1000 digits
JF-Expert Member
- Oct 16, 2012
- 6,260
- 7,936
Ingekua hakuna haja ya mapokezi CCM iliyofanya siasa peke yake kwa miaka mitano wasingepita hata kupiga kampeni kwa fedha nyingi na kuwanunua waandishi wa habari na vyombo vyote vya habari na kuwatisha wasanii wote nchini ili wazunguke nao kujaza watu kwenye mikutano.Kuna tofauti kati ya mapokezi na wapiga kura. Usisahau hilo tafadhali.
Nguvu ya vijana kuunga mkono upinzani isipuuzwa ni taarifa mbaya sana kwa wapenda madaraka wanaotegemea wazee walioanzisha CCM ya madaraka.
Tatizo la wapinzani ni kukosa Timu nzuri ya kampeni na pia Wasimamizi wa uchaguzi kuvuruga uchaguzi mapema bila kuchukuliwa hatua yoyote inawakatisha tamaa wapiga kura . Hata kuchukuliwa sheria mkononi ingewatia moyo wapinga dhulma duniani na mbinguni pia. Kuacha dhulma ishamiri ni kuiunga mkono.