IGP Wambura na RPC Masejo, huu ni ushauri wangu kwenu wenye nia njema

ngaiwoye

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
1,748
2,436
Mheshimiwa IGP (Mkuu wa jeshi la polisi) natumaini unaendelea vyema katika kipindi hiki ambacho ni kipindi kitakatifu kwa wakristo (quaresma) na pia ni kipindi tukufu kwa waislam (Ramadan). Amani ya Mungu iwe juu yako.

Nimelazimika kukuandikia waraka huu nikiwa na uchungu mkubwa, KUTOKANA na mambo ambayo baadhi ya polisi wammekuwa wakitufanyia sisi raia wema.

Mheshimiwa IGP, kama ujuavyo jeshi letu ni "police force" na sio "police service"..kwa mawazo yangu nilidhani kwa kuwa polisi ni jeshi, ingekuwa vyema kama wanajeshi hawa wangeishi makambini kama MAJESHI mengine. Hii ingesaidia askari polisi kutochanganyika na kuwazoea raia, hivyo kuwafanya kufanya kazi zao kwa weledi, ufanisi na haki. Huku uraiani kila mwananchi ana tabia aina mbalimbali nyingine nzuri, nyingine mbaya.

Mheshimiwa IGP kwa kuwa askari polisi nao ni binadamu kama sisi raia, tunavyoishi nao huku uraian, tunachangamana nao, tunakula nao bata, tunaoana nao, tunajenga nao urafiki, Sasa hapa kwenye urafiki na bata ndo mahali askari wetu wanakengeuka na kujikuta wanapata marafiki majambazi, matapeli, mafisadi na waonevu na kila aina ya watu ambao baadae huwatumia polisi hawa kuwasaidia pindi wanapopelekwa polisi kwa hatia mbalimbali.

Mheshimiwa IGP, KADHIA HII haipo kwa askari wadogo tu, bali ipo pia kwa askari wakubwa. Mfano Kuna askari wadogo ambao wanapenda kutenda haki lakini wanashindwa kwa sababu ya kupewa order na askari wakubwa na wao wanakuwa hawana jinsi bali kutii.

Mheshimiwa OCCIDs wamegeuza vituo hivyo kuwa mali zao. Askari (OCCIDs) hao ambao wanakuwa wamekaa sehemu kwa muda mrefu sana wanatumika kusaidia kuonea watu, kukandamiza watu, kuwanyima haki zao, na kuchelewesha haki za watu pia kusimamia uonevu. Yani OCCID anajimilikisha majukumu yote, na hii huwavunja moyo askari wadogo na pia kuwafundisha tabia mbaya. Mathalan unakuta OCCID ana rafiki yake ambaye ni mhalifu, na rafiki huyo pindi anapotenda uhalifu na kutakiwa kukamatwa, OCCID huzuia polisi kufanya kazi Yao. Na ikitokea amekamatwa huachiwa haraka na kusaidiwa Ili aonekane sio mhalifu, kitu kinachofanya wananchi walichukie kabisa jeshi la polisi. Hii ipo sana hapa nchini, lakini mheshimiwa IGP hii ipo zaidi kenye majiji makubwa zaidi Arusha inaongoza. Nayasema haya kwa sababu nimeyashuhudia kwa macho sio mara moja na nimeyasikia kwa wananchi wenzangu wakilalamika sana. Malalamiko haya Sasa yamekuwa ya muda mrefu, na HATUA za haraka zisipochukuliwa wananchi wataendelea kuumia.

Mheshimiwa IGP, natambua kwamba kuna tatizo la nyumba za makazi za askari hivyo kupelekea askari hawa kuanzisha makazi yao mitaani. Nakubali pia itatuchukua miongo mingi kumalizia tatizo hili, (la nyumba/makazi ya polisi) hivyo basi kuna haja ya kufanya jambo Ili kuwaokoa askari wetu na kuwaepusha na tamaa mbalimbali wao kama binadamu.

IKIWA NI HIVI MHESHIMIWA NAFIKIRI KUNA HAJA YA KUWAOKOA ASKARI WETU, KWA KUWAHAMISHA VITUO VYA KAZI. HII ITAPELEKEA KUWAFANYA WASIZOEANE SANA NA WAHALIFU NA WATU WASIO WAAMINIFU NA WAONEVU, NA KUSAIDIA HAKI KUPATIKANA POLISI KAMA LILIVYO LENGO LAKO AMBALO NAAMINI NI KUJENGA JESHI LA POLISI LILILO BORA KABISA.

Ujumbe huu pia uende sambamba kwa RPC wa Arusha. Kweli tunashukuru kwa kutuletea OCD mpya ambaye hakika tunaona anajitahidi sana kufanya kazi kwa weledi na ufanisi. Lakini naona ugumu atakaoupata huyu OCD ikiwa huyu OCCID ambae amekaa hapa muda mrefu na hivyo kuifanya kazi yake kwa mazoea na sio kwa kufata utaratibu wa kazi akiendelea kuwepo, ni wazi atamwangusha.

Hakika tunashukuru sana kwa kazi alizowahi kuzifanya Gwakisa na tunasikitika sana kwa mambo yake mengine, lakini kumuokoa na kumfanya arudi kwenye mstari ni kumsaidia kwa kumpa seminar elekezi, ama kama itawapendeza atafutiwe kituo kingine. Vinginevyo hali sio nzuri kabisa. Amegeuza central police Arusha kama yake. Yani yeye maamuzi yake yanaumiza watu tena bila haya wala aibu

Pia hao polisi hapo upelelezi ofisini kwa gwakisa (wp mweusi na kijana mrefu maji ya kunde) wakalishwe, waelezwe wasiwe WAKOROFI kwa wateja, wasiwe na tamaa ya vihela vidogovidogo, Yani wamegeuza kukamatwa watu ni biashara. Kutwa kuomba hela kwa watu wakawakamatie watu wao, na walifika huko wanaharass watu na unakuta hata mtu kumbe Hana kosa. Wp ni mweus, amenyoa nywele kaweka kalkiti. Na WA kiume sio yule James, ni mrefu mweusi na Kila mara utawakuta na huyu wa kalkiti wakiwa kwenye biashara Yao ya kukamatwa raiya kwa kulipwa fedha.
Afande RPC, je Evarest ameenda wapi?? Yeye akiwa pale at least anajielewa na kusukuma mambo ambayo kimsingi yamemshinda Gwakisa.

TUNAOMBA SANA TUWAOKOE ASKARI WETU KWA WEMA ILI WANANCHI TUTII SHERIA BILA SHURTI.

Nawatakia kazi NJEMA na majukumu mema ya kukijenga TAIFA

Ngaiwoye, Leo nipo Temii
 
moja ya majeshi yanayofanya kazi kwa mazoea ni hilo mojawapo

nilienda kuripot muhalifu nikaulizwa kama nina hela ya mafuta ili tuwashe tenga tumfate muhalifu

nikasema stupid kama sa100
Yani dada afande alienyoa nywele fupi akawela kalkiti ndo kazi zake hizo. Yani kafanya ndio biashara. Akilipwa aende kwa huyo mtuhumiwa Sasa, utasema tuhuma zishathibitishwa.

Anageuza wananchi wenye shida na huduma za jeshi la polisi kama saccoss yake. Na mwenzake wa kiume, very smart boy, lakini saasaa
 
Back
Top Bottom