Kwa mwendo wa Kilometa 50 kwa saa, sidhani kama Tanzania kuna 'Highway'?

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,928
3,225
Najiuliza tu, kama Barabara za highway gari inatembea speed 50 km per hour

Sehemu chache sana gari inapewa 80 kph..

Elimu kwa mpita njia hakuna, Traffic police ni wakusanya mapato

Watanzania wapewe Elimu ya usalama barabarani...Halafu kuwa na adhabu kwa waenda kwa miguu wanaovunja Sheria..mfano kuvuka pasipo na Zebra...Kuvusha mifugo kiholela etc

Kwa speed 50 kph ni kinyume na SADC na pia nchi inarudi nyuma

Wastage of time on road,

Msingi wa HAPA KAZI tu uko wapi kama muda unapotea barabarani

TRAFFIC watoe elimu ya usalama barabarani, hata kwa madreva

Minimum speed iwe angalau 70 na mazimum iwe 120

Sehemu ya mji au kupita kijiji inaweza kuwa 50 kph

Tuache unafiki--Mbona mawaziri wanakimbia na V8 zao?

watu wengine hawana kazi za kufanya, walipa kodi wakubwa etc
 
barabara zako nyingi si za kuendesha speed kubwa kona kibao,milima,miji vivuko vya wanyama miteremko mikali.....na ndiyo maana kwa traffic kudhibiti mwendo imesaidia sana kupunguza ajali zilizokuwa zimezoeleka huko miaka ya nyuma .....kumbe tunaweza kudhibiti ajali.

wenzetu ncha za majuu barabara nyingi si za kupishana utakuta barabara upande mmoja ziko mbili za kwenda tu na upande mwingine ziko mbili za kurudi tu hakuna suala la ku overtake
 
Kwa hiyo hizi barabara hazina viwango vya kuitwa highways...correct?

Je elimu ya usalama barabarani...
 
Highway ya wapi njia nzima zimejaa makazi ya watu wanaojenga kufuata barabata na vibao vya 50
 
Bora hii speed ya 50km per hour isee siku hizi ukisafiri hata presha huna unalala kabisa kwenye basi..

Trafiki hongereni sana kwa kuthibiti mwendo kwa mabasi mmeokoa maisha yetu sisi hatujali hata kam tutasafiri wiki zima kutoka kwenda mwanza ilimradi abiria wote tufike salama tu

sio tutumie masaa 10 kutoka dar kwenda mwanza afu nusu ya basi wamekufa njiani kwa ajali.
 
Kuna aina nyingi sana za barabara, hapa nazungumzia single lanes, double lanes, dual carriages wayes, highway. N. K ili barabara iitwe highway kigezo kimojawapo kinachozingatiwa ni kuwa ile barabara haitwaki kuwa na muingliano na barabara zingne (Street road) yani barabara iwe ni kutoka na kwenda tu hakuna kukunja..
Hizi barabara za highway design speed yake ni kuanzia 80kp/h zngine mpaka 110km/h..Kwa Tanzania hatuna highway..
Speed ya 50km/h inatumika sehemu yenye mkusanyiko wa watu au iliyo na makazi kwa watu especially maeneo ya mijini. Kwa nn iwe ni 50km/h?

Sababu ya kutumia speed ya 50km/h ni kwamba kulingana na utafti uliofanywa hapo zamani(AASHTO) mtu anakuwa na chance kubwa ya kupona akigongwa na gari lililo kwenye speed ya ya 50km/h,speed inapozid kuongezeka na cganceya mgongwaji inazid kuwa ndogo, mfano speed ya 55 mtu akigongwa anakua na propability ya 45% kupona..

