Kwa kosa hili, Lowassa huji kuiona Ikulu

DARKMAN

Senior Member
Aug 23, 2012
122
85
Mimi ni mmoja wa watu wanaoamini uwezo wa kiuongozi alionao lowassa tokea zamani sana pamoja na kukataliwa na Baba wa Taifa. Uwezo wa Edward Ngoyai Lowassa katika uongozi wan chi hii uko dhahiri katika mambo mengi tu aliyoyasimamia kuanzia kwenye wizara alizozisimamia hadi alipokuwa waziri mkuu. Tena kama kungekuwa na fursa ya kuwalinganisha Kikwete na Lowassa mwaka 2005 katika mtandao wao nani awe raisi basi mimi ningemchagua Lowassa kwa kuwa alikuwa ana proven record nzuri kuliko Kikwete mwaka 2005.

Ukiongelea intergrity wakati wa uchaguzi wa 2005 kati ya lowasa na kikwete, Lowassa alikuwa na tuhuma za kuwa na utajiri usiolingana na kipato chake kama mtumishi wa uma ambazo zilikuwa hazina ushahidi wa wazi wakati Kikwete alikuwa na kashfa ya IPTL ambayo aliisaini akiwa waziri wa nishati na madini. Kashfa ya Richmond ambayo kikwete aliishikia bango kumwadhibu Lowassa ni replica ya Richmond. Mkataba wa IPTL ulisainiwa IPTL ikiwa ni briefcase company ndio wakaenta Malaysia kuwatafuta Wartisila wakaingia nao mkataba wa kuja kufunga mtambo wa megawatt 100 pale tegeta. Hata ukiangalia wanavyouza umeme tanesco ni kwamba watisila akishaingiza umeme kwenye gridi ya tanesco, mwisho wa mwezi anaandaa invoice anawapa IPTL ikiwa na price ambayo wamekubaliana na IPTL, halafu IPTL wanaandaa invoice yenye rate nyingine pamoja nay ale madude yao ya capacity charges ambayo wanaipeleka tanesco. Hata ukienda pale tegeta ofisi za IPTL utawakuta watatu tu, mkurugenzi Mageshi, Finance manager GIre na secretary. Kwa hiyo huu uzoefu wa kupiga dili za aina hii ni wa Kikwete alianza nao na IPTL akataka kupiga na Richmond

Kosa kubwa alilolifanya Lowassa la kutuletea Kikwete kuwa raisi ambalo limetugharimu watanzania kwa muda wa miaka 10 ni tosha kumuadhibu lowassa kutoiona ikulu mpaka kifo chake yeye na wanafamilia wake. Lowassa na mwnzako Rostamu mlituletea Kikwete, Rostamu ameshakimbia nchi, Lowassa hana kwa kukimbilia kwa kuwa ni wa hapahapa, Nakuhakikishia Lowassa katika ukoo wako hakuna mtu atakayekuja kuwa kiongozi wa nchi hii kutoka katika familia yako.
 
Mungu atunusuru kwenye hiki kipindi kigumu kuliko vipindi vyote nilivyo wahi kuongozwa na viongozi wengine.
 
Lowasa aliamini hana uwezo kuliko JK, ndio maana alimwachia kipindi kile ili yeye ajifunze.

Sasa role model yake ni dhaifu, mdini, uteuzi wake ni wa mafisadi, ewamzungukao ni waropoka matusi, yeye amefisadi kila kitu, JE tukimchagua si tume kwisha na vita vya wenyewe kwa wenyewe aliyoianzisha role model si itaimarika?

Wale wote waliotupa huyu wa sasa asionekane hata mmoja ikiwa pamoja na six
 
Akiwa rais sjui utasemaje tena?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Kachukue posho yako pale kinondoni manyanya.

Na wewe nenda lumumba ukachukue buku 7 yako ukale chipsi mayai, mishikaki na kinana bariiidii kabisa..ili uishi upate nguvu ya kuitumikia magamba vizuri.
 
