Kwa kasi hii ya Magufuli, Lowassa anapoteza pesa zake na CHADEMA, CHADEMA wanapoteza muda na Lowassa

hebu nitajie hayo mafanikio kwa siku 25...ameanza vizuri Rais wetu. Makini kusema wamepata mafanikio zaidi ya ile miaka 2 ya Lowassa ni hyper reality.

Sasa kukamata makontena ambayo hayajalipiwa ushuru si mafanikio?? Kukata matumizi yasiyo ya lazima ambayo yanaweza kutengeza lami kilimota 400 si mafanikio?? Au kwao mafanikio ni nini???
 
Wakati mnaendeleza ujinga wenu Magufuli anayeshikiria rekodi ya kuwa na akili nyingi kwa mwaka 2015/2020 kuwazidi CCM wote anaendelea kuchapa kazi kwa kutumia ilani na sera za UKAWA,wananchi tunachohitaji ni maendeleo,UKAWA tunachofurahia ni kujitambua kwa Magufuli kuwa ilani na sera za UKAWA ndilo jibu pekee la kuwaletea wananchi maendeleo.

JPM anatumia sera nyingi za Mwl Nyerere kama sera ya viwanda ambayo vilikuwa kipindu cha nyerere na vikaleta maendeleo.....na pia anatumia dira ya maendeleo ya 2025 sema ndo kuna baadhi ya njia ambazo anazitumia kufikia hayo malengo anatumia njia za nyerere ambazo zimekuwa zikisemwa sana na UKAWA....
 
Sasa kukamata makontena ambayo hayajalipiwa ushuru si mafanikio?? Kukata matumizi yasiyo ya lazima ambayo yanaweza kutengeza lami kilimota 400 si mafanikio?? Au kwao mafanikio ni nini???

Kurejesha nyumba zote za Serikali na kurejeshwa pesa iliyonunua kivuko kibovu cha 1978 na Serikali ihamie Dodoma haraka na kupunguza misafara na foleni jijini Dsm hayo ndiyo mafanikio ya kweli.
 
Hapana shaka kabisa kwa kasi hii ya Rais Magufuli ya kuirudisha nchi katika mstari ulionyooka ni wazi kuwa kuelekea 2020, ni wazi LOWASSA anapoteza pesa tu kwa chadema huku CHADEMA wakipoteza muda na LOWASSA.

Lowassa alivyo na uchu wa madaraka pengine anaamini bado ana nafasi ya kuingia ikulu mwaka 2020, kwa kasi hii, anaota ndoto ya mchana.

CHADEMA nao kwa sababu ya LOWASSA kuwasaidia kupata viti vingi vya Wabunge na hata kura za urais ukilinganisha na chaguzi zingine zote walizwahi kushiriki, nao huwenda wanaamini, kupitia LOWASSA bado wanaweza kupata nafasi ya kuingia IKULU. Kwa kasi hii ya MAGUFULI , ndoto ya mchana.

Dalili ya mvua ni mawingu. kwa sababu ya moto wa Magufuli, CHADEMA wameahama kabisa kwenye agenda za kisiasa kwa maendeleo ya taifa na kuhamia kwenye agenda za kutafuta umaarufu wa mambo ya ajabu ajabu tu.

Kufungua kesi za kutaka kuaga maiti kwenye viwanja vya hadhara, kudhalilisha maiti na watoto wa marehemu kwa kuwapandisha kwenye majukwaa yakisiasa eti nao wahutubie , siyo agenda za maendeleo tena, huku ni kuingiwa na hofu ya kasi ya Magufuli, ni kutaka kufunika tu kasi ya uongozi mpya ulioko katika madaraka ya nchi.

TAFAKURI YANGU KUHUSU KASI YA JPM NA SIASA WANAZOFANYA CHADEMA
1. Lowassa anapaswa kufikiri upya anachokitafuta kuelekea 2020, kama ni uras anapoteza muda na pesa zake bure, lakini kama anakisaidia chama, ni vema, hizo ni fedha za umma , ameliibia sana Taifa hili, siyo vibaya akizirudisha kwa njia hiyo.

2. CHADEMA kama wanaaamini 2020 kupitia LOWASSA wanaweza kuingia ikulu, wanapoteza muda, wanatakiwa waanze kumtafuta mwana CCM Mwingine anayeweza kupambana na JPM 2020(historia inawahukumu, mgombea wao lazima atoke CCM) na siyo fisadi LOWASSA. Lakini kama wameamua KUFYONZA PESA ZA WALIPA KODI ambazo LOWASSA aliwaibia kipindi chote alichokuwa mtumishi wa UMMA na CCM, nawapa hongera kwa hilo.

