Uwezo Tunao
JF-Expert Member
- Nov 14, 2010
- 6,942
- 1,190
SERIKALI NA KAULI MKANGANYIKO JUU YA 'WANANCHI KUTAKA KUANDIKA KATIBA MPYA' SASA HIVI, NI ASHIRIO SAED MWEMA AGIZA MABOMU YA KUTOSHA MWAKA MPYA TUKAUANZE KABISA UWANJANI MPAKA KIELEWEKE??
Tangu CHADEMA kianzishe upya madai ya KATIBA MPYA na wananchi wengi wakatukonga nyoyo, kwingineko serikali imeshatoa kauli hamsini kidogo hadi hadi kero kwetu hivi sasa.
Kuna kauli kibao ambazo kwa kweli zinasumbua sana kuzipokea. Hii hali inatokana na hali ya mikanganya isioisha. Kila mmoja serikalini akijitokeza kwa vyombo vya habari na hili na yule nalile
Miongoni mwa kauli ambazo bado ziko vichwani mwetu ndani ya kipindi kisichozidi miezi miwili ni kama hivi hapa chini:
1. Makamba kujitokeza kasema; HAKUNA NAFASI YA KUSIKILIZWA MTU HAPA,
2. Chiligati; CHADEMA WASITULETEE UTANI HAPA, LETU NI KUWATIMUA WOTE KULE BUNGENI ili wakashike adabu,
3. Chiligati huenda akaja akakutana na Malaika; ... aaahhh, unajua haya madai ya CHADEMA ni ya msingi na YANAZUNGUMZIKA,
4. Mama Celina Kombani akaja na sura kiutawala zaidi; SUALA LA KATIBA kwetu kama Serikali HAPANA, NI GHARAMA KUBWA, MANENO YA MTAANI, NA WALA SI MUHIMU KWA SASA,
5. Mzee Tyson naye hakuondoka mdomo mkavu alipokutana na vyombo vya habari; Hili la MADAI YA KATIBA MPYA linaongeleka tu kati ya serikali na CHADEMA na wala halina shida.
Si unajua sisi kama serikali tunazo njia zetu nyingi tu za kutatua mambo kama haya. Na zaidi, zipo zile njia zetu nyingine ambazo KWA KAWAIDA HUA HATHITAJI KUZITANGAZA popote,
6. Jaji Mstaafu Mzee Bomani alipofika akanena; Suala hili ni halikwepeki na ninashauri Serikali iteue JOPO LA WATAALAM kuliangalia KATIBA na kubaini MAHITAJI yaliomo;
7. Mzee Ruksa alipofwatwa mapumzikoni kwake na waandishi wetu wa habari kwa matarajio ya BUSARA KATIKA HILI JAMBO ZITO KITAIFA nay alisema; Kwa nini Wa-Tanzania muhitaji KATIBA MPYA SASA HIVI, KUNA NINI???
8. Mwana-JF 'Dar es Salaam' inayosadikiwa kuwa ni sauti ya KIFICHONI cha aka JK naye hakutafuna maneno baada ya kuona madai na moto wa katiba mpya ni mkali ajabu, akiuliza; Nani kawambieni kwamba Mhe Kikwete mwenyewe hapendi Kuandikwa KATIBA MPYA???
8. 'Mtoto wa Mkulima' alipofika kwenye kio (TV) akaja akaweka ngoma hadharani kabla ya kukataliwa na wengi; Mimi mwenzenu nitatumia nafasi yangu kama PM kumshauri Rais ateue JOPO LA WATAALAM kuipitia katiba na kushauri HATIMA YAKE NI NINI.
9. Mama Kombani baada ya pengine kutembelewa na malaika lakini bila kutafsiri nafasi na madaraka yake KIKATIBA akageuza muziki; Jamani sasa tayarisheni na mkaniletee mezani kwangu hizo Rasimu Sifuri zenu za KATIBA MPYA kwangu ili tupate kujua cha kufanya,
10. Jaji Mkuu Augustino Ramadhani naye hakufanya ajizi mpira wa KATIBA MPYA ulipomtwa miguuni na akaelekeza ngoma moja kwa moja kwenye nyavu; Wa-Tanzania kutaka KATIBA MPYA, hili nijambo ambalo tulihitajika tuwe tumeukamilisha tangu miaka majuzi.