Unaujua ugomvi wa Nape na Lowasa ? Ukilifahamu hili utaongeza sababu nyingine kwa Lowasa kutoweza kuwa kiongozi wa nchi hii ! Hata kule Monduli Mtaji wake ni Ujinga wa wamasai wa kukubali Mishikaki na pombe basi ! Waulize yale mamilioni ya Mradi wa maji yalikopotelea , ukimpata Dr Toure utayajua Mengi .
 
kwa miaka yote na maneno ya wazi ya wazee wa ccm na watoto wao kuhusu tanu yao na uhuru wa nchi na baadae ccm.angekuwa na akili angejua kuwa yee si mswahili na kamwe hakuna mswahili atampa ahsante kwa kumsaidia jk.waswahili wanajua wao ndio wanastahili fanyiwa kazi,na lowasa si sehemu ya chama hata kama ana vigezo na kafanya makubwa.Atabaki ni wa bara watokapo watumwa,makafiri na wasiotakiwa shika nchi,walimpa kavu km hakujua anadhalilisha kaskazini. Hata baada ya tangazo tolewa kuwa kaskazini wasahau. Ni dini na kanda yake tuu itamfaoya ashuhudie akina kigoda,h mwinyi,karume,vuai na wengine wakiutaka uraisi na kupewa na kamwe si yeye.

Yeye si muislam wa pwani uzao wa masherifu wa mwambao wa tanzania hadi mombasa.

Hjui kuwa nae wangependa yamkute ya mwandosya na wengine.hajui pwani ni bora watoto km malima liyeibiwa na malaya moro kuliko lowa linapokuja suala la uongozi chini ya chama cha kiswahili ccm
 
kwa miaka yote na maneno ya wazi ya wazee wa ccm na watoto wao kuhusu tanu yao na uhuru wa nchi na baadae ccm.angekuwa na akili angejua kuwa yee si mswahili na kamwe hakuna mswahili atampa ahsante kwa kumsaidia jk.waswahili wanajua wao ndio wanastahili fanyiwa kazi,na lowasa si sehemu ya chama hata kama ana vigezo na kafanya makubwa.Atabaki ni wa bara watokapo watumwa,makafiri na wasiotakiwa shika nchi,walimpa kavu km hakujua anadhalilisha kaskazini. Hata baada ya tangazo tolewa kuwa kaskazini wasahau. Ni dini na kanda yake tuu itamfaoya ashuhudie akina kigoda,h mwinyi,karume,vuai na wengine wakiutaka uraisi na kupewa na kamwe si yeye.

Yeye si muislam wa pwani uzao wa masherifu wa mwambao wa tanzania hadi mombasa.
 
Lowasa aliamini hana uwezo kuliko JK, ndio maana alimwachia kipindi kile ili yeye ajifunze.

Sasa role model yake ni dhaifu, mdini, uteuzi wake ni wa mafisadi, ewamzungukao ni waropoka matusi, yeye amefisadi kila kitu, JE tukimchagua si tume kwisha na vita vya wenyewe kwa wenyewe aliyoianzisha role model si itaimarika?

Wale wote waliotupa huyu wa sasa asionekane hata mmoja ikiwa pamoja na six

Nilinena huko nyuma na ningependa kurudia tena kwa manufaa ya wana JF wapya. "WE MAY NOT KNOW WHO WILL BE OUR NEXT PRESIDENT BUT WE KNOW WHO WILL NOT BE, IT IS EDWARD NGOYAI LOWASSA". Endeleeni kuongea mtakavyo lakini ukweli ndiyo huo!
 
Sijawahi kuota kwamba Lowassa ni Rais 2015 ila nimewahi ota kwamba ataleta mgawanyiko na mauaji.
 
Mimi ni mmoja wa watu wanaoamini uwezo wa kiuongozi alionao lowassa tokea zamani sana pamoja na kukataliwa na Baba wa Taifa. Uwezo wa Edward Ngoyai Lowassa katika uongozi wan chi hii uko dhahiri katika mambo mengi tu aliyoyasimamia kuanzia kwenye wizara alizozisimamia hadi alipokuwa waziri mkuu. .

Bwana wewe, umesahau EL alipokuwa Wizara ya Ardhi hadi Wahindi walimtuhumu kwamba ananuka rushwa na habari ikatoka magazetini? Ujue hadi mhindi anasema unanuka rushwa basi wewe ni kiboko kweli kweli. Hawa jamaa huwa wanaambiana.

Hata siku moja sintakataa kwamba EL ni kiongozi mzuri kiutendaji. Ila tatizo lake kubwa sio mwadilifu - hana "ethics" za kiuongozi, au kwa lugha nyepesi, si msafi. Anyway, labda kwa kuwa sasa kawa tajiri sana atakuwa ameridhika anaweza kutusaidia. Ila ujue tatizo la utajiri ni kama ulevi - huridhiki kamwe hata unywe kiasi gani. Kesho utataka ukanywe tena zaidi ya jana!
 
Back
Top Bottom