Kwa mtazamo wangu!

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
5,565
836
Wakuu uchaguzi wa 2010 ndiyo huo ushaisha. Raisi kasha apishwa na serikali "mpya" inaelekea kuundwa. Pamoja na tuhuma nyingi za uchakachuaji ukweli ni kwamba hii isha pita na hakuelekei kuwa na upinzani wowote wa maana katika kupinga matokeo.

Uchaguzi wa mwaka huu umeonyesha kitu kimoja ambacho mimi na wengine wenye mawazo kama yangu tumeongelea sana humu ndani ya JF. Ili kuwe na mabadiko yoyote ya maana ni lazima katiba ibadilishwe kwanza. Wengi wetu tulio kuwa tuna sema tokea mwanzo kwamba Dr. Slaa pamoja na kuwa chagua bora hato shinda tulionekana watetezi wa upinzani na waoga wa mabadiliko. Ukweli tuliona na tulisha juwa kwamba system iliyopo haiwezi kuruhusu mpinzani ashinde uchaguzi.

Leo hii tuna jiita nchi yenye vyama vingi yani multipartism lakini tuko hivyo kwa jina tu kama ilivyo jina tu kwenye katiba kwamba sisi ni taifa la kisoshialisti wakati tunaendeleza ubepari. Leo hii upinzani kushindana na CCM ni sawa sawa na timu zishindane wakati timu moja kati ya hizo ndizo zinazo chagua refa, viwanja na hata sheria za mchezo wenyewe.

Katika katiba yetu ya sasa tume yote ya uchaguzi ime chaguliwa na CCM. Je tuna tegemea nini hapa? Wakuu wote wa wilaya ambao ndiyo viongozi wakuu wa serikalini ambao wapo karibu zaidi na wananchi (grassroots) wana toka chama cha raisi je tuna tegemea nini?

Ndiyo maana siku zote nawaambia watu. Ili kuwe na mabadiliko ni lazima katiba ibadilishwe kabisa na siyo hali ya sasa ya kupachikwa viraka vya hapa na pale. Mpaka hapo wananchi tutakapo dai kwa nguvu zote katiba ibadilishwe kila siku tutaendelea kuota ndoto za alinacha kuwa uchaguzi ujao utakua tofauti.

Kuna sababu kuu mbili ambazo zinafanya CCM ing'ang'anie kwa nguvu zote katiba iliyopo. Katiba ambayo inadai sisi ni wasoshialisti na wakati kiuhalisia ni kinyume na hapo:

1. Katiba iliyopo inaipa nguvu CCM:
Nisha dokeza kuhusu hili hapo juu. Kwamba tuna mfumo wa vyama vingi lakini katiba ya chama kimoja. Hii inamaanisha kwamba tulipo anza mfumo wa vyama vingi katiba tayari ilikua ina ifavor chama tawala ambacho raisi wao ndiye huchagua wajumbe wakuu wa NEC na chama hicho hicho ndicho kina husika kwenye kuandaa na kuendesha uchaguzi. Je unadhani CCM wapo tayari kuachia advantage hii?

2. Muungano:
CCM inaogopa kwamba pindi tu mchakato wa kuandika katiba mpya itakapo anza basi swala la Muungano ni lazima lijadiliwe na hapa kuna makundi yata taka mabadiliko tena makubwa sana. Wote tunajua CCM ilivyo sensitive linapo kuja swala la Muungano. Wanajua fika katiba mpya ita husisha kuangalia upya Muungano. Wanacho ogopa ni kwamba katiba mpya aidha itaua Muungano kabisa au kubadilisha kabisa sura ya Muungano ambayo wamezoea.

Kwa hiyo wakuu 2010 isha pita. Raisi stahiki kashindwa kwa sababu ya mfumo mbovu unao tokana na katiba iliyo pitwa na wakati. Tusi tarajie kufanya mambo yale yale na kupata matokeo tofauti. Njia pekee ya kuinusuru taifa ni kubadilishwa kabisa katiba na kuiandika upya. Nawasilisha hoja!
 
Back
Top Bottom