ONYO: pesa hizo wanazofyonza kutoka kwa LOWASSA zitumike kwa manufaa ya CHAMA na kwa maana hiyo kwa maendeleo ya taifa na siyo ziwanufaishe watu wachache.

3. NI ONYO TU KWA CHADEMA:
MAGUFULI akiendelea na kasi hii, kwa takribani mwaka mmoja tu(leo ana siku 25 tu), siku akigeukia kukijenga chama kwa manaa ya kupita kwa wananchi kama kiongozi wa CHAMA na siyo Rais, kuna uwezekano mkubwa sana wa kuzoa hata viongozi wa kitaifa wa CHADEMA na UKAWA kwa ujumla(nimesikia KATIBU WA BAWACHA/BAVICHA MKOANI PWANI KAHAMIA CCM TAYARI) na huo ukawa mwisho wa CHADEMA na UPINZANI kwa ujumla.

Upinzani upo kwa ajili ya maendeleo ya watu wote, usije kuombea upinzani ufe au uwe legelege kwani serikali itajisahau na italala. Uchaguzi umekwisha lakini upinzani wapo na wataendelea kutoa sera na njia mbadala za kuleta maendeleo nchini
 
Lowasa hakuwa Rais hakuwa na maamuzi ya mwisho Waziri mkuu na Rais wapi na wapi? Billion 250 zilipotea wizara ya Ujenzi kwa kulipwa makandarasi hewa kivuko cha 1978 kilinunuliwa kwa billion 8 Mbona hamkumwita Magufuli Fisadi? Nyumba Serikali ziliuzwa na Magufuli zingine akagawa kwa michepuko Mbona hamkumwita Fisadi, Acha kukariri Akili za Membe na Nape jifunze kutafakari kwanza.
Kweli we Minyoo
 
Kati ya ahadi za mwanaTANU ambazo CCM ilirithi ni hizi
1_nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko
2_rushwa ni adui wa haki sitatoa wala kupokea.
Haya mambo yapo toka kitambo mtu kujisifia kuwa ameasisi au anatimiza ilani ya chama Kingine sidhani kama ni sahihi.
 
CDM haipo baada ya 2020. Watapotezana sana. Naamini wengi watapigwa mitaloni. Siasa wanazofuata sasa si za kiushindani. Na hii ilitabiliwa mwanzo kuwa wamekosea kumchukuwa jamaa. Inawezekana Dr Slaa angesimama pasingekuwa panaonekana gap kama hili la kisiasa maana inawezekana kuwa Magu asingeonyesha kasi hii. Hii kasi ni ya kukomoa mtu.

Vijana sahizi wabishi tu ndo wanaongea Chadema mitaani. Waelewa wanaitikia "Hapa Kazi Tu".
Hapana shaka kabisa kwa kasi hii ya Rais Magufuli ya kuirudisha nchi katika mstari ulionyooka ni wazi kuwa kuelekea 2020, ni wazi LOWASSA anapoteza pesa tu kwa chadema huku CHADEMA wakipoteza muda na LOWASSA.

Lowassa alivyo na uchu wa madaraka pengine anaamini bado ana nafasi ya kuingia ikulu mwaka 2020, kwa kasi hii, anaota ndoto ya mchana.

CHADEMA nao kwa sababu ya LOWASSA kuwasaidia kupata viti vingi vya Wabunge na hata kura za urais ukilinganisha na chaguzi zingine zote walizwahi kushiriki, nao huwenda wanaamini, kupitia LOWASSA bado wanaweza kupata nafasi ya kuingia IKULU. Kwa kasi hii ya MAGUFULI , ndoto ya mchana.

Dalili ya mvua ni mawingu. kwa sababu ya moto wa Magufuli, CHADEMA wameahama kabisa kwenye agenda za kisiasa kwa maendeleo ya taifa na kuhamia kwenye agenda za kutafuta umaarufu wa mambo ya ajabu ajabu tu.

Kufungua kesi za kutaka kuaga maiti kwenye viwanja vya hadhara, kudhalilisha maiti na watoto wa marehemu kwa kuwapandisha kwenye majukwaa yakisiasa eti nao wahutubie , siyo agenda za maendeleo tena, huku ni kuingiwa na hofu ya kasi ya Magufuli, ni kutaka kufunika tu kasi ya uongozi mpya ulioko katika madaraka ya nchi.

