Kwa mara nyingine tena napelekwa polisi

Kwa mara nyingine tena napelekwa polisi

Jurrasic Park

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2013
Posts
3,833
Reaction score
6,889
Mara ya kwanza nilienda baada ya yule mwandani wangu kumpiga
Hii ya jana ilikuwa kali. hapa kwangu ninapokaa tupo majirani na wana watoto ila mimi nakaa kibachela. huwa nina tabia ya kutokupika mpaka awepo miss.

Jana kama kawaida yangu nimerudi home nipo na take away za mirinda. mtoto kaingia ndani(hana mazoea ya kuingiaga mama au baba yake wakiwa) kuona mirinda mtoto kilio. nikachukua glasi nikammiminia. akaanza kunywa na michezo michezo akaivunja. mimi nikamchapa yule mtoto.

Mama yake kuskia mtoto analia na midomo mekundu kanijia juu na mimi sitaki ujinga na wanawake nikamtukana sana yule mwanamke. jioni mme wake kaja, ilikuwa ligi ndefu kidogo tupigane nashukuru majirani.

Leo napelekwa polisi kwa kosa la kumzalilisha huyo mwanamke. sasa sijui namalizaje huu msala. nimetaka kuhonga lakini wamenikazania wale wazazi lazima lifike mahakamani.

Ushauri jamani natokaje hapa sitaki kwenda mahakamani tena
 
Unachekesha kweli, kwahiyo unaandika huu uzi huku umejitwisha mtondoo au? Au nyapala amekua mtu wako wa karibu amekupa simu uombe ushauri?
 
we ni mshamba!unapigaje mtoto kisa glasi!mambo ya kizamani hayo,mbona baa tunavunja glass na hatulipishwi,kwanza mtoto uwekewa soda kwenye chombo cha plastik sio glas
 
Uende tuu hamna namna nyingine,hatutaki RAIA wasumbufu uraiani.
 
Sasa mtoto anavunja glass unamchapa jaman bora angekua wako mtoto wa mtu unamuacha tu
 
We jamaa ni mkorofi kama Faru John
 
Kwanza ni aibu mwanaume kurushiana maneno na wanawake. Sio tabia ya kiume kabisaa. Jifunze kuwa conflict solver, waulize wenzio wanawezaje kuishi bila magomvi ya namna hiyo na utaishi kwa amani.

Ushauri:
Mtafute jamaa (mume wa huyo Dada chemba, zungumza nae kiume umweleze picha lilivyokuwa mpaka ukajikuta umeshindwa kujizuia kugombana na mkewe, na umwombe akamshawishi mkewe yaishe kiujirani mwema maana ipo siku mnawezapata shida mkasaidiana kama majirani.
 
Kumchapa mtoto ujanikera, ila umenikera mtoto wa kiume kuanza kutukanana na mwanamke. Hivi hukuona aibu? Pelekwa mahakamani wakakufunze ustaarabu maana unaonekana mkorofi
 
Una nyota ya jela??????

Kulikuwa na haja gani ya kumpiga huyo mtoto???
 
na kwa nini unamzaoea na watoto wa watu? ongea na wazazi jishushe
 
Hivi mwanaume unaanzaje kurushiana maneno na mwanamke. Kisa glass tu na inatakiwa ujue ipo siku ingevunjika tuu sidhani kama ingekaa siku zote.

Wavulana mna mambo nyie.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom