Kwa Nini 0 and 1?

JAYJAY

JF-Expert Member
Oct 31, 2008
7,924
8,174
Kwenye masuala ya digital wenyewe wanadai taarifa zinakuwa katika mfumo Wa 0 na 1 tu.

Sasa wadau hii inakuwaje maana vyombo husika ni vya kielektroniki na taarifa zinasafirishwa kwa mfumo Wa umeme!? Hizo 0 na 1 zinaibukaje!?
 
mkuu binary code hizo 0 na 1 zipo siku nyingi ila kwenye computer alizileta konrad zuse mjerumani alietengeneza computer ya kisasa ya kwanza ukimsoma huyu jamaa utaelewa kwanini watu wanatumia hizo namba

kunakuwa na switch za on na off kwenye memory ikiwa 0 ni off na ikiwa 1 ni on

binary-number-switches.png

hivyo technology yetu ya sasa tumeishia hapo kwenye switch 2 inategemewa mpaka kwenye quantum computing ndio wataongeza hizo switch.

angalia switch za conrad kwenye computer yake ya kwanza

Z1-Closeup-c.jpg
 
Binary codes inamaana katika katika umeme kwanza originally huwa ni ANALOG (CONTINOUS SIGNAL) wakiifanyia sampling (kuikatakata kwenye fixed intervals) na kumodify hiyo sampled signal ndo tunapata 0&1 ikiwa na maana kwamba namba 0 ni sawa na NULL VOLTAGE yaan instant ambayo kunakuwa hakuna volts na namba 1 inawakilisha fixed volts fulani let's say 5V physical implication ya hii ni kwamba kwenye Binary codes ni EITHER TV YAKO INAONESHA PICHA YA QUALİTY 100% İKİWA NA MAANA 1 AU HAIONYESHI CHOCHOTE İKİWA NA MAANA 0 hakuna nusu nusu (chenga chenga) kwenye digital ITS EITHER 100% OR 0% hakuna quality ya 40%,60%nk cjui kama nimejibu vzr kiswahili ni Jipu ujue
 
true

true mkuu
 
Mkuu hii concept ni ndefu sana kuielezea inahitaji somo refu kabisa. Kuelewa jinsi gani 0 na 1 zinaleta picha unaziziona, au maandishi unayosoma sio kitu kidogo. Ningekuelezea mambo mengi sana ila tutajaza vitabu, kwa leo ngoja nikuelezee kitu kidogo tu ambacho ni rangi unazoona kwenye monitor maana hata zenyewe ni computer ndiyo inayotuma signal kwenye monitor kudisplay na hiyo nayo ni 1 and 0 ile ile. Ukitaka kujua kiundani zaidi subiri nitakapoanza youtube series weekend hii kufundisha programming kwa kiswahili ntakua nagusia na hizi concepts.

Tuanze chini kabisa:
Rangi nyeupe siku zote inatokana na muunganiko wa rangi tatu, red, green na blue (RGB) kama umeshawahi chokonoa monitor utakua ushawahi kutana na neno RGB. Sasa kwa kawaida ukichanganya red,green na blue kwa amount sawa utapata nyeupe, na kumbuka ndani ya hizi rangi tatu ukichanganya unaweza pata rangi zote unazozijua wewe.

Monitor yako kuna kitu kinaitwa resolution, unavosikia 720p,1080p,4K... monitor resolution ni idadi ya pixels zilizopo kwenye monitor, mfano 720 = 1280 x 720 maana yake width (upana) unakua counted kama pixels 1280 na height (urefu) kama pixels 720. Hizi pixels ni taa tu ndogo sana ambazo kawaida zina taa zenye rangi red,blue na green, ili pixel moja itoe mwanga mweupe maana yake itachanganya rgb sawa, utapata nyeupe, ili zionyeshe nyekundu zitaweka red kua maximum alafu zitazima blue na green.

Sasa picha inavyotunzwa kwenye computer inatunzwa kama namba, kila pixel moja iliyopo kwenye ile picha inakua na namba yake, kawaida red, green, blue zote zinaanzia 0 hadi 255. Sasa mfano wa picha moja tuseme inaresolution 1x2 yaani upana 1pixel urefu 2 pixels. Computer itaitunza hivi

r-255, g-255, b-255
r-0 , g-0 , b-0

notice mstari ya kwanza rgb zina value sawa ya 255 maana yake pixel ya kwanza ni nyeupe, mstari wa pili zote ni 0 maana yake pixel ya pili ni nyeusi. Ikidisplay kwenye screen yako utaona picha yenye rangi nyeupe juu na nyeusi chini.

Sasa 0 na 1 zinaingiaje hapa, 0 na 1 unaweza kuzigeuza zikarepresent namba, mfano 0 ikawa 0, 1 ikawa 1, ila ukitaka kupresent mbili itabidi urudi 10, tatu - 11, nne- 100, tano 101. Kama ambavyo wewe unahesabu 0-9 alafu unaanza 10 then unarudi 11-19, na hii binary representation ni hivyo hivyo sema yenyewe badala ya kufika mbili ukifika 1 unaanza tena 0.
kwa hiyo kamba hiyo namba 255 ya kawaida kwenye binary ni 11111111.

Sasa computer imetengenezwa kwa transistors ndogo ndogo nyingi bilioni kadhaa, hizi transistors ni switch tu, na kumbuka switch siku zote ni either iko off au on. Sasa hii off ndo tunaichukulia kama 0 na on kama 1. Kwa hiyo zikijipanga kama 10 - sisi kawaida tunaassume ni namba 2. Hiyo concept ndio basic kabisa, tunachofanya ni kurepresent kila kitu kama namba, kuanzia picha, maandishi na kila unachokiona kwenye computer, hata simu ni computer kumbuka zote zinarun kwenye principle hii hii pamoja na programmable electronic devices zote.

Mkuu haya maneno ni mengi kuyaandika hivihivi bila proof reading ya editors kama wanaoandika vitabu yanaweza kua magumu kueleweka kidogo, ni rahisi kuyaelezea kuliko kuyaandika. Hope utakua umepata kitu, kama ni mvivu wa kusoma basi mwingine atakua kasoma na imemsaidia
 
duh! unahitaji lecture kbs!

Ila its the easist way of counting(transmiting information) ndo maana computer iko fast zaidi ya binaadamu
 
Somo limenipa mwanga. Ningekuwa hizo binary counting sizijui nisingepata kitu kabisa.
 
Back
Top Bottom