TAFAKURI YANGU KUHUSU KASI YA JPM NA SIASA WANAZOFANYA CHADEMA
1. Lowassa anapaswa kufikiri upya anachokitafuta kuelekea 2020, kama ni uras anapoteza muda na pesa zake bure, lakini kama anakisaidia chama, ni vema, hizo ni fedha za umma , ameliibia sana Taifa hili, siyo vibaya akizirudisha kwa njia hiyo.

2. CHADEMA kama wanaaamini 2020 kupitia LOWASSA wanaweza kuingia ikulu, wanapoteza muda, wanatakiwa waanze kumtafuta mwana CCM Mwingine anayeweza kupambana na JPM 2020(historia inawahukumu, mgombea wao lazima atoke CCM) na siyo fisadi LOWASSA. Lakini kama wameamua KUFYONZA PESA ZA WALIPA KODI ambazo LOWASSA aliwaibia kipindi chote alichokuwa mtumishi wa UMMA na CCM, nawapa hongera kwa hilo.

ONYO: pesa hizo wanazofyonza kutoka kwa LOWASSA zitumike kwa manufaa ya CHAMA na kwa maana hiyo kwa maendeleo ya taifa na siyo ziwanufaishe watu wachache.

3. NI ONYO TU KWA CHADEMA:
MAGUFULI akiendelea na kasi hii, kwa takribani mwaka mmoja tu(leo ana siku 25 tu), siku akigeukia kukijenga chama kwa manaa ya kupita kwa wananchi kama kiongozi wa CHAMA na siyo Rais, kuna uwezekano mkubwa sana wa kuzoa hata viongozi wa kitaifa wa CHADEMA na UKAWA kwa ujumla(nimesikia KATIBU WA BAWACHA/BAVICHA MKOANI PWANI KAHAMIA CCM TAYARI) na huo ukawa mwisho wa CHADEMA na UPINZANI kwa ujumla.
 
Kwa hiyo Unataka kusema 1st world hakuna upinzani sio? Jiongeze acha uraza
 
Uko sawa, ila anachosema mleta maada ni juu ya uimara wa upinzania hasa baada ya Magu kufanyika kazi hoja zao. Hii inamaana kuwa panatakiwa nguvu mpya upinzani na hii inahitaji kusimamia hoja zitakazokuwa za msingi zaidi si zile za hata Sugu na Lema anaweza kuchangia.Tunajua hali itakuwa ngumu, itabaki kwa wale wanaotafuna maandishi tu na si kukurupuka na kutaja taja tu matukio.

Hili ndo hata mimi naliona. Kama hamna watu wa nguvu, hoja za upinzani zinaweza zikapoza mwaka huu. Mpaka watafute gia mpya.
upinzani n muhimu katika nchi yoyote inayohitaji maendeleo chanya; kama si upinzani kupiga kelele miaka iliyopita kuhusu upotevu wa fedha za umma hakuna ambaye angejua kwamba kuna wizi serikalini; mleta mada naomba nikukumbushe kwenye sakata pesa Epa Dr. slaa alibezwa na hao hao CCM kwamba hoja aliyoleta haina ukweli wowote na hakukuwa na pesa iliyoibiwa. Umoja wa ulaya ukaibana serikali ifanyie
uchunguzi madai ya upinzani la sivyo watasitisha misaada kwa nchi. nakumbuka kwa Shingo upande serikali ikafanya hivyo na wananchi wengi wakatolewa tongo tongo juu ya wizi ulokuwa ukifanyika serikalini. Anachofanya magufuli n matokeo ya kelele za wapinzani na si ya chama chake; tunampongeza kwa hilo! lakn upinzan n muhimu kuendelea kuibana serikali; maeneo ya upigaji yapo mengi mno na inahitaji watu makini wa kukemea uozo huo! wapiganaji hao si wengne Bali n wapinzani; Wabunge wa Ccm kazi yao tunaijua n kupiga makofi na kupitisha mambo kwa ushabiki bila kuangalia maslahi mapana ya nchi!
 
Wamefanikiwa vipi? We unaona waliompigia Lowassa ni wanachama wa Chadema au ni wale waliokuwa wafuasi wake? na kama ni hivyo, unafikiri baado wataendelea kumfuata wakati Magu anatekeleza waliyokuwa wanataka?

Amini kimoja tu kuwa watu walikuwa hawana na imani na CCM na si Magu. Na walisema Magu hatafanya lolote chini ya CCM. Na upande wa Lowassa watu walimwamini yeye si chadema kama unavyofikiri.

