Kwa mfumo wa ajira Tanzania, kujiajiri ukiwa umeajiriwa ni ngumu sana na kujiajiri ukiwa huna ajira ni ngumu zaidi! Nini kifanyike?

miamiatz

JF-Expert Member
Dec 4, 2017
504
927
Habari wanajamvi,

UTANGULIZI

Kwa asili ya ajira za kitanzania, ajira ambazo una uhakika wa kupata pesa ya kujikim ila sio ya ziada, ajira ambazo una uhakika wa kubanwa na kazi kwa masaa yote ya kazi, ajira ambazo zinagombaniwa na maelfu ya watu, etc kufikiria kujiajiri huku ukiwa umeajiriwa laweza kuwa bomu la kujilipua mwenyewe kama hukuwa makini.

Kwa asili ya hali za kibiashara Tanzania, ukiamua kujiajiri huku ukiwa huna sehemu unapopata kipato japo kidogo cha kujikimu cha kuajiriwa na ukaanza kuitegemea biashara changa ukilishe, ikuvishe, ikulipie pango, etc, basi kujiajiro huko kwaweza kuwa ni bomu zaidi ya lile la hapo juu.

NINI CHA KUFANYA?

1. Acha kuwaza biashara bali waza kupiga ela

Iwe umeajiriwa ama hujaajiriwa, uwe una mtaji ama huna mtaji jambo la kwanza unatakiwa kufanya ni kuachana na wazo la kuanzisha biashara badala yake anza kuwaza nawezaje kupiga ela. Nani ana ela niipige? Wapi pana ela nikaipige?

Tuelewane lakini sio kupiga ela kwa maana ya kupora, kuiba, kudhulumu, etc no sina maana hiyo. Zipo njia halali za kupiga ela ya mtu. Unamset fresh anaingia 18 zako unapiga ela.

2. Unaanzaje kupiga ela ya mtu huku akiwa amerizika kabisa wala hujamuibia na wala hujamzulumu?

a. Hatua ya kwanza ni kuchagua nani unataka upige ela yake?

b. Hatua ya pili ni kumchunguza anapendelea nini?

c. Hatua ya tatu ni kuchunguza je anapata kila anachotamani kukipata?

d. Hatua ya nne ni kuyaorodhesha yale ambayo unajua jamaa anayapenda ila hana pa kuyapata japo anayamudu.

e. Hatua ya tano ni kumset kwa nguvu kubwa ya ushawishi kuwa jambo flani linawezekana yeye tu akiamua.

f. Hatua ya sita ni kukomaa kumshawishi afanye jambo hilo.

g. Hatua ya saba ni wewe ku bridge the gap kati yake na jambo alipendalo kwa kumtoza pesa ama kwa kumuongezea bei.

ZINGATIA

Kukiwa na watu 10 ambao umepanga kupiga ela zao hao tunawaita leads.

Unaconvert leads ngapi kuwa pesa ni jambo la msingi. Jitaidi ukilenga watu kumi basi wanne usikose.

Ukiufanya huu mchezo kwa muda wa miezi kadhaa kwa mafanikio basi sasa upo tayari kuanza kufanya market research na kuamua biashara gani ya kufanya.

Biashara za kufanya watu hawatafuti mitandaoni kwa kusearch ama kwa kuuliza jf/fb/insta wala twitter. Wanazipata kwa kuwaza wapi pana ela nikapige.

Nawasilisha na nakaribisha michango yenu. Nakaribisha kukosolewa. Nakaribisha kupingwa. Nakaribisha kuungwa mkono. Ila plz sikaribishi matusi, dhihaka wala kejeli. Hapa ni Jamii Forums - The Home of Great Thinkers.
 
Ume-generize tu, toa mfano mkuu usiwe kama wale wanasema “Anzisha idea yako mpya kama rahisi vile.

Sent using Jamii Forums mobile app
Its simple and clear sahau kuhusu kujiuliza biashara gani nifanye na anza kuwaza pesa ya kina nani nikaipige kwa njia gani?

Time travel theory inasema sote tunasafiri ktk speed ya sekunde moja kwa kila sekunde. Anaeweza ongeza speed kidogo tu basi anakuwa ndo mpiga ela za wapigwaji.

Pesa zipo wapigaji tu ndo wachache ila hao wachache wanatupiga haswa.

