Kwa Makanisa yetu Tanzania

Kwa Makanisa yetu Tanzania

Desire Dizaya

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2015
Posts
6,476
Reaction score
11,671
hivi kama mtu hana sadaka ndo asije kabisa kanisani..semeni tu kuliko kudhalilisha wanyonge huko ibadani.
naona tukiingia ibadani mmekazia michango hadi tusio nacho tunaona aibu..
ukiingia na mia tano yako unakuta sadaka za aina tano sijui..mwenye mia yake afanyeje?
kanisa nnalosali walah tena mchungaji alikua anakera ila hajui tu..anashika mic anatangaza mchango halafu anamfuata mmoja mmoja alipokaa na kumwekea mic aseme aahidi..au kama ana hela atoe yoyote..halafu anaitangaza na jina la mtu
kibaya zaidi ni hii tabia ya kutangaza sadaka ya mtu
maandiko yanasema sadaka ni siri ya mru na MUNGU wake..yani vile anapoishika mkononi ..mkono mwingine usijue..sembuse bindamu mwenzie.???

na sasa mna maombi kwa kiwango cha sadaka..eri wafanyabiashara sadaka maalum elfu sitini..uiweke kwenye bahasha maalum ukienda kutoa ndo eti unaombewa baraka na mafanikio...si kila mfanyabiashra anamudu..kwahiyo wao wasiomudu.hawastahili baraka na kufanikiwa kutoka kwa Mungu?

mimi mara ya mwisho kwenda kanisa la kilokole ni pale mtongani..toa sadaka uwekewe mkono...wasio na sadaka za kuweka kwenye bahasha wanaona bora wabaki tu..wanaovoangaliwa sasa ni aibu!!

nkarudi nkawa nasali kwenye dhehebu langu...siku ya pentcoste akaja muhubiri wa siku zote kanisani..baada ya sala na maombi mazito nashangaa watu wanatoa bahasha za khaki wanaingiza hela..noti!!..
mi nlikuja na buku yangu..sadaka nshatoa..naambiwa hii sadaka ya mafuta ya baraka sijui upako..yale ya mzeituni
tatizo sikuwepo jumapili ilopita..na wasiokuwepo pia jpili lopita wakapewa bahasha..tia hela humo...wakaanza kupanga foleni ya kupakwa mafuta..lakini kwa utaratibu kwamba wewe usiyeenda unaonekana ukiwa umekaa umebaki benchi walipotoka...mi nlijiskia vibaya sana..kilichoniuma zaidi kuna mabint wawili karibu yangu..nkawauliza mbona hamuendi..wakasema tunajua lakini hatuna hela
mavazi yao yalionesha kabisa wapo duni.
nlitarajia wahudumu wa kanisa wanaosimamia wawaambie nendeni hivohivo hata kama hamna hela..walaa!wanawapita tu!
mi wananiuliza huna sadaka!?.nkawaambia sina nlikuja na sadaka kuu tu..nshatoa.wanajibu haya!
kule mbele sasa..tumbukiza bahasha..pakwa mafuta kwenye paji! tumbukiza bahasha ya sadaka nkupake mafuta utsinii..

najua mnatoa bahasha coz taget zenu ni noti noti tu..maskini na mia yake aiweke kwenye bahasha?

jiskieni aibu!
 
Vitendo hivi vinawaudhi wengi lakini hawana namna. Mtu akiwaza mazishi yake yatakuwaje akijitenga na makanisa anaogopa, hivyo kuendelea kujikaza.

Kuna haja ya kuwa na umoja wa kusaidiana kiroho na faraja kipindi cha matatizo. Umoja ambao imani yake ni Mungu lakini hauwaibii watu. Maana kinachotutisha wengi ni pale mtu asiyehudhiria kanisani anapopata matatizo ama kufiwa au kufa mwenyewe. Katika kipindi kile ndipo mahubiri ya vitisho hutolewa na kuwaogofaya watu. Hofu huwafanya wavumilie kuibiwa ili mradi wanafurahia Security ya kundini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Salute, Comrade.

Historia inaonyesha kuwa "Primitive thinking ndiyo source ya uwepo wa vitu pasina kuhoji, kusaili, kudodosa na kadhalika", They just need command from the above. No reasoning, No truth. Nje ya hapo utakuwa huna tofauti na Dubu wa kwenye maonesho kule Ulaya.

Biblia inasema ....bisheni nayi mtafunguliwa. Ni kweli tu wabishi wa kuongozwa katika Roho na kweli?. If not why?.

