not otherwise a candidate greadyness.

Please as a Jamii Forum member please put a constructive articles to benefit us all ...
 
Kwangu mimi naona kama ni dalili ya ULAFI tu,
chagua moja kati ya Urais, Ubunge ama Udiwani, ukipigwa chini kajipange,
kama ulikuwa unagombea nafasi ya juu zaidi i.e. Urais, uchaguzi ujao rudi chini i.e. ubunge au Udiwani, kama vipi gombea tena
Na kama ulishindwa udiwani, pambana
 
Back
Top Bottom