Kwa jinsi navyoona, naona mama apumzike 2025 kulinda heshima yake

Mikelele kelele inakuja kwa sababu hizi

1) Ni Mzanzibari
2) Ni Muislam
3) Ni Jinsia Yake
Naona wana Jf wamekupuuza kila uzi unaohusi madhaifu ya Rais Samia na serikali yake haiwi comment yako ila ni hiyo.

Basi kwa taarifa yako wapo wanawake wengi ,wanzanzibar hadi sisi waislamu ambao hatumuelewi sasa sijui utatuweka kundi lipi chagua mwenyewe..
 
Uko sahihi. Mama anapaswa kupata muda wa kupumzika na kutunza legacy yake. Nchi hii inahitaji watu vichwa wenye kupambana na mikiki hii inayoendelea. Kwa mtu ambaye umri umeenda sana anaweza kujitafutia matatizo ya kiafya kutokana na stress ya kuongoza watu wasioridhika.

Kwa mtu yeyote mwenye kujali afya ya kiongozi wake, lazima atamshauri Mama kupumzika 2025.
Acha uvivu,fanyakazi,watu wavivu kwa kulalamika,hamuwezekani.
 
Ongezeko la bei la vyakula sio jambo la kishangilia hata kidogo. Chakula ndio hitaji kuu katika mahitaji muhimu ya binadamu kuliko hata malazi-bei za vyakula zinavyopaa unatengeneza anguko baya sana la kiuchumi.
Hawa mamluki wamezidi sana awamu hii...Useless and stupid fools mocking on fellow Tanzanians for no sane reason.
 
Naona wana Jf wamekupuuza kila uzi unaohusi madhaifu ya Rais Samia na serikali yake haiwi comment yako ila ni hiyo.

Basi kwa taarifa yako wapo wanawake wengi ,wanzanzibar hadi sisi waislamu ambao hatumuelewi sasa sijui utatuweka kundi lipi chagua mwenyewe..

Wanaopuuza ni watoto waliozaliwa juzi au waliokuja mjini siku za karibuni. Siye tunaoijua hii nchi tunaelewa maana tuliona yaliyompata Mzee Mwinyi na leo tunayaona yanayompata SSH.
 
Kazi unaifanya wewe tu Tanzania nzima? Usiwe kama K!
Watu wavivu ndio kazi yenu kulalamika,Asiyefanyakazi asile.
Fanyakazi,kama utapata mda wa kulalamika.
Wengi,mnaolalamika hamfanyikazi,mnataka mkulima alime,halafu awauzie mahindi,bei ya kutupa,nenda kalime wewe,uje uuziwe wavivu wenzako,bei ya kutupa.Acha uvivu.
 
kiujumla mama anakiamini kile kikundi cha Msoga gang kuwa kitampa uraisi hata kama wananchi wasipo mpigia kura huo ndoo ukweli mchungu.
Huo ndio ukweli, na hata wanasiasa wa upinzani wanalijua hilo. Hata mimi naamini hivyo, mama atakua Raisi 25 hatakama hamkumchagua.
 
Acha kutuaminsha uongo. Wakulima wanaenjoy Sasa hivi. Jpm aliharibu mazao yote mbaazi, korosho, tumbaku. Kwa Sasa siko ni la uhakika. Sisi wakulima mama anatufaa Sana. Pili wafanyabiasha huwaambii kitu kwa mama mana hakuna anyevamua accounts zao Tena na biashara ni nzuri Sana. Nyie wafanya kazi mmevulrugwa mnahisi nchi nzima ni wafanyakazi tu. Nyie ni asilimia ndogo sana
Msimshauri Mh. Rais vibaya.
Hakuna mfanyakazi anayedai mshahara anaitaka yeye Mwenyewe. Mishahara inapangwa na serikali.Serikali ndiyo iliyowaahidi kuwa itawaongezea. Na inaoaswa kutekeleza nyongeza kama ilivyoahidi bila kupigiwa magoti au kupigwa magoti.