11. Mzee Warioba, CCM Uadilifu lakini masikini, mshabuliaji wa UFISADI asiyechoka kitu hata siku moja, akatahadharisha serikali isicheleweshe zaidi kushughulikia suala la KATIBA MPYA.
12. Mzee wa RICHMOND / DOWANS, CCM Ufisadi Mabilionea, naye baada ya kutoka kanisani siku ya jumapili akaimarisha madai ya raia wenzake kwa kusema; Kwa usalama wa nchi yetu KATIBA MPYA haikwepeki.
13. Vuai Nahodha, waziri wa mambo ya ndani ambaye amepokelewa kazini na mitihani ya uchakachuaji na kupitishwa moja kwa moja kwenye tanuri la migomo vyouni, hasira limbikizi za wananchi kutaka kuandamana kila pembe ya nchi naye akapiga magoti chini na kusema; Wananchi chonde MSILETE VURUGU NA KUANDAMANA kwani vilio vyenu kutaka KATIBA MPYA vinashughulikiwa.
14. Werema, Mwanasheria Mkuu na Mshauri Mkuu wa SERIKALI kuhusu UTUNGAJI NA UTUMIAJI SHERIA MBALIMBALI (lakini si Mshauri wa Wananchi Juu ya UTUNGAJI KATIBA) naye akatia timu kwenye kio chetu cha taifa akisema; Sasa sisi kama serikali tumepata jibu sahihi hata bila ya Jopo la Wataalam au bila hata kupeleka popote hizo RASIMU SIFURI zenu za kutaka KATIBA MPYA.
Jibu lenyewe ambalo ni sahihi kabisa na kila mwananchi LAZIMA kuikubali ni kwamba 'WATANZANIA HAMUHITAJI KUANDIKA UPYA KATIBA BALI VIRAKA TU VICHACHE VINATOSHA.
15. Wanaharakati, Asasi za Kiraia, Wakulima vijijini, Vyama Vya Wafanyakazi, Vijana, Wana-JF, Vyama vya Siasa, Taasisi za Kidini na Vyuo Vikuu nchini nao wakasema; Saa ya Kuandikwa kwa KATIBA MPYA kwa njia Shirikishi kwa wananchi wote ni sasa.
16. Kesho au keshokutwa bado hatujui atajitokeza nani tena na kauli ipi; ....
Sasa mpaka hapo wananchi, zaidi ya hasira za kudhulumiwa haki ya kumchagua kiongozi umpendaye, mpaka sasa ni maelezo mkanganyiko kushoto na kulia sasa tushike lipi? Kwa hali hii ni aheri MAFISADI watuambie kama sasa JIBU ALIYOYATOA WEREMA SASA NDIO MSIMAMO RASMI WA SERIKALI ili tujue kimoja tangu sasa.
Kwetu VIJANA vyeo wanavyovigawana leo havituhusu bali macho yetu, fikra na roho zetu kila dakika zipo kwenye KATIBA MPYA. Na kama kweli ndilo jibu na msimamo rasmi wa serikali juu ya jambo hili la msingi na wa UMUHIMU WA PEKEE HASA KWETU VIJANA na walalahoi tuliowengi nchi hii basi nasi tunaomba kumshauri murua kwenu.
Kwa kuwa HAKI hua hauombwi wala kuletwa bila ya purukushani mivutano ya kujitakia MAFISADI, na watu kibao kuzidi kutuchanganya na kauli tata toka serikalini, je inamaa tushike lipi na tuache lipi sasa??? Kama vipi, basi tumuombe mwenzetu Saed Mwema akaagize upesi MA-BOMU YA MACHOZI YA KUTOSHA ya kutosha ili Mwaka Mpya madai ya KATIBA MPYA rasmi sasa yahamie uwanjani na tuondoke kulaghaiana KWENYE BOARD-ROOMS za watawala wasiosikiliza kitu
Kwa Kauli ya Werema tujue kimoja kama tayari ndio kusema kwamba hata hoja ya wananchi kupelekwa kule Bungeni Dodoma na Mhe Mnyika ndio hivyo tayari WATAWALA watakua wanajifariji kwamba wananchi tunapoteza tu wakati.