Kwa hyo basi speed ya 50km/h imeekwa kwa ajili ya kumlinda muendea kwa miguu, mtumia baiskeli. Hvo tuvumiliane tu..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu nao wamewekewa Zebra ya kuvukia, lakini hawafuati

Wanavuka ovyo ovyo

Sheria iweke ili wavuka ovyo wapigwe fine
 
sheria ya speed' ya 50 si sawa kabisa , inaonyesha watanzania hatuko serious '' na suala la muda. embu niulize swali, hivi kweli mtu ambaye ni dereva kweli speed ya 65 atashindwa kulimudu gari wakati wa dharura ?!! , nasema hivi kwasababu nchi ya jirani wenzetu wanafanya hivyo kwenye makazi afu ni nchi ndogo, sasa kweli mtu atoke MWANZA aende DAR kwa speed ya 50 kweli tuko serious'' na maendeleo, au anatoka sumbawanga anaenda DAR na speed ya 50 kweli tuko serious. angalau iwe 65 maana tatizo la nchi yetu kila sehemu ni makazi sasa mtu ni kama anasafiri kwa speed ya 50 nchi nzima. kitu kingine kiwango cha juu cha mwendo kiwe angalau 90, hizi ni speed ambazo kwa mtu anaekwenda safari ndefu tunamsaidia pia sheria isiangalie upande mmoja tu. speed ya 90 dereva anauwezo mkubwa wa kulimudu gari na hasa ukizingatia kwamba hiyo speed itatumika maeneo yasiyona makazi.
kitu kingine ambacho jeshi la polisi liangalie ni sheria ya ''ku overtake'' juzi kuna lori lilipaki barabari mlimalni, kukawa na lori lingine likashindwa kuli ''overtake'' hili lililo kuwa kwenye mwendo mdogo mlimani kiasi kwamba likasimama kwanza, lilipotaka kuondoka
gari lilianza kurudi nyuma na kuangukia mtoni . hii ni sheria ambayo ni kandamizi na ina madhara sana.
 
Ukiboresha barabara ndiyo kwanza makazi, shule na vituo vya afya vinaongezeka pembeni mwa highway. Sehemu zote hizo yanafuata matuta nna vibao vya 50km/h
Tatizo nchi hatujui tunataka nini. Tafsiri ya highway na faida zake haipo tena. Dar - Mbeya hadi saa tatu usiku wakati zamani njia hiyo hiyo ilikuwa saa 11 mtu keshafika. Huu ni upuuzi. Mwendo wa kobe lakini ajali ziko pale pale.
Chanzo cha ajali si lazima iwe over speeding tu. Kuna magari mabovu mengi sana yapo barabarani. Tushughulike na hilo kwanza.
 
Najiuliza tu, kama Barabara za highway gari inatembea speed 50 km per hour

Sehemu chache sana gari inapewa 80 kph..

Elimu kwa mpita njia hakuna, Traffic police ni wakusanya mapato

Watanzania wapewe Elimu ya usalama barabarani...Halafu kuwa na adhabu kwa waenda kwa miguu wanaovunja Sheria..mfano kuvuka pasipo na Zebra...Kuvusha mifugo kiholela etc

Kwa speed 50 kph ni kinyume na SADC na pia nchi inarudi nyuma

Wastage of time on road,

Msingi wa HAPA KAZI tu uko wapi kama muda unapotea barabarani

TRAFFIC watoe elimu ya usalama barabarani, hata kwa madreva

Minimum speed iwe angalau 70 na mazimum iwe 120

Sehemu ya mji au kupita kijiji inaweza kuwa 50 kph

Tuache unafiki--Mbona mawaziri wanakimbia na V8 zao?

watu wengine hawana kazi za kufanya, walipa kodi wakubwa etc

Barabara za highyway ambazo utawezakuendesha speed zaidi ya100 inatakiwa barabara isiwe na kona kali, na isiwe na milima mikali na kusiwe na watu wanaotembea kwa mIguu au baiskeli au chombo chochote kisichoweza kufikisha speed ya 80 kmh. Na hiyo barabara iwe double line ili iwe raisi kuovertake gari ambalo linakwenda chini speed inayotakiwa. Je barabara hizo tunazo Tanzania ilituweze kuongelea highyway?
 
Habari

Wataalamu wa Tanroads waje...!
 
Back
Top Bottom