Mchokoo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2015
- 1,179
- 1,579
Wazo langu hili limezaliwa jana wakati wa mjadara wa Kigoda cha mwlimu Nyerere pale mlimani nilipomsikia katibu Mkuu wa CCM ndugu yetu A . Kinana, akiwaambia watawala wetu wawe tayari kukosolewa na kuomba radhi pale wanapotambua wamekosa!
Kwa wafuatiliaji wa mambo ya siasa za nchi yetu watakubaliana nami kuwa; hali kama ile agharabu haitokei pale ambapo mwenyekiti wa chama anapokuwa ndiye huyo-huyo rais wa nchi pia; hata kama kutakuwepo makosa kibao.
Ndipo nilipogundua kwamba kumbe nchi yetu kuendelea na mtindo wa kuwa na rais ambaye pia ni mwenyekiti wa chama kunasababisha tuwe na ombwe kuu la wakosoaji, watu wenye hurka ya Kinana , naam wale wenye nia njema ya kukosoa kwa kujenga.
Watu wanaochangia kuondoa magugu kwa upande mmoja na upande mwingine wakipalilia ngano ili izidi kustawi katika shamba Tanzania.
Hiki ndicho tulichokuwa tukikimiss kwa mda mrefu huko nyuma.
Mimi nimeipenda hali hii kwa kuwa itamsaidia rais yeyote atakayekuwa madarakani kutoka chama chochote cha siasa katika kuliongoza taifa hili.
Kama nawe wapenda karibu.