Kwa niliyoyaona Burundi, itoshe kusema Tanzania ni nchi tajiri sana

KENGE 01

JF-Expert Member
Mar 12, 2021
1,592
3,839
Kwenye "kusaka tonge" Nimejikuta mara kadhaa nadondokea kwenye nchi jirani ila hii nchi ya BURUNDI inanifanya kila siku nizidi kuthamini na kuipenda TZ..Burundi ni nchi ambayo imepitiwa na Bonde la UFA "Rift valley" sasa sijui ni geographical area ndo inasababisha umaskini huu au ni nini? Lakini mbona Rwanda Nao ni nchi ndogo tena walikua Level moja kiuchumi miaka kadhaa ila Leo Rwanda iko mbali sana.

MIUNDOMBINU:
Barabara ya TZ ni nyembamba ila ya Burundi ni nyembamba Pro max na inamabonde,Mashimo,Kona na miinuko ya kufa mtu.Ajali ni kila siku tena zinaua kuliko za bongo.Mbaya zaidi wanatumia protocol ya barabara(Left na Right) kinyume na hii yetu hali ya kuwa magari mengi ni (Right hand)Kwaio kuovertake mpama utokeze mzimamzima kuchungulia hapo ndo msala unaanzia.kifuatacho ni INNALILLAH..BWANA ALITWAA..RIP

USAFIRI:
Burundi inamikoa zaidi ya 7 ila Airport iko moja tu nchi nzima (BUJUMBURA tu)..Usafiri wao sanasana ni TAX(probox mchomoko) bodaboda na Baiskeli ndo za Kumwagaa....!!!

MAMBO YANAYONISHANGAZA:

~Sio waislamu wala christians Burundi watu ni wafia dini yani wanajua na wanapenda dini balaa makanisani panajaa miskitini panajaa.Naamini dini zetu zinachangia pakubwa sana kwenye umaskini hapa Mzungu na Mwarabu walituweza washenzi wale...!!!

~Elimu HONGERA kwa Sekta ya Elimu ya TZ japo mtaala ni mbovu ila kwenye uniform TZ ilipatia sana..Haiwezekani wanafunzi wa Burundi sketi hazijawekewa Marinda yani zinachora shepu na vitoto vya sikuizi miaka 14 tu shape hiyoo.Watu kama KENGE tunapata tabu sana Wakuu..pia hata KENYA vyanafunzi vinavaa sketi fupi mno sijajua kwa UG na Rwanda.

Burundi wanapata sana Scholarship za France kwakua ni Colon lao..Elimu ni kuanzia la kwanza mpaka 13-16...

~Burundi hakuna Vivutio vya Utalii wala Mbuga za wanyama.Cha zaidi ni (Game reserve) Kinachoniuma kwenye Geography tulisoma Maeneo yaliyopitiwa na Rift valley yanaasilimia kubwa kutoa milima mirefu kama Oldonyo Lengai,Everest n.k Lakini kwa Burundi Hakuna Mlima hata mmoja wa kivutia cha utalii licha ya kuwa na miinuko,Mabonde nchi nzima

Cha kusikitisha kuna Ziwa Tanganyika ila Hakuna Mamlaka ya maji kama DAWASCO kwa TZ yaani kifupi kuna mgao wa maji hasa kule RUMONGE mkoa mzima umepakana na Ziwa ila kuna shida kubwa sana ya Maji Umeme ndo usiulize.

Mziki wanasikiliza wa TZ na Maeneo kama Rumonge wanaongea kiswaili vzuri kabsa ila Bujumbura ndo kuna baadhi wanaelewa kiswahili licha ya kuwa lugha mama ni Kirundi lakini asilimia kama zote wanabonga Kiswahili

Burundi ni nchi pekee unayoweza kusema wewe ni Tanzanian na wakakushobokea..Yaani pamoja na kwamba Nina ngozi ngumu kama ya KENGE na Sura mbaya kama Lori la Mchele kule Mbeya...Lakini huku kwa warundi nikisema tu mimi M-TZ basi watoto wananishobokea balaa kiasi kwamba wanavuka mpaka na kuniita (Hensam boi) Hapa ndo nikashtuka..Nenda Kenya sasa Useme wwe ni m-bongo uone wanavyokudharau...!!

Pia,Nilichogundua Bongo machokoraa wa stendi ni wasafi kulinganisha na wa Burund...Choko wa Burundi wanajua kuomba aisee hawakuachi na ni vichafu kinoma ukijumlisha Udongo ni mwekundu maeneo mengi basi vinakua vichafuu,,vyeusii..Mungu atuepushe na Umaskini aisee lakini Awezi kutuepusha kama sisi wenyewe tumebweteka kusubiri wazungu watutengenezee kila kitu.

