Kwa wale mnaopata KBC na citizen muwe mnafuatila bunge la kenya mjifunze. Ukiwaangalia wabunge Kenya ni makini sana na wana hoja nzito na wanakuwa wamesoma na kuwa na uelewa wa mambo kabla ya kuzungumza. Asilimia kubwa ya wabunge wana kiwango cha Dr Slaa, Mbowe, Zitto Kabwe, Mnyika, Tundu Lissu, lema nk. Ukifuatilia bunge lao ukilinganisha na upupu wa watu wa cuf na ccm unakuwa sawa na unapima kiwango cha shule ya msingi na chuo kikuu. Wabunge wa ccm na cuf wajifunze maana kizazi hiki cha wasomi kinazidi kukua hawatachaguliwa tena kwa ajili ya blabla.
Ukiangalia speaker wao alivyo na uwezo utafurahi.
Sure yaani Speaker wa bunge la Kenya ndio angepaswa kuitwa speaker wa standard and speed. Halafu nimejifunza kitu kimoja kutoka bunge la Kenya speaker wao hakubali kumaliza swali kinyemela mpaka liwe exhasted vya kutosha na wabunge warizike, Ikitokea Waziri ameshindwa kuja na jibu la kuridhisha kwao huwani kawaida kwa speaker kuahirisha swali na kumuagiza waziri husika akatafute majibu ya kuridhisha.
Kitu kingine kwa bunge la Kenya ni kwamba mbunge anaposimama kwa point of order speaker huwa haachi kumsikiliza and then anafanya maamuzi kama point of order iliotolwa ni valid au sivyo sasa sisi Anna Makinda anakwambia hana muda hata wa kusikiliza miongozo ya wabunge eti kwa sababu tu wanatoka upinzani. Kwa hakika Makinda angelipewa kuongoza bunge la Kenya nafikiri angefukuzwa kazi na wabunge kabla hata ya mwezi mmoja kumalizika.