Kwa lipi Lowassa apewe nchi?

Kwa lipi Lowassa apewe nchi?

Nikukumbushe

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2013
Posts
2,602
Reaction score
408
Kwa lipi la maana alilolifanya Lowassa hadi apewe nchi?

Kuna sababu nyingi za kusema Lowassa hafai kuwa rais wa nchi hii licha ya kuwa mgonjwa wa macho na mgongo pia ni mmoja wa watu 11 waliotajwa kuwa ni mafisadi.

Amefanya nini la maana hadi tumpe nchi? Unamkumbuka kwa lipi zaidi ya kujiuzulu?

Pesa zake sio tiketi kuwepo ulazima wa kuingia ikulu. Kama anatafuta umaarufu,umaarufu sio kwa mazuri tu hata ufisadi na kujiuzulu napo aljulikana ndani na nje ya nchi.

Anaitwa mtu wa maamuzi magumu,maamuzi yapi? Kujiuzulu ni uwajibikaji sio maamuzi magumu. Maamuzi magumu yapi? Alikuwa anafukuza watumishi wa serikali majukwaani bila hata kuwapa nafasi ya kijitetea(natural justice).

Kama sio kuwaonea ni nini? Yeye alikuwa analalamika ooh mh spika,nimeonewa sana,nimesikitika sana hata sijaulizwa juu ya Richmond sijapewa hata nafasi ya kujitetea(natural justice),amesahau kuwa usihukumu usije ukahukumiwa(mathayo 7:1)

wanasema alijenga shule za kata,je,alitumia pesa yake badala ya kodi za watz? Walitaka afanye nn wakati ulikuwa wajibu wake kama mtendaji mkuu wa shughuli za serikali za kila kitu?

Sababu zipi za kunishawishi kumpigia kura Lowassa awe Rais wa awamu ya tano?
 
afadhali apewe, maana kwa miaka 9 sasa nchi ipo auto pilot! hakuna wa kuamua jambo! kila mtu analalamika! bora aje atuibie lakini awe na maamuzi endelevu!

Ndugu Masese Nakuunga Mkono sana, Edward ni kiongozi mwenye uamuzi , mtendaji na pia Fisadi (Japo ni mtenda kazi makini lakini hilo lipo) Juu ya ufisadi wake yeye anazitumia hizo pesa nchini na zinasaidi uchumi wetu, kuliko wale walioiba na kuziweka Uswisi. Ninachoogopa Jee tukimpa madaraka, ataendelea na mtindo wa kujilimbikizia mali kufidia alizotumia kuutafuta utawala kwa nguvu ya pesa zetu????
 
Kwa lipi la maana alilolifanya lowasa hadi apewe nchi? Kuna sababu nyingi za kusema Lowasa hafai kuwa rais wa nchi hii,licha ya kuwa mgonjwa wa macho na mgongo pia ni mmoja wa watu 11 waliotajwa kuwa ni mafisadi.
Amefanya nini la maana hadi tumpe nchi? Unamkumbuka kwa lipi zaidi ya kujiuzulu? Pesa zake sio tiketi kuwepo ulazima wa kuingia ikulu. Kama anatafuta umaarufu,umaarufu sio kwa mazuri tu hata ufisadi na kujiuzulu napo aljulikana ndani na nje ya nchi.
Sababu zipi za kunishawishi kumpigia kura Lowasa awe rais wa awamu ya tano?
swali hili alijibu Mwenyekiti wa kamati yake ya Ushindi, Apson Mwang'onda, yeye aliwahi kufanya naye kazi, lipi la kujivunia toka kwa LOWASSA?
 
Ndugu Masese Nakuunga Mkono sana, Edward ni kiongozi mwenye uamuzi , mtendaji na pia Fisadi (Japo ni mtenda kazi makini lakini hilo lipo) Juu ya ufisadi wake yeye anazitumia hizo pesa nchini na zinasaidi uchumi wetu, kuliko wale walioiba na kuziweka Uswisi. Ninachoogopa Jee tukimpa madaraka, ataendelea na mtindo wa kujilimbikizia mali kufidia alizotumia kuutafuta utawala kwa nguvu ya pesa zetu????

Nini zaidi alichoamua kama siyo umeme wa RICHARD MONDULI?
 
