Kwa Kauli hii ya IGP Sirro akiwa ziarani Zanzibar siyo Kielelezo tosha kuwa Police Tanzania...

Prognosticator

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
40,125
2,000
Jana alipokuwa katika Ziara ya Kujitambulisha huko Visiwani Zanzibar Mkuu mpya wa Jeshi la Polisi nchini IGP Sirro alisikika na kuonekana akiwa na hasira sana aliposema kuwa namnukuu “ Sitaki kuona ama kusikia kuna Askari wa Jeshi la Police ni Muoga / Mwoga. Hii Kazi mliitaka wenyewe sasa kwanini siku hizi kumezuka na Kundi kubwa la Askari Police waoga? Hivi kwa style hii tutaweza kupambana na Wahalifu kweli? Katika Uongozi wangu sitaki kuona au kusikia kuwa nina Askari waoga tafadhali kwani hii ni Kazi ya Kishujaa hivyo tuonyeshe Ushujaa wetu katika kuwalinda Raia na Mali zao “ mwisho wa Kumnukuu

Je kwa hii Kauli ya IGP Sirro haitoshi kuwa ni Kielelezo tosha kuwa Jeshi la Police Tanzania

1.Ni Goigoi

2.Hawana Ueledi

3.Wanapewa Mafunzo mabovu

4.Si Wazalendo

5.Wameajiri wataka Mishahara na si Watendaji / Wachapa Kazi wa Kutukuka

6.Hawajui Majukumu yao

7.Usaili wao una walakini / matataizo

Nawasilisha.
 
Evans-Arsenal

JF-Expert Member
Jan 10, 2016
868
1,000
Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dr. Ali Shein amekutana na kufanya mazungumzo na IGP Simon Sirro kwenye Ikulu ya Rais Zazibar.

Rais Shein amempongeza IGP simon sirro kwa kazi nzuri anayofanya ya kuimarisha usalama na ulinzi.
IGP sirro ameeleza kushukuru kwa ushirikiano anaoupata toka kwa serikali ya mapinduzi zanzibar na kwamba wataendelea kulinda usalama wa raia wote wa Tanzania kama inavyopaswa.
Rais Dk Alli Shein ameeleza pia mkakati wake wa kujenga nyumba za polisi na kuondoa hadha kwa wale askari waishio uraiani kupata usumbufu.

Pia Rais Dk shein amechukua nafasi hiyo kumpongeza IGP Sirro kwa kuteuliwa kwake kuwa mkuu wa jeshi la polisi nchini.
 
MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,744
2,000
Jana alipokuwa katika Ziara ya Kujitambulisha huko Visiwani Zanzibar Mkuu mpya wa Jeshi la Polisi nchini IGP Sirro alisikika na kuonekana akiwa na hasira sana aliposema kuwa namnukuu “ Sitaki kuona ama kusikia kuna Askari wa Jeshi la Police ni Muoga / Mwoga. Hii Kazi mliitaka wenyewe sasa kwanini siku hizi kumezuka na Kundi kubwa la Askari Police waoga? Hivi kwa style hii tutaweza kupambana na Wahalifu kweli? Katika Uongozi wangu sitaki kuona au kusikia kuwa nina Askari waoga tafadhali kwani hii ni Kazi ya Kishujaa hivyo tuonyeshe Ushujaa wetu katika kuwalinda Raia na Mali zao “ mwisho wa Kumnukuu

Je kwa hii Kauli ya IGP Sirro haitoshi kuwa ni Kielelezo tosha kuwa Jeshi la Police Tanzania

1.Ni Goigoi

2.Hawana Ueledi

3.Wanapewa Mafunzo mabovu

4.Si Wazalendo

5.Wameajiri wataka Mishahara na si Watendaji / Wachapa Kazi wa Kutukuka

6.Hawajui Majukumu yao

7.Usaili wao una walakini / matataizo

Nawasilisha.
Mimi naona kauli yake ni sahihi kabisa, sasa waende kibiti wakaonyeshe ushujaa wao
 
username1

JF-Expert Member
Jan 14, 2016
263
250
Ushujaa wao wanauonesha Kwa walemavu na waandishi wa habar na viongozi wa dini Arusha..... Kibiti vipi wakaoneshe ushujaa tena apelekwe yule WA kumtolea malima bunduki... Mapumbaf Sana haya ma askari ya Jeshi la polisi tz
 
Prognosticator

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
40,125
2,000
Sio kielelezo kuwa ASKARI ni goigoi, sio weledi n.k. Bali afande ametoa MSISITIZO katika UTEKELEZAJI WA KAZI

Ila Kisaikolojia Kiongozi wa Jeshi akisema ' Kauli ' kama hiyo huwa anakuwa na maana fulani au ameshagundua ' tatizo ' fulani kubwa linalowakabili. Wewe unadhani ni kwanini labda jana alipokuwa anazungumza na wale Askari Polisi Zanzibar IGP Sirro alikazia sana hilo neno la Uwoga?
 
Prognosticator

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
40,125
2,000
Sio kielelezo kuwa ASKARI ni goigoi, sio weledi n.k. Bali afande ametoa MSISITIZO katika UTEKELEZAJI WA KAZI

Kwahiyo unataka kukataa kwamba pengine IGP Sirro kwa Kauli yake hiyo ya ' Uwoga ' hajaona au kugundua tatizo lolote kwa Wapiganaji wake? Nijuavyo ni kwamba kwa kutoa tu ile Kauli huku akiwa anaikazia mno na kuonekana imemgusa na inamuumiza nadhani IGP Sirro ameshagundua kuwa tatizo kubwa la Askari wa Jeshi la Polis nchini Tanzania kwa sasa ni Uwoga wa Kutukuka.
 
Ramadhan James

JF-Expert Member
Dec 14, 2015
2,190
2,000
Hiyo ni kauli ya kiutu uzima(Askari wetu ni waoga na pia wanasahau kwa wao ni Askari Kazi yao ni kulinda Raia na Nchi bila uoga wowote!) Sirro Kazi unayo……
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom