Kwa mtindo huu, kweli tutafika?

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,063
22,755
jamaa_anakojoa_ferry_Dar_es_Salaam.JPG

Ndio kawaida hapo Magogoni Ferry halafu wanashangaa wanapokimbiwa na samaki. Tuna safari ndefu !!
 
Kiipo kya mangi! In broad day light?! hao wanaotumia hayo maji hapo pembeni hawamwoni au ni norm?
 
Ni kweli safari tunayo ndefu.
Hawa watu wapelekwe vijijini ama wafundishwe nini sasa hapa.
Yani njemba hata haina aibu inakojolea mahala chakula inatoka halafu pambaf mwingine naye yumo ndani ya maji hayo hayo kiaina.
Sasa picha kama hiyo aipate mzungu si justification ya kutawaliwa inaendelezwa?
 
Labda pale hakuna vyoo vya bure jamaa wanaona ni gharama kutoa bati au fisi akakojoe kunako choo. Mamlaka husika ijaribu kujenga vyoo nya free na kuvihudumia si wataongeza kodi ktk samaki hao. Walipie vyoo indirect hii itasaidia kupata vyoo vizuri na vinavyovutia watu kwenda kujisaidia huko. May be ni umbumbu na ujinga kama ni hayo basi kuwekwe ulinzi na atayekamatwa apewe azabu kali ikiwa pamoja na kifungo. Ustaarabu unalazimishwa most of the time. Otherwise apewe muwekezaji wa ndani hilo eneo alisimamie
 
Ndugu zangu kukujoa kwa kuchafua mazingira ni just one thing..Huyu anakojoa mahali chakula(samaki)kinapatikana..Ni dharau na ujinga na sijui nini...Unaweza kuona ni issue ndogo lakini trust me si issue ndogo kabisa hapa....Huyo mtu ama watu hao wameshindwa kuwa oraginzed kudai haki zao ama ni ujinga?
Kwasababu kuwa civilized ni tofauti...Kodi watu wanalipa kwanini wachajiwe kutumia vyoo mahali kama ferry panapoingiza mapato tosha kabisa kuprovide service hiyo bure?
 
Ndugu Mushi,
Ninaamini unafahamu hata sisi wanadamu ni sehemu ya Mazingira; hivyo hata mtu akichafua chakula chako amechafua mazingira.
Hili suala la kulipia huduma ya kujisaidia/choo naona ni suala la jamii kuelimishwa tu, naamini kuwa hata wewe hapo ulipo kama unafanya kazi au unasoma utaniunga mkono kuwa unalipa kodi; lakini ukienda kwenye baadhi ya vyoo vya umma huwa unalipia.
Sie hapa kwetu Tanzania ni vyema wananchi waelimishwe kuwa na huu utamaduni wa kilipia huduma za vyoo maana ni fedha kidogo tu kama TZS 50/= au 100/= ambayo wengi wetu (hasa wafanya biashara) tunaweza kumudu.
 
Back
Top Bottom