Kwa mfumo huu wa TRA wengi tutafunga Biashara

ubongokid

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
2,030
3,907
Habari wadau;

Ni hivi;Nilitembelewa na wakaguzi wa TRA ofisini kwangu.Walipofika walianza kuniuliza maswali mengi na nikawapa nyaraka zote walizotaka na kwa mujibu wa Taarifa zangu kodi yangu nilishalipa yaani sikuwa na deni.

Basi baada ya kuona niko safi wakaanza kuniuliza maswali ya kipuuzi.Moja wapo ilikuwa niwaonyeshe risiti ninazowapa wateja wanaponunua nikawapa wakajumlisha sana kisha wakasema mbona kodi unayolipa ni ndogo kuliko mapato yako?

Nikawatazama kwa jicho la dharau kisha nikiwauliza kivipi?Wakanipa maelezo mazuri sana.Nikiwaambia hivi kodi inatozwa kwenye faida au kwenye mapato wakasema kwenye faida basi nikawaulizambona hamjauliza taarifa za matumizi?Wakasema tupatie basi nikawapatia.

Katika matumizi ikaonekana kwa faida ninayopata basi hata kodi ninayolipa nikubwa hivi inabidi nipunguze kiwango cha kodi kwani kwa faida niliyopata ni kama vile tunagawana robo kwa 75.Yaani mimi nabaki na 25 wao wanakula 75% ya faida yangu.

Walipoona hivo wakaanza kukagua risiti zangu za matumizi,kwa kuwa mimi ni mjasiriamali na biashara yangu ni ya kuuza chakula kwa hiyo kiasi kikubwa cha manunuzi yangu hayana risiti kwa hiyo tulianza kubishana sana na hawa watu wakaweka kofuli kwenye ofisi yangu wakitaka niende TRA ofisini kwao.

Kiukweli kutokana na biashara kuwa ngumu na kwa kuwa kodi yangu inaisha mwisho wa mwezi wa pili niliwaambia sawa na walipomaliza kufunga usiku nimeita fundi welding nimevunja lile kofuli lao nimebeba materials zangu zote,kisha nimeenda polisi kufungua kesi kuwa nimevamiwa na majambazi wameiba kila kitu.na niko hapa TRA na RB yangu ya kuibiwa nawaona wanavojichnaganya tu kunitishia huku wakifikiri mimi sielewi ninachofanya.Yaani mfungie masufuria yanu,bakuli,majiko nakadhalika kwa sababu tu mnataka kunikamua.

Kakamueni wake zenu na kama mmechafukwa mnifunge basi ila kodi silipi tena huko ninakoenda naenda kufungua biashara bila kulipa kodi.Huu wizi wizi sitaki tena kufanyiwa nimechoka
 
Saafi! Fanya biashara ndogo mbele ya macho ya TRA na biashara kubwa, nyuma ya pazia. Hawa watu ukiwachekea wanaweza kukufilisi.
Ndio maana mimi nimeachana na biashara zooote. Nimebaki na biashara ya udalali tu.

Kwa biashara hiii, silipi kodi milele, na deni la bodi ya mikopo kawaambie tu wajiandae kulifuta maana there is no way nitalilipa kwa shughuli yangu ya udalali.
 
Hahahahaha......sasa kaa mtu unalipa kodi kuna haja gani ya kufatiliwa
 
Bora wewe mimi nilifuatwa hadi Whassap.. nilikuwa na biashara nimesafiri sasa niliyemwachia akachelewa kupeleka pesa zao.

Wakawa wananipigia hawanipati mwezi uliopita nimekaa nasoma meseji ya TRA nadaiwa kiasi fulani... nikamwambia nimefunga biashara nilifilisika na sitafanya tena.

Kodi ni ugonjwa hasa ukikutana na maafisa ambao ni wanazi.
 
Nchi hii ina mfumo mbaya sana wa kodi za kinyonyaji, manake kufanya biashara nchi hii ni kama kosa la jinai, wanakuekea vikwazo ushindwe kabisa
 
Kiukweli nilisema hapa kama waziri wa fedha hatabadili mfumo wa tra basi wafanyabiashara watafunga biashara zao na serikali itakosa mapato. Binafsi walikomaa na mimi ninunue mashine ya efd mpaka nikanunua lakini kiukweli hata sielewi hii mashine ya efd nafanyia kazi gani.

Asilimia 90 ya wateja wangu ni wa kununua sigara mojamoja, sabuni kipande kipande, miswaki na dawa za jerojero, soda, juice, maji ,chumvi, mafuta ya kupikia ya kupima, sukari ...jaman hapa ndo biashara yangu na efd ninayo. mteja akinunua biscuit ya 200nimchanie risiti? TRA whatch out! You are going to loose businessman
 
Bora wewe mimi nilifuatwa hadi Whassap.. nilikuwa na biashara nimesafiri sasa niliyemwachia akachelewa kupeleka pesa zao.

Wakawa wananipigia hawanipati mwezi uliopita nimekaa nasoma meseji ya TRA nadaiwa kiasi fulani... nikamwambia nimefunga biashara nilifilisika na sitafanya tena.

Kodi ni ugonjwa hasa ukikutana na maafisa ambao ni wanazi.
ati??? Umefilisika?? na hufanyi tena biashara ..sasa hawajafuatilia mahali pa biashara tena?
 
Saafi! Fanya biashara ndogo mbele ya macho ya TRA na biashara kubwa, nyuma ya pazia. Hawa watu ukiwachekea wanaweza kukufilisi.
Ndio maana mimi nimeachana na biashara zooote. Nimebaki na biashara ya udalali tu. Kwa biashara hiii, silipi kodi milele, na deni la bodi ya mikopo kawaambie tu wajiandae kulifuta maana there is no way nitalilipa kwa shughuli yangu ya udalali.
Mimi bodi ya mikopo wakaniuze utumwani Libya kufudia hilo deni ila Sina hela ya kuwalipa
 
Back
Top Bottom