Kwa matukio haya mawili kada mtiifu kwenye mitandao wa CCM, Magoiga unatakiwa kuomba radhi familia 2

Nimesoma andiko la mtu mmoja anayejiita "Magoiga SN" akieleza kuwa eti Roma hakutekwa ila alifichwa ili kumuangushia jumba bovu Bashite. Kwa maelezo yake mpango huo ulipangwa na anaowaitwa "wauzaji wa sembe".

Sikutaka kumjibu lakini kwa faida ta watanzania ngoja nimjibu ili asiendelee kupotosha.

Ili kuweka kumbukumbu sawa, niwakumbushe tu kuwa Ben alipopotea huyu Magoiga alisema ni filamu iliyotengenezwa na Chadema ili kujipatia umaarufu kisiasa. Nilimuonya uache ujinga kwenye mambo yanayohusu uhai wa mtu. Lakini hakusukia. Alipoona anashindwa kudhibitisha namna viongozi wa Chadema walivyohusika akasema Ben kajiteka mwenyewe. Ninazo nakala zake zote za maandiko kuhusu Ben (hata zile alizofuta).

Kubenea alipojitokeza kueleza UONGO kuhusu Ben, Magoiga aliamua kukaa upande wa Kubenea. Akamsupport. Magoiga akatumia nguvu nyingi kuwaainisha watu kuwa yaliyoandikwa na MwanaHalisi ni kweli. UTG waliposema Kubenea anapotosha, Magoiga huyuhuyu akajitokeza na kusema UTG walikua na dili la kuuza tishirt, kwa hiyo Kubenea aliharibu dili lao ndio maana wanampinga.

Baada ya Kubenea kueleza kile alichokiita "Ben kuonekana kwenye vijiwe vya kahawa" Magoiga akasema filamu inakaribia kufika mwisho na Ben atapatikana kutoka huko alikojificha. Leo ni mwezi wa 5 Ben hajapatikana. Unafiki.!

Magoiga huyuhuyu alipoona issue ya Ben ni serious na sio "filamu" kama alivyowaaminisha watu, hakuomba radhi. Badala yake akaanza kujirudi na kusema viongozi wa Chadema hawakuwa serious kumtafuta Ben alipopotea. Yani Magoiga yuleyule aliyesema Ben amejificha, leo anasema Ben amepotea na eti viongozi wa Chadema hawakuwa serious kumtafuta?? Viongozi walewale aliosema wamecheza filamu ya kumficha Ben ndio haohao anaosema hawakuwa serious kumtafuta? Huu ni UNAFIKI wa kiwango cha juu mno.

Sasa hili la Roma nalo ameanza kufanya upuuzi uleule alioufanya kwa Ben. Magoiga aliandika hapa juzi kuwa tuungane kumtafuta Roma bila kujali itikadi zetu za kisiasa. Akasema tusianze kuhukumu Polisi bila kujua wahusika halisi waliomteka Roma. Watu wakashikamana kwa umoja kupiga kelele hadi Roma na wenzie wamepatikana.

Cha ajabu baada ya Roma kupatikana, hata kabla Roma hajaeleza kilichomfika, Magoiga ameshamhukumu. Ameibuka na kusema eti ni movie iliyotungwa ili kumng'oa Bashite madarakani. Yeye anasema "kumuangushia jumba bovu" Akili gani hizi??

Magoiga yuleyule aliyesema tusihukumu Polisi bila kujua wahusika halisi, yeye tayari ameshamhukumu Roma bila kujua wahusika waliomteka. Roma kasema ataongea kesho kueleza yaliyowafika, Magoiga kabla hata hajamsikiliza Roma ameshamhhukumu kuwa eti ni filamu.

Magoiga ana-bore sana kuweka siasa kwenye uhai wa watu? Hata kama anatafuta uteuzi lakini si kwa namna hii. Anadhani maisha ya mtu yana thamani sawa na cheo cha Bashite? Yani cheo cha Bashite kwa Magoiga kina thamani kuliko uhai wa binadamu wenzie? Yani uRC wa Bashite, ni wa maana kuliko maisha ya Roma, Ben etc?? Ndio maana haoni hatari ya uhai kwa watanzania waliotekwa, ila anaona hatari ya cheo cha Bashite kupotea. Lini huyu Magoiga ataacha kufikiri kwa kutumia fuvu?

Kama kutekwa kwa Roma lengo ni kumuondoa Bashite madarakani, vipi watanzania wengine waliotekwa na kupotea?? Tarehe 13/03/2017 kijana Erick Msyaliha alichukuliwa nyumbani kwake Sinza na watu waliojitambulisha kuwa "polisi" na hadi leo hajulikani alipo. Je huyo nae amefuchwa ili kumuondoa Bashite ofisini?? Juzi mkoani Mara mtu mmoja alitekwa na kuuawa kisha kufungwa kwenye baiskeli kama kifurushi na kutoswa majini, je huyo nae alifichwa ili kumuondoa Bashite ofisini?

Katika hili Magoiga ameonesha uwezo mdogo sana aa kufikiri. Has proved to be weak minded, lunatic, empty headed, vacuous, vapid, boring and tedious.

Kuna mambo ya kufanyia siasa lakini si maisha ya mtu. Mwambieni Magoiga aache kabisa huo UPUMBAVU. Afanye siasa kwenye mambo mengine sio kuhusu uhai wa watu. Na kama hajui kitu ajifunze kunyamaza sio kuonesha hadharani alivyo blank kichwani.

Kwa matukio haya mawili Magoiga anapaswa kuziomba radhi familia ya Ben na familia ya Roma. Maisha ya binadamu hajawezi kulinganishwa na cheo cha Bashite wala cheo cha mtu yeyote duniani. Uhai wa mtu haujawahi kuwa na mbadala. Tuheshimu uhai wa kila mmoja wetu. Tutetee maisha ya kila mmoja wetu bila kujali tofauti zetu za kisiasa, kidini, kikabila etc.!

Malisa GJ
Kwanza ungeanza kuomba radhi wewe na Mange wako kwa raisi kwa kuadai raisi anataka kiki wakati alipoyashika makontena 3 yenye magari ambayo mlidai ni uongo
 
Kwanza watanzania tuanze kujiuliza haya yanatokea kwa sababu ya nini hasa?
Hawa watu walioibuka kipindi hii kwa kujifanya wao ndio walioiumba Tanzania kwa hiyo wanauchungu nayo sana kuliko watu wengine na kufikia mahali pa kuteka na hata kupoteza watu wengine ni lazima jamii iwakatae kwa nguvu zote.
Kama tunaweza kupambana na madawa ya kulevya kwa nguvu zote basi pia tupambane na hawa watu waovu kwa nguvu zote.
Wasituletee maisha ya ajabu ya kuua au kuteka watu na kuwatesa kwa ajili ya kutisha watu.
Hii nchi ni ya vyama vingi na kila chama kinapingana na kingine katika sera.
Kwa hiyo ni jukumu la wale walioshinda na kupewa dhamana ya kuongoza nchi kwa mishahara inayotokana na kodi za watanzania wote kulinda uhuru na uhai wa wale waliokosa, maana kazi yao ni kubweka mana wakekosa.
Waliopata walipewa ridhaa na watanzania hivyo wasijitenge .
Si busara kwa chama au kundi lolote kuteka watu wasio na silaha wala vurugu na hata kama kuna tofauti za kiushabiki ni bora watu wakajiepusha na umwagaji wa damu za watu.

Mtu mwenye nia njema na hii nchi ni lazima pia ajiepushe na kumwaga damu za watu wengine.

Tusipoangalia Kwa sasa adui ujinga ,umaskini,maradhi, uhalifu kama ujambazi utakua hauna vita vikali kama ilivyo vita dhidi ya wale wanaotofautiana kimitizamo ya namna bora ya kuleta maisha bora kwa kila mtanzania.

Kauli mbiu ya maisha bora kwa kila mtanzania iliasisiwa na CCM na kiongozi wake aliyepita. Siamini kuwa imeshafikia mwisho kwani maisha ni safari ndefu hivyo bado kila mtu anahitaji maisha bora na sio kutekana.
Tuchape kazi tusipoteze muda kwa kutekana na kufichana ndani.

Kuna watu wamesahau kabisa kuwa babu zetu walimwaga damu zao wakati wa kupigania uhuru sio kwa sababu serikali ya mkoloni haikuwa imewajengea barabara au mashule au maji au umeme au kuondoa ufisadi au haikuwa inakusanya kodi la hasha ; babu zetu walimwaga damu zao kupinga udhalilishaji, uonevu, utekaji , ubaguzi , dharau, kutwezwa utu wao , kudai uhuru wao kama binadamu, kudai uhuru wa kuisemea nchi yao na kutoa maoni yao kwenye nchi yao, kudai heshima yao kama binadamu, na kupinga vitendo vya kuwakamata na kuwanyonga wale waliowapinga wakoloni.
Babu zetu wangefufuka leo wangeshangaa kuona kuwa sisi tumegeuka kuwa wakoloni weusi kwa waafrika wenzetu.
Tunatenda yale yale waliyoyakataa babu zetu ambao waliamua kukataa utawala wa mkoloni pamoja na ukweli kuwa mkoloni angekuwepo mpaka leo huenda tungekuwa mbali zaidi kimaendeleo na katika nidhamu ya kazi. Lakini hata hivyo babu zetu hawakuaweka fikra zao kwenye maendeleo ya vitu bali walipigania UHURU na UTU wa mwafrika kama binadamu. Binadamu alizaliwa bila kitu chochote hivyo ule utu wake aliozaliwa nao ni wa kwanza kabisa ili awese kutafuta mambo mengne kama nguo fedha na mali.

Hawa watekaji wanajifanya nianze kuwaza kuwa kumbe hata hata mkoloni Mwarabu alipoamua kuuza watu kama samaki sokoni ni kwa sababu alikua anapewa support na waafrika wenzetu amabao walikua hajali UTU wa binadamu wenzao kwa sababu tu ya kupata ujira wao.
Siamini kuwa watekaji wanatumwa au wanatoka ndani ya serikali lakini najiuliza ni kwa nini watu wengine wanalichukulia kama jambo dogo kwa mtu kutekwa au hata kupotezwa kwa sababu tu eti anaonekana kuikosoa sana serikali. Kwani mtu akiikosoa serikali iliyowekwa na wananchi tena wanalipwa pesa nyingi kwa hayo madaraka kuna dhambi gani?

CCM na serikali yake ndio yenye dhamana ya maisha ,Uhuru na UTU wa watanzania mil.45 hivyo ni wajibu wao kuwalinda wote hata wale watukutu, vichaa, waropokaji na wahuni wa kila namna. Kama mtu amekosea au amevunja sheria basi akamatwe afikishwe mahakamani na sio kuleta ushabiki juu ya maisha ya watu au kutekana.
Hili halifai kabisa na sio vizuri likaachwa likajirudia tena.

Tumeona watu wakileta ushabiki wa kuona maisha ya wengine yanakatishwa na watu wasiojulikana kwa kusema kuwa amejitakia mwenyewe mana anaropoka ropoka. Kama kuropoka kwake ni kosa akamatwe hadharani na kufikishwa mahakamani. Afungwe ili kama baadae itakuja serikali atakayoamua kuiunga mkono basi ataiunga mkono.

Watanzania wote Tumuunge mkono Mh Rais kwenye kauli mbiu ya hapa kazi kwa kuiomba serikali kupitia waziri wa mambo ya ndani na Jeshi la Polisi watokomeze huu uhalifu mbaya kabisa dhidi ya binadamu. Mtu akitekwa anakosa muda wa kufanya kazi.

Hakuna sheria inayomuelekeza mtu yeyote kumteka mwingine kwa namna yoyote.

Ulinzi shirikishi uanzishwe kwenye kila mtaa kwa ajili ya kulinda maisha ya watu, pia kila mtu achukue tahadhari dhidi ya hawa watu waovu wanaoteka binadamu wenzao kwa faida zao wenyewe na waliowatuma.
 
Back
Top Bottom