Kwa maneno haya ya Pele, soka litakuwaje baadaye?

Tena ukiongeza na VAR ndio kabisa Hatuwez kuona ubora wachezaji .. Yaani wanataka wachezaji wachezaji wacheze Kama Maroboti wasizidi hata ukucha .. This is so disgusting.
Mimi ndo maana kuna wakati sitazami kabisa mpira hata ziwe big names
 
Pele yupo sahihi, kwa sasa wala hata sikatishi usingizi kusubiri mechi, huwa nasubiri tu matokeo kwenye vyombo vya habari. Ukisikia mechi ya UEFA labda Real Madrid na Bayern, hata haushituki unaweza lala kabisa kwa amani. au Simba na Yanga, kawaida mno.

Mpira wa sasa hauvutii kabisa, ni upotevu wa muda na kuunguza calories kukesha kuangalia maigizo
Huku tupo pamoja. Mpira wa sasa haushtui. Michezaji haina kabisa talanta.
 
Wakati akizungunza na Gazzeta dello Sport na nchini Italia, Pele aliongea mambo kadhaa, (Kimsingi alikua anamzungumzia ubora wa Messi)

Jambo lilinivutia ni hili naunukuu "but feels there are not as many truly world-class talents around now as there have been in notable eras of the past'', akimaanisha kwa sasa hakuna wanasoka wenye vipaji kama wakati uliopita.

“Once you found two or three in every country with a great football culture'', kwamba kipindi ambacho ungeweza kupata wachezaji wakali angalau wawili au watatu katika kila nchi. Akiendelea na kuwataja baadhi, akisema "There were so many. Today we have two or three in total". Messi, Ronaldo na labda Neymar (nadhani alimtaja kwa sababu ya Ubrazil).

Nadhani wote tutakubaliana kuwa kwa sasa vipaji halisi vya soka vinapungua sana,

Future ya mpira wa miguu itakuwaje, football without talent?
Sio mpira tu fananisha kina MOHAMMAD ALLY, MIKE TYSON, SUGAR RAY, BRUNO na hawa wa sasa kina Maywether, Khan,Kilitshko

Pia fananisha kina Michael Jordan, Scott Pipen, Thompson Snr, Shacq na hawa kina Harden, Criss Paul, Green n.k

Dunia imeshafikia kipindi ambacho individual skills ni secondary aspect, watu wanafuata mifumo/styles itakayowawezesha kushinda
 
Sio mpira tu fananisha kina MOHAMMAD ALLY, MIKE TYSON, SUGAR RAY, BRUNO na hawa wa sasa kina Maywether, Khan,Kilitshko

Pia fananisha kina Michael Jordan, Scott Pipen, Thompson Snr, Shacq na hawa kina Harden, Criss Paul, Green n.k

Dunia imeshafikia kipindi ambacho individual skills ni secondary aspect, watu wanafuata mifumo/styles itakayowawezesha kushinda
Kama mdau wa juu alivyosema Hela na biashara kwenye michezo zinaharibu kwa kiwango kikubwa sana vipaji.

Mfano mzuri angalia uwiano wa mishahara baina ya wachezaji wanaoshambulia na wachezaji wanaozuia, hii inasababisha kila mtoto anaezaliwa kupendelea kushambulia zaidi kuliko kukaba ndio maana tunafikia age kama hii ambayo mtu Kama Ramos amba Van djik kuonekana bora zaidi duniani, wachezaji ambao ukiambiwa utaje mabeki 50 bora toka mpira uanze wanaweza hata wasiwemo.

Kushuka kwa quality ya wachezaji wanaokaba kunasababisha pia ku overate wachezaji wanaoshambulia ndio maana hii age yetu mchezaji kufunga Goli 50 kwa msimu ni kitu cha kawaida sana kina Harry kane, Ibrahimovic, Messi, Ronaldo, etc hivyo kufunga ama kushambulia kumekuwa rahisi kutokana na level ya uzuiaji kushuka inasababisha pia kupunguza vipaji maana akili ya ziada haihitajiki sana kucheza na timu yenye beki mbovu.
 
Back
Top Bottom