Vilevile Ukitembea jiji zima hakuna nyumba iliotengenezwa kwa Tofali za Block..ni mwendo wa (Tofali za Choma)

Nchi kama hizi Chakula sio shida kwasababu uti wa uchumi wetu ni Kilimo kwaiyo vilevile Burundi Wanakima kila kitu na Kufuga kwaio nyama na Maziwa ni kama zote..Wana Ugali wao wa Roi umetengenezwa kwa Mihogo bongo inabidi tuutumie ni mzuri kwa Afya japo ukiskia unavyotengenezwa unaweza kuhairisha/Kususa kula..

Screenshot_20230501-224356_1.jpg

~VYUO VIKUU vinapatikana Bujumbura tu
~AIRPORT ni moja tu nchi nzima
~FARANGA haina thamani kabsaa ukichange 100k Tsh kuwa Faranga wewe ni taita..
~Kama wabongo tu wanaamini South kwa Madiba ndo kuna Maisha yani ukifika umetoboa..
~Maeneo mengi vijijini gari likipita wanalishangaa wakubwa kwa watoto

Pamoja na yote BURUNDI wanazaliana balaa sio ajabu kukuta Mzee anawake wawili na kila Mke anawatoto 10+ nafkir ni kwasababuSTAREHE YA MASKINI NI KUDINYANA

Fursa za Ajira kwa wabongo ukija ukosi kabsaa yani kama unataka utoboe mapema ujenge mapema nenda Burundi kama unaakili ya pesa utapiga sana kwasababu bado wako nyuma ya muda

Narudi kuendelea,bado nipo bujumbura
Screenshot_20230501-211032_1.jpg


Zaidi soma>>>
 
Tanzania ni Nchi nzuri kushinda Nchi kibao hapa Afrika sio Burundi pekee..

Shida ya hao Jamaa wa Burundi ni kama Waha ubishi hawawezi kusikilizana ndio maana unaona Kila siku ni kupinduana..

Japo komesha ya ubishi ni Wasomali ,Wana akili na wanafanya biashara wakubwa ila ujuaji mwingi.
 
Tanzania ni Nchi nzuri kushinda Nchi kibao hapa Afrika sio Burundi pekee..

Shida ya hao Jamaa wa Burundi ni kama Waha ubishi hawawezi kusikilizana ndio maana unaona Kila siku ni kupinduana..

Japo komesha ya ubishi ni Wasomali ,Wana akili na wanafanya biashara wakubwa ila ukuaji mwingi.
Umepita kwenye mstari kabsaa Jamaa ni wabishi kinoma hata kwenye ukweli wanabisha tu
 
Waburundi wengi wanakidharau kifaransa na kusema ni lugha ya umaskini.. ndoto zao ni kujua kiingereza. Pia kiswahili chao kimenyooka karibu sawa na bongo. Kiukweli Tanzania kwa sasa ipo kasi sana kulinganisha na nchi nyingi zinazotuzunguka. Bongo naona shida kubwa sana ni umeme. Kwa ukubwa wa nchi na idadi ya watu kiukweli umeme tulio nao ni mdogo mno.
 
Nchi nyingine nasikia ni masikini wa kutupwa ni central Africa. Hapo Bangui makao makuu ya nchi nasikia pako Kama chalinze. Unaambiwa huko watu wanakula kila mdudu Hadi vyura watu wanapita nao
Ila sijawahi fika mie nmesimuliwa tu.
Izo chai sasa..Fika ushuhudie hata mm naskia Zambia Lusaka ni kama Nyuyok ila siamini najitahidi kufika nijionee
 
Izo chai sasa..Fika ushuhudie hata mm naskia Zambia Lusaka ni kama Nyuyok ila siamini najitahidi kufika nijionee
Lusaka hakuna kitu. Magorofa ni ya kuhesabu. Daladala zao bado ni Hiace. Walichotuzidi ni mpangilio mzuri wa mji wao. Mitaa karibu yote inafikika. Sio kama Dar ambapo Manzese, Kigogo na mitaa mingine ya uswazi imejengwa kiholela.
 
Tanzania ni Nchi nzuri kushinda Nchi kibao hapa Afrika sio Burundi pekee..

Shida ya hao Jamaa wa Burundi ni kama Waha ubishi hawawezi kusikilizana ndio maana unaona Kila siku ni kupinduana..

Japo komesha ya ubishi ni Wasomali ,Wana akili na wanafanya biashara wakubwa ila ukuaji mwingi.

Somali yenyewe ipo wapi kimaendeleo? Mbona kila siku wanakimbia nchi yao na kulipuana tu. Huo uhodari wao umewafikisha wapi?
 
Back
Top Bottom