Kwa sasa unaweza kuta zaidi ya 70% ya waliompigia kura Lowassa wanampigia Magu.
Hakuna pesa inatoka kwa Lowasa hizo Story zilitengenezwa na Membe na Nape ili kumchafua lowasa aonekane amenunua chadema lakini wajinga wachache wamekariri Akili za nape pasipo kuchanganya na zao hadi leo , lakini wajanja wengi wanajua Lowasa alikuwa na watu wengi ndiyo maana chadema wakamwalika ahamie kwao ili wapate wanachama wengi jambo ambalo wamefanikiwa.
 
Kama kuna jambo ambalo hatupaswi kulipuuza basi ni upinzani pamoja na Viongozi wa upinzani.JPM anachokifanya sasa ni jitihada za muda mrefu za kambi ya upinzani katika kuliletea Taifa maendeleo.JPM anahitaki mawazo ya upinzani zaidi kuliko ya chama chake cha Mapinduzi..Amini nakuambia; UKAWA itaimarika zaidi kipindi hiki kuliko wapiga dili wa CCM ambao watakuwa busy kuficha mali zao na kutafuta mahali pa kujificha.

mkuu mbona unadanganya. angalia vipaumbele vya tingatinga na vya rais aliyeshindwa. edo aliwaahidi kina mama wa chadema wakati wa kampeni kuwa kama angeshinda wangeenda ngurdoto kujimwaga wakati mwenzake kapiga marufuku starehe na fahari zake zote. hapo ndiyo unasema anatekeleza ilani ya ukawa? unatudanganya
 
Lowassa alikuwa Waziri Mkuu kwa zaidi ya Miaka Miwili - lakini hakuwahi kufikia hata nusu ya mafanikio aliyoyafikia Magufuli kwa siku 25 tu.

Mamlaka ya Uwaziri Mkuu yanashahibiana na malaka ya Rais? By the way nipe output (na sio process) ya alichokifanya JPM ndani ya siku 25? Labda ni wagonjwa kulalia vitanda pale muhimbili.
Tusihalaishe takwimu za kimtaifa zinazoonyesha Wananchi wa TZ wana IQ ndogo. Kipimo cha JPM sio siku 25 au miezi 6 ndani ya siku 1825. Tutampima mafanikio ya JPM ndani ya siku 1825 kwa output yake na si processing au input yake.
 
Ifike kipindi watanzania wenzangu muwe na mtazamo makini, hivi magufuli kuna sera yoyote anayo tekeleza ya CCM? I doubt that, na mnajua upizani umeleta mafanyikio kwa Tanzania hata kuliko CCM yenyewe? Kila anachofanya magufuli ni kwa sababu ya upinzani.

Na mtoa mada kwa kwl na sikitika sana kwa ww kusema kwamba wapinzani wanapoteza muda na Lowasa na Chadema wanakula pesa za Lowasa na Lowasa ni fisadi? OK sawa Lowasa ni fisadi do u have evidence for your allegations or u are a fool led by instincts just like an animal ama a man with brains?

Hebu acha ushabiki be real and speak sense si nonsense tu. Kumbuka we are in the 22 century where knowledge is what we aspire not madness and stupidity of the highest degree.

And something else don't judge a book by its cover, as we did that with JK and we ended up in the dark. So before u write anything be critical and be wise nice time Comrades.

Kama anatekeleza sera za upinzani jiungeni nae...
 
Mtoa mada sio mzalendo,bali ni shabiki tena usiyejitambua na siasa unaipandia kwa mbele,na unapoleta mada jaribu kufanya tafiti na sio kukurupuka kama mfungwa.Ukawa wako vizuri na kama Magufuli anafanya mema kwa nini tumpinge,kama nyie masisiem mwanzo mlidai safari za nje ni faida na tukazipinga mkatucheka,leo magufuli kasema safari za nje zimetuingizia hasara unataka ukawa waseme tunataka safari za nje?Akifanya yaliyomema tutamsupport,huoni kama sisiem ndio imehamia ukawa,kaa chini na utafakari.
 
Sasa hizo siku 1825 ndani yake si ziko 25 pia?? Output ni upatikani wa huduma ambazo zilikuwa hazipo pale Muhimbili. Output nyingine ni hawa jamaa ambao walikuwa wanatafuna kodi kukamatwa;output nyingine ni savings kwenye matumizi ya safari ya nje. Na output kubwa tunayoisubiri ni hizi kodi za kontena 349 zilipwe. Inaonekana hiyo "Operations Mgt" au "Organization Behaviour" unayoisoma imekufanya ujione une IQ kubwa sana kuliko kila mtu??
 
Back
Top Bottom