Kwa ninavyoelewa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa ninavyoelewa

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Graph Theory, Nov 27, 2011.

 1. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #1
  Nov 27, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,129
  Trophy Points: 280
  Kuna post katika jukwaa hili inayoulizia juu ya chimbuko la majina ya siku, nami leo nimeona nieleze japo kwa ufupi kuhusu baadhi ya miezi.
  1. Kuhusu mwezi wa kwanza kuwa na jina linalofahamika kama january, katika historia za ulimwengu kulikuwa na utawala wa kirumi, ndani ya utawala huu kulikuwa na mungu waliyekuwa wanamuabudu na alifahamika kwa jina la YANU, huyu mungu alikuwa ametengewa siku maalum ya sherehe katika mwezi mmojawapo katika mwaka, na ilikuwa inafanyika katika siku ya kwanza ya mwezi ulioamuriwa. Katika harakati za kutengeneza gregorian callender waliamua kumuenzi huyu mungu wao kwa kuingiza sikukuu ya kumuabudu huyo mungu wao katika hiyo callender na ikabidi iendelee kubaki katika siku ya kwanza ila jina la huo mwezi likabadilishwa na kupewa jina lililofichwa kidogo likiwa ni jina la mungu yanu yaani y i ka be replaced by j na kuwa janu, then ikaongezewa herufi tatu ambazo ni ary na hapo ndipn tunapata jina january.
  2. Kwa upande wa mwezi wa pili nitaunganisha pamoja na miezi ya saba na nane. Ikumbukwe ya kuwa mwanzoni miezi yote katika mwaka ilikuwa na siku 30 tu. Sasa ilikuwaje mwezi wa pili uwe unaotaneti siku mara 28 na wakati mwingine 29?
  Jibu ni kama ifuatavyo.
  Katika ufalme huo wa kirumi kulikuwa na kaisari aliyefahamika kwa jina la Julius, lakini aliamua ya kwamba ni lazima afanye jambo ambalo litamfanya asisahaulike katika vizazi vilivyofuata, naye aliamua kuita mwezi mmojawapo katika mwaka kwa jina lake, ila pia alikusudia kuufanya huu mwezi uwe wa tofauti na mingine kwa hiyo akaamua kuchukua siku moja ya mwezi wa pili na kuileta katika mwezi aliouchagua na hivyo akauacha mwezi wa pili ukiwa na siku 29, na mwezi aliochagua mwezi wa saba kwa leo ambapo alifupisha jina lake kutoka Julius na kuwa July ambalo ndio jina la mwezi wa saba kwa kimombo, ile siku ukijumlisha na 30 inafanya jumla ya siku katika mwezi July kuwa 31. Kuhusu mwezi wa nane alikuja kaisari aliyefahamika kwa jina la Augustus, huyu naye alikusudia kufanya jambo kama alilofanya kaisari Julius, naye akaufata mwezi wa pili akachukua siku moja na hivyo kuuacha mwezi wa pili ukiwa na siku 28 na akachagua mwezi unaofuata baada ya ule aliochagua mtangulizi wake na hivyo akauita kwa kufupisha jina lake kuwa Augost na jumla ya siku kuwa 31 na ili kuwaenzi hawa watawala wakaamua kurotate jumla ya siku katika mwezi wa pili, kwa kuweka utaratibu wa kupisha miaka mitatu yenye siku 28 katika mwezi wa pili ikifuatiwa na mwaka mmoja wenye siku 29 katika mwezi wa pili. Na hii ndiyo sababu mwezi wa saba na nane ni miezi pekee inayofuatana katika mwaka yenye siku 31. Ukifuatilia kuanzia mwezi wa kwanza mpaka wa sita ukipata mwezi wenye siku 31 unaofuata una siku pungufu ya 31, vivyo hivyo kwa miezi ya tisa mpaka wa kumi na mbili. Handsome wa mama nawasilisha, kama kuna mwingine anayefahamu zaidi uwanja ni wako.
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Nov 27, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  nzuri na ngumu kumeza. Asante ma maelezo mafupi na ya kina.
   
 3. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #3
  Nov 28, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,701
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  ahsante kwa kushea. Nalog off
   
Loading...