"Kwa kuwa umepata ulichokuwa unakitaka"

Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,983
12,702
Hivi kwa nini pale uhusiano unapovunjika hawa wenzetu hukimbilia kutoa kauli hii:
"............kwa kuwa umepata ulichokuwa unakitaka...".
 
Kuna ukweli lakini:-
  • Je ulichokuwa unakitaka haujakipata?
  • Na kama ulichokuwa unakitaka umekikuta kama ulivyokitaka kwanini umuache?
Kwahiyo tunaweza kusema unamuacha sababu ulivyofikiria sivyo au umechoka unataka pengine, au ameanza kukuboa
 
Yaani mimi mwenyewe huwa nashangaa sana, unakuta wao ndio wanalazimisha uhusiano....pale mambo yakienda ndivyo sivyo wanalalamika kuwa ulikuwa unanichezea, kwa kuwa umepata ulichokuwa unakitaka....na mengine mengi. Kwani wao huwa wanataka nini???
 
Kuna ukweli lakini:-
  • Je ulichokuwa unakitaka haujakipata?
  • Na kama ulichokuwa unakitaka umekikuta kama ulivyokitaka kwanini umuache?
Kwahiyo tunaweza kusema unamuacha sababu ulivyofikiria sivyo au umechoka unataka pengine, au ameanza kukuboa
Na kama kanitongoza yeye na sio chaguo langu, hapo inaonekana kuna kitu anakitaka kutoka kwangu, inabidi nimpe ANACHOKITAKA then kila mtu aendelee na hamsini zake. sasa hapo ndio wenzetu wanaanza kulalamika!!
 
Kama alianza kukutongoza mwenyewe sawa naanza kukuelewa, huyo hatakiwi kukulaumu na wewe kwa nini ulimkubalia ilhali huna nia nae? Hata wewe ulikua unamtamani vile vile
 
..............Aliyetongozwa anahaki ya kusema hivyo, na kwa kuwa wanawake kwa kawaida ndo hutongozwa(kuna exceptions lakini) wanahaki ya kusema hivyo,ukizingatia ki maumbile na kihisia wao ni inferior mara zote.
 
Mmmh!! Sisi huwa tunaugulia maumivu kimyakimya...

Ndo hulka ya kiume.
Ila seriously, hii wanaitumia kama defence mechanism ya kukufanya uogope na walau kumuonea huruma. Incase huna maamuz firm (kama ccm) unajikuta unarudi ilhali moyo haupo hapo tena.
 
Mmmh, nyie viumbe wa kiume bwana, hata mimi ukinitongoza halafu nikikubali kwa moyo wangu wote, tena ukanibadilikia,
Lazima nikuulize ulichokuwa unakitaka umehakipata?

Kwa maana umekipata na umefanikiwa kwa kiwango ulichokusudia sasa umeamua kunimwaga. Ok Fine.....

Kama ni mimi nimekutongoza nikiona nilichokita huna, nakuambia tu, bwana eeh nilidhani waweza kuwa so and so, lakini naona haitakuwa hivyo....
So nisamehe kwa yote, tukae kwa amani. Kama nilichokitaka nimekipata na wewe kiumbe wa kiume umeridhika na hayo matakwa yangu, maisha yanaendelea.

Sasa nyie mnamtumia mtu, akili hadi na damu yake, unampotezea muda msichana wa watu halafu unamkimbia unadhani nini? Hujui mwaka mmoja wa mtoto wa kike una maana kubwa sana kwenye swala la mahusiano?

Niko na wewe nikiwa na miaka say 27, baada ya miaka 2 nina miaka 28, halafu unitupa kule.............Mmmmh ndo hapa unatamani hata kuchinja mtu.
 
Katavi bwana umeshikwa penyewunae nini? hahaha hommie kumbe waga unataka ile kitu tu? Wengine tukiacha tunabadili na makao hata contacts zote change kabisa.....
 
Kinachoulizwa ni kwamba na wewe si umemtumia mwenzio?? unadhani kwa hiyo miaka 2 wewe hujamtumia mwenzio..ni issue ya chaki na ubao..hebu fungua macho..
 
Ahahahaah!! Si hivyo mkuu, juzi nilikuwa nasuluhisha ishu ya rafiki yangu na mpenzi wake, bibie muda wote analalamika tu, "amepata alichokuwa anakitaka", mara "kanichezea".
 
Kinachoulizwa ni kwamba na wewe si umemtumia mwenzio?? unadhani kwa hiyo miaka 2 wewe hujamtumia mwenzio..ni issue ya chaki na ubao..hebu fungua macho..
Kweli mkuu kama ni kuchezeana na kutumiana, wote tumefanyiana hivyo. Inakuwaje upande mmoja ndio unaonekana umeonewa?
 
Back
Top Bottom