Uganda na Burundi Kujenga Barabara ya Kuziunganisha Kupitia Kagera Kuikwepa Rwanda. Tanzania Tuchangamkie Fursa

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,060
49,744
Nchi za Uganda na Burundi zimekubaliana kujenga Barabara ya kuziunganisha Moja kwa Moja Kupitia Tanzania Ili Kuikwepa Rwanda ambayo imekuwa haiaminiki.

Barabara hiyo ambayo inatajwa kama ya Kimkakati Kwa Nchi zote 3 itaanzia Kobero(Burundi&Tzn Border)-Bugene-Mutukula-Kakagati(Uganda&Tzn Border) itakuwa ni kiungo muhimu Cha Biashara baina ya Nchi hizi 3.

Screenshot_20240117-090723.jpg


Lengo kuu la Barabara hii ni Kuikwepa Rwanda ambayo imekuwa na mizozo ya mara Kwa mara na Majirani zake kiasi kamba haiaminiki tena hivyo kuharibu biashara
Screenshot_20240117-085501.jpg


Nitoe wito Kwa Serikali yetu kuharakisha kujenga Barabara kama hizi za kimkakati ambazo zitanufaisha Nchi kibiashara ikizingatiwa kwamba inapitia Mkoa wa Kagera ambako anatokea Waziri wa Ujenzi hivyo sitarajii akawa kikwazo au Kushindwa ku push mradi muhimu kama huo.

Ikumbukwe Barabara hii inatajwa kuwa itapunguza umbali Kwa masaa 2 zaidi ikilinganishwa na Barabara ya Sasa inayopitia Rwanda ambayo haiaminiki.

Uganda imekuwa Ina push ajenda hii ya kuitenga Rwanda Kwa sababu za kiusalama.Uganda imefanikiwa kujenga Barabara za kuunganisha na DRC Moja kwa Moja badala ya Kupitia Rwanda na kukuza zaidi Uchumi.
Screenshot_20240117-085734.jpg


My Take
Huu ndio Wakati Kwa Tanzania kusimama na kuwaunga mkono marafiki zake wa Kihistoria Uganda na Burundi badala ya kutaka kumfurahisha Kila Nchi.Rwanda itengwe maana inachochea Vurugu hapa Afrika Mashariki waende Kwa wapuuzi wenzao Kenya.
 
Back
Top Bottom