Mhe.Mabula sisi wananchi wa Ilemela tulikuchagua kwa kura nyingi sana tukitumaini utatuletea maendeleo. Mhe.Mabula kero ya barabara ya kutoka Buswelu mpaka barabara ya lami ya Mwanza mpaka Musoma imekuwa kero kubwa kwa wananchi wako kutokana na sababu zifuatazo:-
- Wananchi tunaoishi kando kando ya barabara hii tumeathirika sana kwa vumbi inayotokana na magari yanayopita katika barabara hiyo. Takriban magari 1000 kwa siku yanapita kwenye barabara hiyo.
- Watoto wetu wanaugua kila mara inayotokana na vumbi inayotokana na magari.
- Tulio na biashara tumeshindwa kuendelea na biashara hasa mahoteli na wateja wametukimbia.
- Nyumba zetu zimegeuka vumbi tupu kutokana na vumbi inayotimuliwa na magari.