Sisi wananchi waishio kando kando ya barabara ya Nyakato National mpaka Buswelu tulikupa kura za kishindo lakini umetutelekeza kutokana na adha ya vumbi inayotimuliwa na magari takriban 2000 yanayopitia barabara hiyo kila siku kukicha. Watoto wetu wanaugua kikohozi kila siku, Vyakul vyetu vimejaa vumbi kila siku, Mavazi yanachafuliwana vumbi kila siku, Kelele za magari ndiyo usiseme, Biashara zetu wateja wametukimbia. Mama tumekupigia kelele na kukueleza bila mafanikio. Ingekuwa nchi za weupe tungeenda mahakamani na kupata fidia lakini Tanzania hii haiwezekani. Nasikia sasa hivi uko Mwanza, nakuomba upitie barabara hiyo ndo utajua ukweli ninaousema. Tulielezwa kuwa barabara ingeanza kujengwa kwa kiwango cha lami tangu mwaka jana lakini hadi leo hakuna kilichofanyika. Tusaidie Mheshimiwa. Mateso tunayopata yanatisha.