Kwa mara nyingine Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na Kanda ya Kusini zimetengwa kwenye ufadhili wa masomo ya ubobezi wa kitabibu

The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
19,586
14,138
Bila kuchoshana,

Juzi hapo Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alitangaza ufadhili wa fani za kibingwa kwa watalamu wa Hospitali za Rufaa za Kanda na Taifa. Katika ufadhili huo unaoitwa Samia Health Specialisation, hospitali zote za kanda zimepata ufadhili wa kuwa bobezi kwenye baadhi ya fani.

Cha kusikitisha na kushangaza Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ya Mbeya haipo kwenye huo mpango. Kana kwamba haitoshi, Hospitali ya Kanda ya Kusini Mtwara nayo haijawekewa specialisation yeyote.

Swali, hivi kwa nini Serikali ya CCM imekuwa na tabia ya kuitenga mikoa ya Kusini mwa nchi kiujumla, hususani Mbeya?

Toka zama za Mkapa kumekuwa na hii tabia, kuna Miradi mingi tuu ilikwepeshwa na kupelekwa maeneo mengineyo. Kwa mfano airport pekee ya Kanda ya Songwe haujakamikika toka alivyoanzaga kujenga Mkapa.

Pia inashangaza kwamba hata viongozi wengi wanaotokea Kusini huwa hawafanyi cha maana, angalia Hayati Mkapa, PM, Pinda na sasa PM Majaliwa, kwani nyie viongozi hamuoni wenzenu wanachofanya?

Kwamba Kusini kwa ujumla hakuna watu na hakitakiwi kuwa na huduma bora kama kanda zingine? Hii mambo inakera sana.👇
 

Attachments

  • 20221029_220712.jpg
    20221029_220712.jpg
    169.5 KB · Views: 10
  • 20221029_220645.jpg
    20221029_220645.jpg
    139.5 KB · Views: 9
  • 20221029_220552.jpg
    20221029_220552.jpg
    139.1 KB · Views: 9
  • 20221029_220724.jpg
    20221029_220724.jpg
    142.8 KB · Views: 9
  • 20221029_220613.jpg
    20221029_220613.jpg
    157.7 KB · Views: 8
  • 20221029_220539.jpg
    20221029_220539.jpg
    151.8 KB · Views: 7
  • 20221029_220658.jpg
    20221029_220658.jpg
    140 KB · Views: 12
Mkuu hayo mambo kawaida sana ..Bora hamjawai kupew majina mabaya kama sie kanda zetu ,tumepewa majina mabaya kisa tulikataa wakoloni mpake leo ,ila tuna kila kitu talents kila kona ..


Sio kama mbeya ni sehemu ya kuisahau maana kuna wasomi kibao, wakulima hata idadi ya watu ni kubwa.

Yote yote mambo mengine ukiona yanakuumiza kichwa achana nayo maana wakubwa washaaamua ivyo.
 
Bila kuchoshana..

Juzi hapo Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alitangaza Ufadhili wa fani za kibingwa kwa Watalamu wa Hospital za Rufaa za Kanda na Taifa..

Katika Ufadhili huo unaoitwa Samia Health Specialisation, Hospital zote za Kanda zimepata Ufadhili wa kuwa bobezi kwenye baadhi ya fani..

Cha kusikitisha na kushangaza Hospital ya Rufaa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ya Mbeya haipo kwenye hiyo skimu..

Kana kwamba haitoshi, Hospital ya Kanda ya Kusini Mtwara nayo haijawekewa specialisation yeyote..

Swali,Hivi kwa nini Serikali ya CCM imekuwa na tabia ya kuitenga Mikoa ya Kusini mwa Nchi kiujumla? Hususani Mbeya?

Toka zama za Mkapa kumekuwa na hii tabia,kuna Miradi mingi tuu ilikwepeshwa na kupelekwa maeneo mengineyo..Just kwa mfano airport pekee ya kanda ya Songwe Haujakamikika toka alivyoanzaga kujenga Mkapa..

Pia inashangaza kwamba hata Viongozi wengi wanaotokea Kusini huwa hawafanyi Cha maana,angalia Marehemu Mkapa,PM Pinda na Sasa PM Majaliwa,Kwani nyie viongozi hamuoni wenzenu wanachofanya?

Kwamba Kusini Kwa ujumla.hakuna watu na hakitakiwi kuwa na huduma Bora kama Kanda zingine? Hii mambo inakera Sana.👇
Ewe mtanganyika usitarajie maendeleo ya eneo lako na jamii yako chini ya huyu mzanzibari
 
Back
Top Bottom