kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 8,992
- 17,892
Kwa mujibu wa hizi Sheria mpya za zilizotungwa baada ya ripoti za mchanga wa madini ni kuwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) kwa sasa hana mamlaka ya kukagua migodi tena.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG), Prof. Mussa Assad amesema Sheria mpya ya Madini haimpi ruhusa ya kufanya ukaguzi katika migodi na ameisihi Serikali iifanyie marekebisho.
Aidha, amesema mpaka sasa kuna vyama vya siasa 7 havikuwasilisha taarifa za mahesabu yao.
Pia, CAG amesema madeni ya matibabu nje ya nchi yamekuwa makubwa na yanatishia kusitishwa kwa huduma hiyo, hivyo ameishauri Serikali kulipa haraka madeni hayo ili kuepuka matatizo ikitokea dharura.
My take:
Nashauri hii sheria ifanyiwe marekebisho ili CAG awe na uwezo wa kukagua migodi yote nchini. Mfano ni juzi tu Rais katoka kuzindua ukuta wa Mirerani ambao utalinda madini yasitoroshwe kwenda nje kinyemela.
Hili eneo la ukuta wa Mirerani ni mfano wa maeneo ambayo yalipaswa kukaguliwa na CAG ili kujua tathmini kama wizi wa madini umefanikiwa kudhibitiwa na huo ukuta ama lah.