Kwa mtazamo wako,hela imepotelea wapi? Kodi hailipwi?

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Pesa haionekani..pesa haikamatiki, na ukiikamata ni kiduchu ,ni ya kuishikilia kweli kweli. Ikikuponyoka tu,kurudi kwake ni mbinde. Hi ni kwa watu wa kada zote, kuanzia watumishi wa umma, wafanyabiashara, wawekezaji, wakulima, wafugaji na hata wale kule mtaani ambao hawajui hata maana ya neno "ufisadi".

Hata ufanye kazi bila kulala mwaka mzima ni sawa na kazi bure. Service au products zako utamuuzia nani kama mtaani manung'uniko ,simanzi haviishi.

Hela inakwenda wapi? Maana watu wanakusanya Kodi,hazionekani. Hatupewi takwimu za nn kimekusanywa, nini kimetumika na kwenye nini. Tunaambiwa makusanyo yanatumika kulipa madeni ya huko nyuma. How?

Kipindi cha JK kweli ajira zilikuwepo, wanasema tulikuwa na deni kubwa lakini mbona watu walikuwa na maisha mazuri? Malalamiko hayakuwa mengi.

Tunategemea kama hela nyingi zinazokusanywa basi watu wangekuwa na maisha mazuri kuanzia huduma za kijamii zingekuwa safi sana.

Dah.
 
Piga kazi ingekuwa haipatikani mama ntilie mbona wapo wanauza kila siku.
Kazaaa kiume
 
Wewe umesombwa na kauli za kiujumla za mitaani.
Pesa kupotea ni kauli iliyowanufaisha sana wajanja wa maendeleo.
Sijui upo mji gani nikutolee mfano.
Tafakari kauli hiyo kwa kufanya utafiti wa kuzunguka mitaani uone jinsi vitu vya maendeleo vinavyokuja kwa kasi ya ajabu!
Watu wanaporomosha majumba kama hawana akili nzuri.
Tena ni mijengo ya kuogofya kuliko hata wakati wa jk.
Watu wanafanya vitu kwa tafakuri ya hali ya juu kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya Tz.
Pesa kupotea mitaani ni kauli inayotolewa na mabwanyeye wenye nazo kuwanyima fursa watu waliozoea vibomu kupanua midomo yao kuomba.
Lakini kiuhalisia, mitaani watu wanakula, wanavaa, wanashereheka, wanahongana na wanajenga "kama kawa"
Sasa kauli yako hii ya pesa kupotea mtaani umeifanyia utafiti gani na wapi?
Kauli hiyo imekuwa nyepesi mno kutamkwa na watu, kama wasalimianavyo shikamoo.
 
Back
Top Bottom