Kwa kasi hii ya Magufuli, Lowassa anapoteza pesa zake na CHADEMA, CHADEMA wanapoteza muda na Lowassa

Wakati mnaendeleza ujinga wenu Magufuli anayeshikiria rekodi ya kuwa na akili nyingi kwa mwaka 2015/2020 kuwazidi CCM wote anaendelea kuchapa kazi kwa kutumia ilani na sera za UKAWA,wananchi tunachohitaji ni maendeleo,UKAWA tunachofurahia ni kujitambua kwa Magufuli kuwa ilani na sera za UKAWA ndilo jibu pekee la kuwaletea wananchi maendeleo.

Mkuu nmeona umegusia ilani ya ukawa? Ivii mlikuwa nayo kumbe hiyo ilani maan kwenye majukwaa mzee wa deko hakuweza kuinadi wala kuionyesha hiyo ilani zaidi ya maigizo
 
Mkuu nmeona umegusia ilani ya ukawa? Ivii mlikuwa nayo kumbe hiyo ilani maan kwenye majukwaa mzee wa deko hakuweza kuinadi wala kuionyesha hiyo ilani zaidi ya maigizo

Aaa kama hukuiona Magufuli kaiona ndio maana ana itekeleza kwa vitendo.
 
Eti upinzani kufa Akili ya kuku hiyo, mbona club ya Liverpool haijachukua ubingwa zaidi ya miaka 25 na bado INA wapenzi na washabiki dunia nzima, sasa upinzani unaogusa itikadi na tofauti ya Sera na utekelezaji wake utakufa vipi? Ccm wanajidai ni wajamaa, cdm nguvu ya umma, sioni kifo cha upinzani hapo,
Wakati mwingine muwe mnatafari kabla ya kupost mautumbo, siyo kila member humu in mpuuzi kama vijana wa lumumba
 
Kama kuna jambo ambalo hatupaswi kulipuuza basi ni upinzani pamoja na Viongozi wa upinzani.JPM anachokifanya sasa ni jitihada za muda mrefu za kambi ya upinzani katika kuliletea Taifa maendeleo.JPM anahitaki mawazo ya upinzani zaidi kuliko ya chama chake cha Mapinduzi..Amini nakuambia; UKAWA itaimarika zaidi kipindi hiki kuliko wapiga dili wa CCM ambao watakuwa busy kuficha mali zao na kutafuta mahali pa kujificha.
UPINZANI chini ya FISADI LOWASSA siyo upinzani tena, ni genge la kujinyakulia pesa tu.
 
Eti upinzani kufa Akili ya kuku hiyo, mbona club ya Liverpool haijachukua ubingwa zaidi ya miaka 25 na bado INA wapenzi na washabiki dunia nzima, sasa upinzani unaogusa itikadi na tofauti ya Sera na utekelezaji wake utakufa vipi? Ccm wanajidai ni wajamaa, cdm nguvu ya umma, sioni kifo cha upinzani hapo,
Wakati mwingine muwe mnatafari kabla ya kupost mautumbo, siyo kila member humu in mpuuzi kama vijana wa lumumba

umesomeka, CHADEMA ni sawa na CLUB ya LIVERPOOL KABISAAAA.
 
Lowassa alikuwa Waziri Mkuu kwa zaidi ya Miaka Miwili - lakini hakuwahi kufikia hata nusu ya mafanikio aliyoyafikia Magufuli kwa siku 25 tu.

hebu nitajie hayo mafanikio kwa siku 25...ameanza vizuri Rais wetu. Makini kusema wamepata mafanikio zaidi ya ile miaka 2 ya Lowassa ni hyper reality.
 
