Mbao za Mawe
JF-Expert Member
- May 11, 2015
- 23,372
- 55,049
Majuzi kuna wasanii wawili wa sanaa ya muziki wa singeli waliamka na akili za utotoni na kuzua taharuki mitandao. Huwa sina utaratibu wa kusifia kilicho kibovu na ikitokea nimesifia msanii kuwa kafanya vizuri basi ni kweli kwangu anakuwa kafanya kazi nzuri sana.
Tunajua muziki wa singeli unatazamwa kwa taswira mbalimbali wengi wakitazama muziki huu kama muziki wenye kuhusiana na uhuni hasa kwenye tungo na mashairi ya nyimbo hizi. Inawezekana kweli baadhi ya vibao vya wasanii wa nyimbo hizi vina tungo tata na zisizoeleweka kwa wengi.
Leo nimediriki kuangalia wimbo wa singeli wa msanii Dragon Boy unaitwa FOTO ama hakika kijana huyu alijua anachokifanya katika wimbo huu kuanzia uimbaji hadi video yenyewe.
Kijana kwenye wimbo huu anaelezea yuko Dar ila washikaji zake wanaona kama jogoo hawiki, hivyo Dragon anaamua kumpigia simu mpenzi wake aliyepo Morogoro akitaka amtumie picha ambazo zitawanyamazisha washikaji zake maana kampa sifa kedekede.
Hongera sana Dragon Boy kazi hii nitaipenda hata kama utakuja kuvurunda huko mbeleni ila umeacha alama ambayo haitafutika katika anga la burudani.