Mhe. Naibu Waziri wa Ardhi na Makazi na Mbunge wa Ilemela tumekulilia, tumekueleza kupitia mikutano yako na tumekuandikia kuwa wananchi tunaoishi kando kando ya barabara itokayo kwenye kona ya Mwanza - Musoma mpaka Buswelu tuna adha kubwa sana ya vumbi inayotifuliwa na magari takriban elfu moja na mia tano kila siku yanayopita kwenye barabara hiyo.
Tumekueleza barabara iengenezwe kwa kiwango cha lami lakini mpaka leo hakuna kinachoendelea.
Mwaka 2020 siyo mbali na utarudi kutuomba kura. TUNAKUELEZA KWA UWAZI KABISA kama adha hii tunayopata haikupatiwa ufumbuzi basi sahau kura zetu.
Waingereza wanasema ENOGH IS ENOUGH.