Hapana shaka kabisa kwa kasi hii ya Rais Magufuli ya kuirudisha nchi katika mstari ulionyooka ni wazi kuwa kuelekea 2020, ni wazi LOWASSA anapoteza pesa tu kwa chadema huku CHADEMA wakipoteza muda na LOWASSA.Lowassa alivyo na uchu wa madaraka pengine anaamini bado ana nafasi ya kuingia ikulu mwaka 2020, kwa kasi hii, anaota ndoto ya mchana. CHADEMA nao kwa sababu ya LOWASSA kuwasaidia kupata viti vingi vya Wabunge na hata kura za urais ukilinganisha na chaguzi zingine zote walizwahi kushiriki, nao huwenda wanaamini, kupitia LOWASSA bado wanaweza kupata nafasi ya kuingia IKULU. Kwa kasi hii ya MAGUFULI , ndoto ya mchana.Dalili ya mvua ni mawingu. kwa sababu ya moto wa Magufuli, CHADEMA wameahama kabisa kwenye agenda za kisiasa kwa maendeleo ya taifa na kuhamia kwenye agenda za kutafuta umaarufu wa mambo ya ajabu ajabu tu. Kufungua kesi za kutaka kuaga maiti kwenye viwanja vya hadhara, kudhalilisha maiti na watoto wa marehemu kwa kuwapandisha kwenye majukwaa yakisiasa eti nao wahutubie , siyo agenda za maendeleo tena, huku ni kuingiwa na hofu ya kasi ya Magufuli, ni kutaka kufunika tu kasi ya uongozi mpya ulioko katika madaraka ya nchi.TAFAKURI YANGU KUHUSU KASI YA JPM NA SIASA WANAZOFANYA CHADEMA1. Lowassa anapaswa kufikiri upya anachokitafuta kuelekea 2020, kama ni uras anapoteza muda na pesa zake bure, lakini kama anakisaidia chama, ni vema, hizo ni fedha za umma , ameliibia sana Taifa hili, siyo vibaya akizirudisha kwa njia hiyo.2. CHADEMA kama wanaaamini 2020 kupitia LOWASSA wanaweza kuingia ikulu, wanapoteza muda, wanatakiwa waanze kumtafuta mwana CCM Mwingine anayeweza kupambana na JPM 2020(historia inawahukumu, mgombea wao lazima atoke CCM) na siyo fisadi LOWASSA. Lakini kama wameamua KUFYONZA PESA ZA WALIPA KODI ambazo LOWASSA aliwaibia kipindi chote alichokuwa mtumishi wa UMMA na CCM, nawapa hongera kwa hilo. ONYO: pesa hizo wanazofyonza kutoka kwa LOWASSA zitumike kwa manufaa ya CHAMA na kwa maana hiyo kwa maendeleo ya taifa na siyo ziwanufaishe watu wachache.3. NI ONYO TU KWA CHADEMA: MAGUFULI akiendelea na kasi hii, kwa takribani mwaka mmoja tu(leo ana siku 25 tu), siku akigeukia kukijenga chama kwa manaa ya kupita kwa wananchi kama kiongozi wa CHAMA na siyo Rais, kuna uwezekano mkubwa sana wa kuzoa hata viongozi wa kitaifa wa CHADEMA na UKAWA kwa ujumla(nimesikia KATIBU WA BAWACHA/BAVICHA MKOANI PWANI KAHAMIA CCM TAYARI) na huo ukawa mwisho wa CHADEMA na UPINZANI kwa ujumla.
UMESEMA uhalisia wenyewe, ni suala la muda tu.
 
Ulichokiandika unakielewa? Wew unadhani isingekuwa team Lowasa kumpgia Mh. JP ktk kura za maoni JP angekuwa raisi wa nchi hii? Unajua Mh. JPM alikuwa team EL before? Wew unadhani JPM ana bifu yeyote na EL? kwa mawazo yako unadhani watz wanahitaji mabadiliko ya watu au mabadiliko ya maswala? Kajipange upya mkuu au urudi tena.
 
kwakweli hata wavue nguo lazima magufuli awapeleke puta Lowasa ataishia pabaya sana.
 
Lowassa alikuwa Waziri Mkuu kwa zaidi ya Miaka Miwili - lakini hakuwahi kufikia hata nusu ya mafanikio aliyoyafikia Magufuli kwa siku 25 tu.

sahihi kabisa Lowasa tangu aingie kwenye siasa hajawahi fanya la maana hata moja zaidi ya wizi na ufisadi.
 
Hoja kuntu majibu dhaifu. Wenye UKAWA walikimbia harufu chafu. Hoja safi zililetwa mezani na Dr. Slaa, prof.Lipumba,ZZK ikafunikwa na ENL,Kingunge,Mwapachu na Sumaye. Mnisamehe,haturudi nyuma tunaweka kumbukumbu sawa. Si haki hata CCM kuamini kuwa Chenge,Tibaijuka wanamtazamo sawa na JPM.
 
Wajinga utawajua wanamshabikia Magufuli bila kujua anatekeleza ILANI ya CHADEMA siyo ya ccm tena.
 
Wajinga utawajua wanamshabikia Magufuli bila kujua anatekeleza ILANI ya CHADEMA siyo ya ccm tena.
Wewe ilani ya CHADEMA uliiona wapi, wakati hata Lowassa mwenyewe alishindwa kuielezea pale jangwani siku ya ufunguzi wa kampeni. Ilani ya Chadema ipi, ya 2010 au 2015. Ilani ya Chadema ya Slaa au ya Lowassa? CHADEMA walikuwa na agenda ya kushughulika na mafisadi?
 
Back
Top Bottom