Kila mtu atimize majukumu yake. Kodi Kwa mfanyabiashara ni lazima na sio kubembelezana. Sasa watu wanaanza kuhujumu nchi halafu hatuoni kauli Kali za kukemea na watu kutumbuliwa. Wakuu wa Wilaya wengi hawajui majukumu yao ya kumsaidia Rais kuzuia matumizi mabaya ya Kodi za watu. Nchi Wanyama wanatoroshwa. Tembo wanavamia vijiji na kudhuru watu. Idara zinanunua magari ya kifahari kila kukicha Kwa pesa za Mikopo badala ya kupunguza matumizi.

Vitu vinapanda Bei Kwa sababu watu waliaminishwa kuwa Mishahara itaongezwa. Mbona JPM hakuongeza miaka mitano na wafanyakazi wengi walimkubali na kuchapa kazi mana waliona kila mtu anaisoma namba. Leo wachache wanaogelea kwenye anasa na ufahari Kwa kukwepa Kodi,rushwa, kuuza nyara za serikali,vikao visivyo na tija,seminar na safari za kutalii Kwa fedha za umma. Eti wafanyakazi wa idara Fulani wanakwenda kutalii Mlima Kilimanjaro Kwa fedha za umma . Ujinga mtupu. Utalii unapoaswa kufanywa na mtu binafsi au kikundi binafsi Tena wakati wa Likizo sio wakati wa kazi. Watu wanaongezea wafanyakazi kiwango Cha posho za vikao ili iweje ,wanalenga Nini kama sio matumizi mabaya ya Pesa za serikali.

Kuna nchi Moja Waziri Mkuu aliahidi kujenga nyumba laki Moja Kwa Miaka mitano.Na akasema endapo atashindwa basi atachoma moto na kuteketea mbele ya vyombo vya habari. Alipambana akajenga nyumba zaidi ya Elfu sitini. Ahadi yake haikutimia Kwa kipindi hicho. Alichofanya ni kuita waandishi wa habari na kujichoma moto.
Wenzetu wameendelea sio Kwa Viongozi kubebwa Bali Kwa viongozi kuibeba jamii.

Watanzania waamke Sasa. Mabadiliko wasipoyapata ndani ya CCM watayapata nje ya CCM. Kauli ya baba wa Taifa aliitamka akiwa na uzalendo mkubwa nafsini mwake ,akiwa alipenda sana Taifa lake,akiwa ana mzigo mkubwa Kwa ustawi wa watu wake. Maneno yanayonenwa au kutamkwa Kwa hisia ya dhati Toka Moyoni na mtu aliyepewa mamlaka juu ya watu na Kiongozi mkubwa na mtu mzima mwenye mvi kichwani lazima yatatimia.

Na CCM wasijisahau Kwa sababu anguko lao linachukua muda mrefu mana litaanguka wakiwa hawakutegemea na itaangukia mikononi mwa mtu atakayekuwa rungu la kuwasagasaga kabisa kwani atakua ni rungu wasilolitaka.

Ni vizuri Mama akaendelea mpaka 2030 ili Watanzania waendelee kumtafuta mtu wa kuja kuwakamata wezi na mafisadi waliofuja Kodi za wanyonge tangu mwaka 1995 mpaka Sasa. Huo ndio mpango wa Mungu uliokaa vizuri kabisa. Watu watauona ukuu wa Mungu kwenye Taifa lake.

Kazi iendelee.
 
Ongezeko la bei la vyakula sio jambo la kishangilia hata kidogo. Chakula ndio hitaji kuu katika mahitaji muhimu ya binadamu kuliko hata malazi-bei za vyakula zinavyopaa unatengeneza anguko baya sana la kiuchumi.
Huyo hajui kua ukiona chakula kinapanda Bei basi ujue uzalishaji umepungua. Wazalishaji wengi ni wazee. Vijana wengi wamekimbilia mijini kuendesha boda boda na kuuza bidhaa za china. Wengi wanapiga debe mpaka kwenye Bajaji. Tena ni wale Vijana wenye nguvu kabisa . Kilimo kinabaki Sasa na wazee na Vijana wachache sana. Vyakula vinazidi kupanda Bei. Hata vinavyopatika kama matunda ni Yale Yale yaliyopandwa na mababu na wakaloni kama machungwa ,maembe na Nazi hakuna mazao mapy. Kahawa Vijana hawaziwezi, korosho ni zile miti za tangu mkoloni. Epo , Pera, limao, chenza, ndimu ni miti iliyopandwa na mababu n.k. Walaji wanaongezeka wazalishaji wa chakula wanapungua.
 