Ila tambua ili upige lazima umtafute mpigwaji. Ndo mana wanaotembea tembea wana ujuzi mkubwa zaidi wa kupiga ela kuliko wale ambao hawajatembea vya kina.

The more you travel in space and in time the bigger your chances of making money.

Courtesy of miamiatz
 
Mfano Motivation speaker ni wapigaji,wanakushawishi ufanye kitu ambacho wao watafaidika kupitia kwako.
Exactly, huu mfano uko validity kabisa hapa mada imekuwa relevant, hapa nimekumbuka ONTARIO kwenye forex ndio mfano relevant zaidi, hata ile mada ya ONTARIO ya matrekta yaani aliwasoma wabigwaji vyema | chamsingi kuumiza kichwa na kutumia akili utawapata wakuwapiga ila Rule no 1 kwamba wao wenyewe wawe wamerindhia kupigwa kwafaida yao pia.

Hii falsafa nzuri sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata aliekuuzia bundle ya internet unayotumia kuperuzi mitandaoni ni mpigaji tu.

Omba dua hii "Mungu Onesha Njia Wapi Ipo Pesa Nikaipige" full stop mengine waachie wanasiasa.

Courtesy of miamiatz
Yani hutakiwi kufanya biashara ukiwa na njaa yani unategemea ndio ikulishe utaishia tu kula mtaji.
 
Exactly, huu mfano uko validity kabisa hapa mada imekuwa relevant, hapa nimekumbuka ONTARIO kwenye forex ndio mfano relevant zaidi, hata ile mada ya ONTARIO ya matrekta yaani aliwasoma wabigwaji vyema | chamsingi kuumiza kichwa na kutumia akili utawapata wakuwapiga ila Rule no 1 kwamba wao wenyewe wawe wamerindhia kupigwa kwafaida yao pia.

Hii falsafa nzuri sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yani inakuwa win-win,kila mtu anaondoka anafurahi.mfano wanaosema vijana wajiajiri labda kwenye ufugaji,unakuta huyo anaekuambia ufuge amejipanga kukuuzia kitabu cha mafunzo,chakula,madawa na kuku wenyewe.
 
Mungu onesha njia pesa iko wapi nikapige. Full stop. Ilimradi iwe halali basi. Mengine siasa tu.

Courtesy of miamiatz
 
Nimesoma kichwa cha habari tu na ninajibu kwa mujibu wa kichwa cha habari chako.

Kama kujiajiri ukiwa umejiajiriwa ni ngumu basi usijiajiri, baki kwenye ajira tu.

Kama kujiajiri ukiwa hauna ajiri ni ngumu zaidi basi ukiwa hauna ajira usijiajiri pia, baki nyumbani kwa mama unakula na kulala tu. I think i have made my self clear!
 
Poor mind in poor country.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umetoa wazo nzuri sana.Mtu hutakiwi kuwaza sana unachotakiwa ni kuanza hapo ulipo kama ni umeajiriwa unatumia ujuzi ulionao unapiga ela kama hujaajiriwa unajichanganya Na watu unapiga ela.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesoma kichwa cha habari tu na ninajibu kwa mujibu wa kichwa cha habari chako.

Kama kujiajiri ukiwa umejiajiriwa ni ngumu basi usijiajiri, baki kwenye ajira tu.

Kama kujiajiri ukiwa hauna ajiri ni ngumu zaidi basi ukiwa hauna ajira usijiajiri pia, baki nyumbani kwa mama unakula na kulala tu. I think i have made my self clear!
Ni bora umesema umesoma kichwa tu, ni wazi kuwa umechangia bila kuelewa.... kama nia yako ni njema nakusihi kasome tena content. .

Usile Mbegu.
 
Ni bora umesema umesoma kichwa tu, ni wazi kuwa umechangia bila kuelewa.... kama nia yako ni njema nakusihi kasome tena content. .

Usile Mbegu.
Hata nikisoma content, hiyo heading sikubaliani nayo, siyo tu niko tofauti ya hicho kichwa cha habari, bali niko kinyume kabisa, kwangu mimi, " ni rahisi kujiajiri ukiwa umeajiriwa, ila ni rahisi zaidi kujiajiri kama haujaajiriwa"
 
Back
Top Bottom