Tusiwe Primitive thinkers waso hoji lolote hata kama halina mantiki. Tuhoji kila kitu kwa hekima na busara. Kuendeshwa kwa Ibada katika muktadha huo si sahihi kabisa na hata Biblia Takatifu haikuagiza hivyo.

Yakobo 1;27- Dini iliyo safi, isiyo na uchafu mbele za Mungu Baba, ndio hii: kuwasaidia yatima na wajane katika dhiki zao, na kujilinda mwenyewe usichafuliwe na ulimwengu.

Nb: Your Ignorance is their Power. Hoji hadi kanisani na atakayekutishia kuwa UTACHOMWA MOTO mwambie kuwa "Wewe ndiyo kwanza tayari unaungua".

Hekima Ni Uhuru.
 
Hv mkuu unataka useme hujanielewa au unajitoa akili?

Cathoric Churc ok
Heshima boss!

Tafsiri sahihi ya maneno, hati nadhifu, mpangilio bora wa kisarufi ni dira sahihi ya kutuongoza katika majadiliano yoyote yale. Iwe katika mazungumzo ya ana kwa ana au kimaandishi. Kubali kukosolewa na huku ndiko kujifunza kwa dhana ya kimantiki.

Siyo kwamba hukueleweka, la hasha!. Pia sidhani kama aliyeulliza alichokiuliza aliamua kujitoa akili/ufahamu.

Lazima tukosoane ili tufike tunakohitaji kwenda.

Kumradhi.
 
Ahsante mkuu nimekuelewa..
Heshima boss!

Tafsiri sahihi ya maneno, hati nadhifu, mpangilio bora wa kisarufi ni dira sahihi ya kutuongoza katika majadiliano yoyote yale. Iwe katika mazungumzo ya ana kwa ana au kimaandishi. Kubali kukosolewa na huku ndiko kujifunza kwa dhana ya kimantiki.

Siyo kwamba hukueleweka, la hasha!. Pia sidhani kama aliyeulliza alichokiuliza aliamua kujitoa akili/ufahamu.

Lazima tukosoane ili tufike tunakohitaji kwenda.

Kumradhi.
 
Vitendo hivi vinawaudhi wengi lakini hawana namna. Mtu akiwaza mazishi yake yatakuwaje akijitenga na makanisa anaogopa, hivyo kuendelea kujikaza.

Kuna haja ya kuwa na umoja wa kusaidiana kiroho na faraja kipindi cha matatizo. Umoja ambao imani yake ni Mungu lakini hauwaibii watu. Maana kinachotutisha wengi ni pale mtu asiyehudhiria kanisani anapopata matatizo ama kufiwa au kufa mwenyewe. Katika kipindi kile ndipo mahubiri ya vitisho hutolewa na kuwaogofaya watu. Hofu huwafanya wavumilie kuibiwa ili mradi wanafurahia Security ya kundini.

Sent using Jamii Forums mobile app

Dou sasa mkuu tutatokaje huku au tukubali tu kuwa 'Victims' kwa sababu ya hofu ya kufiwa ama kufa muhusika , kiukweli inabidi kama binaadam tunao jitambua pamoja na mazuri mengi katika imani zetu lakini ikifikia tunakuwa 'powerless' tuna mkosea hata muumba wetu

Binaadam anapoanza kujitambua na kutambua nafasi yake hapa duniani hizi hofu zinazoletwa na imani zetu au mitizamo ya kijamii zinapungua sana
 
Hivi ni lini mtaacha kwenda makanisa ya ajabu ajabu?? Tatizo lenu hata neno la Mungu hamsomi ndio maana mnatangatanga kama kondoo waliopotea. Wewe unaingia kanisani unaona kabisa wanafanya mambo ambayo yako kinyume na Biblia (kama kupakwa mafuta kwa hela ilihali Yesu alisema "Mmepewa bure, nanyi toeni bure") alafu unarudi tena?
Jifunze kusoma neno la Mungu na kumwomba Mungu ili akuongoze upate mahali panapofaa kuabudia, hakika huta tangatanga tena kwenda kwenye makanisa ya ajabu ajabu kama hilo.
 
Ndugu tupo pamoja nini? maana nipo Angilikana hapa moro mjini. nimwendo wa sadaka!!
Tena si moja. Zinakuwa tatu au nne. Ipo ya kawaida, sadaka ya pili ya ujenzi, ya tatu ni ya shukrani, ya nne ya kuwategemeza wapakwa mafuta, n.k,. Bado lipo fungu la kumi na michango mingine kadhaa.
 
Back
Top Bottom