Kwa kasi hii ya Rais Magufuli nashindwa kuelewa mzee Mwinyi alifeli wapi hadi viwanda na mashirika ya umma yakafa!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,937
141,909
Nafuatilia kwa makini jinsi taasisi za serikali zinavyozidi kujitokeza kutoa gawio (dividends) kwa serikali.

Nimeona hadi vyuo kama SUA, IFM nk vikitoa gawio sambamba na wakala mbalimbali za serikali na hata vitega uchumi vilivyoko jeshini na magereza mfano Suma JKT.

Natafakari tu endapo Rais Magufuli ndio angekuwa aliachiwa yale maviwanda kama Kiltex, Sunguratex, Tbl,Bora nk....nk....yaani ile Pugu road yote vilikuwa viwanda vya serikali, hakika naamini leo tungekuwa mbali sana.

Najiuliza tu mstaafu Mwinyi alikwama wapi hadi viwanda na yale mashirika makubwa makubwa akina NBC NIC, THB nk yakafilisika?

Nawatakia Dominika njema

Maendeleo hayana vyama!
 
Tumwache Mzee Mwinyi apumzike hata km aliteleza yaneshapita hayo, hatuwezi kuyarudisha nyuma

Ili mradi tumepata Rais Mzalendo kila kitu kitakaa sawa
Historia ni mwalimu mzuri tusije tukarudia makosa!

Mzee Mwinyi ndiye baba wa demokrasia.

Maendeleo hayana vyama!
 
Duh mkuu ina maana hujui nyerere alimkabidhi mwinyi nchi haliyakuwa imemshinda...? That we were in survival mode...? Nchi hata kujinunulia chakula ilikua tabu ndo iwe hayo mambo mengine..?

Sent using Jamii Forums mobile app
Heshima yako mkuu umenena vyema. Mtoa mada inabidi atambue inawezekana kumsifia MTU pasipo kumchafua mwingine. Tanzania ya wakati wa Mwinyi ilikuwa imetoka vitani na serikali haikuwa na pesa muda huo.
Pia economic system ya Mwinyi na economic system ya JPM ni vitu viwili tofauti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbuka kipindi cha mwinyi
1.SAP ndio ilikuwa iko hot
2. Kumbuka viwanda vilijengwa na kuongozwa kwa mfumo wa kiujamaa ndio maana kulikuwa na viwanda vingi vya ushilika
Tangia nchi ipate uhuru mwalimu aliongoza kwa mfumo wa kiujamaa ambao kwa mabeberu walipinga ilifikia hatua hadi kuujumu bizaa zitokazo ndani ya Tanzania kwani kulikuwa na jumuiya ya Africa mashariki ambapo anguko lake nimoja ya ujuma iliyo fanywa
Wenzetu kenya na Uganda mifumo yao haikuwa ya kijamaa
Ujuma nyingne ilikuwa ni anguko la azimio la Arusha.

Hadi mwalimu anatoka madarakani Tanzania tulikuwa na vikwazo vya uchumi ndio maana sera ya mwinyi ikawa rukusa walau kufungua mianya ya uchumi ingawaje haikuzaa matunda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu mradi ulivurugwa na Jiji la Dsm......nadhani umenielewa.

Lakini mambo yamerekebishwa na serikali inategemea gawio soon!
Mkuu mambo gani yamerekebishwa, huduma ni mbovu mno abiria wanasubiri vituoni kwa muda mrefu huku mabasi yakipita tupu, magari pia ni mabovu mno ,

Kimsingi ni swala la muda tu kabla hatujauzika rasmi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom