Kwa mara ya kwanza natoa pongezi kwa aliyekuwa msemaji wa CCM ambaye kwa sasa ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo Nape Nnauye.
Katika taarifa ya habari ya ITV ya saa mbili usiku huu, alipokuwa akijibu hoja ya kukataliwa kwa waandishi wa habari wa redio na televisheni kuingia katika ukumbi wa bunge kurekodi sauti na picha za video, ametoa ahadi kuwa atakaa na wadau ili bunge lirushwe live na wadau wa habari.
Hakika ahadi hii imenikuna sana na namsihi Mhe Nape afanye hima ili ufumbuzi wake upatikane mapema sana.
==================
Dodoma. Uamuzi wa Bunge kuzuia vyombo vya habari vya kielektroniki kuingia ndani ya ukumbi wa chombo hicho cha kutunga sheria na kamera au vifaa vya kurekodi shughuli zinazoendelea, umezua taharuki kwa wanahabari wanaoripoti Bunge la Bajeti lililoanza jana mjini Dodoma.
Wanahabari hao kutoka redio na televisheni mbalimbali nchini walilazimika kufuatilia shughuli za Bunge kupitia televisheni zilizopo katika jengo la Idara ya Habari ya Bunge, huku kila mmoja akilaani uamuzi huo.
Juzi Bunge lilieleza utaratibu huo mpya kwamba jukumu la kurusha matangazo ya vikao litafanywa na Bunge lenyewe kupitia studio maalumu, ili kurahisisha kila kituo cha redio na televisheni kupata matangazo hayo kwa sehemu walipo bila kufunga mitambo yao bungeni.
Kupitia studio hiyo vyombo hivyo vya habari vitachukua matukio mbalimbali jambo ambalo limelalamikiwa na baadhi ya wanahabari na wabunge kwa maelezo kuwa kuna baadhi ya masuala nyeti yatafutwa na studio hiyo.
Jana wanahabari waliopewa vitambulisho maalumu vya Bunge walipigwa ‘mkwara’ na maofisa wa idara ya habari wakitakiwa kuhakikisha hawarekodi jambo lolote linaloendelea ndani ya ukumbi huo, huku wale wa redio wakipewa picha za video badala ya sauti, jambo ambalo liliwapa wakati mgumu kutengeneza habari zao.
Hii ikiwa ni kutekeleza agizo lililotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano cha Bunge, Owen Mwandumbya alilolitoa juzi.
Akizungumzia suala hilo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye alisema kila utaratibu mpya una changamoto zake na kusisitiza kuwa wizara hiyo itakaa na uongozi wa Bunge na wadau wa habari ili kujadili suala hilo.
“Lengo ni kujadili ili kuona ugumu uko wapi ili kushauriana na Bunge kuona wapi linaweza kubadili. Kama kuna tatizo tutajua jinsi ya kulitatua. Mwisho wa siku tunataka kila mdau atimize wajibu wake bila ugumu,” alisema Nape.
Alipoulizwa sababu za mjadala huo kufanyika kabla ya Bunge kuja na utaratibu huo mpya alisema uamuzi wa Bunge kuwa na studio zake ulianza siku nyingi lakini wadau wa habari hawakuwahi kulijadili jambo hilo na kutoa mapendekezo yao.
“Jambo hili halikuanza Serikali ya Awamu ya Tano. Limeanza siku nyingi na linafanyika katika mabunge mengi ya nchi wanachama wa jumuiya ya madola,” alisema Nape.
Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa alisema, “Jambo hili halileti sura nzuri katika ukuaji wa demokrasia na ile hali ya kila mhimili kufanya kazi kwa kujitegemea. Bunge kuminya habari ni kutaka kuubana mhimili mwingine.”
“Habari zitakazotolewa na studio ya Bunge haziwezi kuwa na uhalisia na wananchi hawawezi kupata kila wanachokitarajia.”
Alisema Serikali ya Awamu ya Tano inajipambanua kwa kaulimbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’, haitakiwi izuie mambo ya msingi.
“Kuna ubaya gani wabunge wakionekana kuongea na kueleza mambo yao na wananchi wakaona na kuwapima wabunge wao. Serikali ya Awamu ya Nne ilipeleka demokrasia mbele ila awamu hii nina wasiwasi nayo maana inaturudisha nyuma,” alisema.
Mbunge wa Kilolo (CCM), Venance Mwamoto alisema, “Nadhani pande zote kwa maana ya wadau wa habari, Serikali na Bunge zinapaswa kukaa chini kulijadili suala hili kwa manufaa ya wote.”
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwa sharti la kutotajwa majina, waandishi wa habari wa Televisheni za ITV na Clouds Televisheni walisema uamuzi huo wa Bunge unawanyima uhuru wao wa kufanya kazi.
“Wametunyima uhuru wa kufanya kazi kwa sababu tutashindwa kuripoti habari tunayoitaka ifikie jamii. Wabunge jana wameongea lakini tumeshindwa kupata maudhui ya walichokisema. Studio ya Bunge imetuletea kile chenye manufaa kwao si kile chenye manufaa kwa wananchi,” alisema mmoja wa wanahabari wa Clouds Televisheni.
“Mfano mimi ni mwandishi wa redio lakini badala ya kupewa sauti napewa video ya kilichoendelea bungeni sasa hicho kitanisaidia nini. Mimi nahitaji sauti tu na huu utaratibu wao utatupa kazi kubwa na unatuminya,” alisema mmoja wa wanahabari wa redio ambaye hakutaka jina lake litajwe.
Akizungumzia suala hilo Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania(MCT), Kajubi Mukajanga alisema haoni kama kuna jipya lolote kwa kuwa msimamo huo ulishatangazwa kabla ya kuanza kwa vikao vya Bunge. “Acha niangalie kama nitaona kuna jambo jipya tutatoa msimamo wa baraza.”
Theophil Makunga ambaye ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri(TEF) naye alisema haoni jipya kwa kuwa suala hilo wameshalizungumzia sana.
Chanzo: Mwananchi