Kwa Kuwa Ikulu Ni Sehemu Takatifu Urais Wa 2015,Vetting Ni Muhimu Sana Kuliko Chochote KIle. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa Kuwa Ikulu Ni Sehemu Takatifu Urais Wa 2015,Vetting Ni Muhimu Sana Kuliko Chochote KIle.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DSN, Jan 10, 2012.

 1. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #1
  Jan 10, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hakika Watanzania inavyoonyesha japo si lasmi harakati za baadhi ya wanasiasa wengine kwa hiari yao wengine pasi hiari yao wameanza kampeni za kinyanganyiro kisicho lasmi cha kiti cha urais kwa tiketi ya chama tawala.

  Si vyema lakini ndio hali halisia humu jamvini kuwa kuna baadhi ya watu wanatajwa wengine zikiwa harakati zao za makusudi wengine ni kwa kusukumwa na mazingira halisi kuwa nao wamo katika kinyanganyiro hicho.

  Kwa vyombo vya Dola, Wananchi na Wanajf, hakika Urais wa mwaka 2015 vetting [If someone is vetted, they are investigated fully before being given a particular job, role, or position, especially one which involves military or political secrets.] ni muhimu sana.

  Kwani ni aibu kwa Taifa kukuta mtu anapewa madaraka makubwa ndani ya Taifa huku si raia wa Taifa,au ana makosa ya jina au hata madai.Kwa kuwa kiongozi ni mfano ni vyema basi viongozi wetu tukawapata wakiwa ni viongozi wasafi kwa mfano wa kuigwa na raia zao.

  Ni hatari na inatisha kuwapa watu madaraka ya utawala na uongozi ndani ya Serikali,Vyama vya Siasa,Vyombo vya Ulinzi na Hatari mbaya mbaya kupita zote kutokuwa na watu waadilifu au raia ndani ya vyombo viwili muhimu yani Usalama wa Taifa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania.

  Nimeona baadhi ya document za mashitaka ya mmoja wa mawazili wetu akishitakiwa na Serikali ya Marekani kwa makosa ya jinai hakika ni aibu kwa waziri kuhusishwa na matendo hayo hata japo yalifanywa nae kabla ajawa kiongozi.Ili kuepuka ilo ilipaswa Serikali iwe tayari na taarifa za Serikali ya Marekani dhidi ya Waziri wetu ikiwa ni Assurance kuwa kiongozi huyo kwa tendo ambalo alilifanya kwenye state hiyo ya USA mwaka tajwa basi wao kwao hakuna tatizo la kisheria kumnyima haki mtuhumiwa kwenye shughuri zozote zile za kisiasa na utawala.Yani kwa ujumla kwa Tanzania ilipaswa kufanya kama alivyofanywa Rage, yani mahakama zetu zilizishwe kwa viapo kutoka kwenye makosa tujue hakika mtuhumiwa yu msafi.

  Ajabu nyingine taarifa nyingine humu zinasema Laurance Masha aliepata kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani kuwa ni Raia wa Marekani,hakika ili nalo ni hatari kupita maelezo.Ndiyo masha ni damu ya Watanzania.Lakini sisi kama Taifa ni lazima kuwe na utaratibu jamani.Hivi miiko ambayo Mwalimu aliiasisi na kuijenga kwa baadhi ya watu wazima imepotelea wapi.Inakuwaje mtu asie raia anadiliki kuchukua form na kugombea udiwani au ubunge hatimae anachaguliwa kuwa kiongozi Serikalini au kwenye vyombo vyetu vya ulinzi bila kuthibitishwa uraia wake hakika usalama wetu kama Taifa kwa mwenendo huu kama ni kweli haya yanatokea sisi kama Taifa tuko Mashakani vibaya sana.

  Haijarishi ni Green Cald au nini bado sio sahihi kwa mtu aina hiyo kupewa Madaraka ndani ya Taifa hili.Hivi faida ya Green Cald kwa Watanzania ni nini? Au zaid ni hasara kwa kuwa ukinizuliza mimi binafsi ningesema inawasaidia Wamarekani kupata taarifa zetu sisi kama Taifa kupitia watu wetu wenyewe kwa vigezo ambavyo mpokeaji green cald anaona Marekani ni Bora kuliko Mother Nation.

  Nilipata kusikia nae Sugu anamilki green Cald hakika nae kama ni mmoja wao,wapigwe chini wote, kisha wapewe option ya kukana uraia kama wanachagua kuwa Watanzania basi luksa kugombea na kuchagua.Wakingangania hizo green clad waambie wakiingia Tanzania tunawapokea kama Wageni wakuja.

  Tufike sehemu Mapandikizi haya yaishe Taifa lisonge mbele kwa watu wenye moyo wa dhati kulitumikia Taifa.

  Watanzania kupitia Jamii Forum ni nafasi njema kuwalipua aina yoyote ile ya Watanzania ambao tunamashaka na uraia au wanamakosa ya jinai au walishapata kutenda makosa ya jinai na sasa wanataka madaraka.Na ujio wa vitambulisho vya Uraia tuwalipue humu humu jamvini.

  Nawasilisha
   
Loading...