Ndugu Masese Nakuunga Mkono sana, Edward ni kiongozi mwenye uamuzi , mtendaji na pia Fisadi (Japo ni mtenda kazi makini lakini hilo lipo) Juu ya ufisadi wake yeye anazitumia hizo pesa nchini na zinasaidi uchumi wetu, kuliko wale walioiba na kuziweka Uswisi. Ninachoogopa Jee tukimpa madaraka, ataendelea na mtindo wa kujilimbikizia mali kufidia alizotumia kuutafuta utawala kwa nguvu ya pesa zetu????

maamuzi yapi? Hata JK ana maamuzi magumu kwa ukimya wake
 
Ccm haina rasimali watu imezungukwa na mafisadi hawana dhamira safi ya kuitoa nchi katika mkwamo huu tunahitaji fikra mpya huru mbali na hawa wanamtandao wa ufisadi
 
LOWASSA ni mtu mwenye maamuzi na anayethubutu,si wa kulialia kama wanavyolia na kulalamika viongozi wa sasa,haijulikani mwananchi ni nani na mwenye maamuzi ni nani

kwa maamuzi ya kujiuzulu sawa,pia kwa maamuzi ya kuingia mkataba na kampuni hewa nayo pia ni maamuzi magumu.
 
Kwa sababu ana ela nyingi za ufisadi, afya tata (by membe) na huwa anazigawa kanisan na mckitin
 
Kwa lipi la maana alilolifanya lowasa hadi apewe nchi? Kuna sababu nyingi za kusema Lowasa hafai kuwa rais wa nchi hii,licha ya kuwa mgonjwa wa macho na mgongo pia ni mmoja wa watu 11 waliotajwa kuwa ni mafisadi.
Amefanya nini la maana hadi tumpe nchi? Unamkumbuka kwa lipi zaidi ya kujiuzulu? Pesa zake sio tiketi kuwepo ulazima wa kuingia ikulu. Kama anatafuta umaarufu,umaarufu sio kwa mazuri tu hata ufisadi na kujiuzulu napo aljulikana ndani na nje ya nchi.
Sababu zipi za kunishawishi kumpigia kura Lowasa awe rais wa awamu ya tano?

hivi wewe upo dunia ya ngapi.Katika kipindi cha miaka 2 aliyokaa madarakani bwana EL kajenga shule za kata kibao,chuo cha dodoma na mradi wa maji wa ziwa victoria kupeleka mikoa ambayo haikua na maji ya shinyanga,simiyu na Geita.Sasa unvosema hajafanya kitu mie nakushangaa sana na kuhusu ufisadi ile hela walipiga watu wengi sana ila yeye ndiye aliyekua mbuzi wa kafara.
 
Kwa lipi la maana alilolifanya lowasa hadi apewe nchi? Kuna sababu nyingi za kusema Lowasa hafai kuwa rais wa nchi hii,licha ya kuwa mgonjwa wa macho na mgongo pia ni mmoja wa watu 11 waliotajwa kuwa ni mafisadi.
Amefanya nini la maana hadi tumpe nchi? Unamkumbuka kwa lipi zaidi ya kujiuzulu? Pesa zake sio tiketi kuwepo ulazima wa kuingia ikulu. Kama anatafuta umaarufu,umaarufu sio kwa mazuri tu hata ufisadi na kujiuzulu napo aljulikana ndani na nje ya nchi.
Sababu zipi za kunishawishi kumpigia kura Lowasa awe rais wa awamu ya tano?

A VERY GOOD QUESTION ! Sijawahi KUKUTANA NA SWALI ZURI KAMA HILI !
 
Maamuzi ya kuanzisha shule za kata zisizokuwa na uwezo wa kutoa elimu?

Maamuzi endelevu ya kwenda kutafuta mvua ya kutengeneza?

Maamuzi ya kwenda Niuzilendi ku eti kujifunza kilimo cha vitunguu?

Maamuzi ya kushiriki mikataba ya richmond ya kitapeli huku akijua eti kwa sababu hata kikwete alifahamu?

Analipi la kutuambia huyu Watanzania huyu mtu?

Hatutaki. Unafiki mtupu

Back
Top Bottom