Acha haya maneno yako siyo mazuri hata kidogo. Halafu pia mnajua uchumi wa dunia nzima umevurugika tena Tanzania sisi tuko vizuri sana! Tumshukuru Mungu. Tumia hii simu janja yako kufuatilia mfumuko wa bei Marekani na Ulaya.
Sisi sio Marekani mkuu.
Tanzania ardhi ni Mali ya umma. Unaweza ukalima popote na ukavuna ,tatizo mitaji hawapewi wakulima wakati fedha zipo. Wanasiasa walioko madarakani na wallnaolamba asali hawana Nia ya dhati wa kuhakikisha Marekani inakuja kujifunza kwetu. Tanzania ingeweza kuwepo bila Marekani.
Kwani Marekani ikitokea imepigwa na Kimando Toka angani na ikapotea basi watanzania na sisi tutakufa. Jibu ni Hapana.
Nenda kaangalie Mikopo inayovyotolewa kisiasa. Mikopo ni vikundi vya wahuni wanaopeana TU na haizalishi chochote zaidi ya kutafuta umaarufu wa kisiasa. Unatoaje Mikopo Kwa wauza nyanya kabla hujatoa Mikopo Kwa wakulima wa nyanya ili wazalishe Kwa wingi. Mikopo yenyewe haijawahi kurejeshwa. Ni Mikopo ya wapiga kura wangu.
Nenda Tassaf uangalie uhuni na usanii unaofanyika. Mabilioni ya pesa yanaliwa Kwa vikao kila siku. Eti wanafanya seminar za kuwabaini maskini kwenye vijiji. Pesa zimetengwa Kwa ajili ya maskini lakini zinawaneemesha walioshiba tayari na maskini wanapiga miayo. Unaita watu hamsini kwenye kikao unawalipa kila siku posho ya vikao Kwa siku 14 halafu unakwenda kuwapa sh. Elfu 20 kaya kumi 10 maskini. Halafu unalinganisha Tanzania na Marekani.

Kuna Tatizo mahali sio Bure.
 
Amekuwa makamu wa raisi kwa miaka mitano na sasa ni raisi hatujui ya mungu mengi kama 2025 atafika

Kwa kuangalia mwenendo mzima jinsi anavyoongoza wananchi ni wazi kuwa anafaa apumzike kwani hawezi kufatilia jambo lolote linalohusu serikali yake zaidi ya safari anazoenda marakwamara akitafta mikopo, bidhaa zimepanda kila kitu hakishikiki, watumishi wa umma kila aliyeenda enda benki amebaki analialia kwani matarajio yao hawakuamini kama wangeongezewa kiasi cha tsh 20,000/= siyo wakulima wanalia na mbolea tukirudi kwenye bati nondo na saruji vyote kwa sasa ni mwiba kwa mtu mwenye kipato cha chini

Mimi kwa kuwa naona mama amebaki kutuma wasaidizi wake na wanamletea taarifa za uongo huku fesha zikitafunwa naomba apumzike

Kuna mambo mama anayaamini amejiewekeza kwenye kundi la wanasiasa wachache akiamini kwamba wao watamsaidia kuchaguliwa kuwa rais, wananchi amewasahau na ndiyo maana hata waziri yoyote anayesemwa ni mzigo hawezi kumtoa wananchi mtapiga kelele mtakaa kimya mambo yako hivo kiujumla mama anakiamini kile kikundi cha Msoga gang kuwa kitampa uraisi hata kama wananchi wasipo mpigia kura huo ndoo ukweli mchungu.
Hayo Mambo ya vitu kupanda Bei Kama sukari, cement, bati nk tulipiga Sana kelele enzi za JPM mkasema tunatumiwa na mabeberu . Kitu Cha ajabu Leo hii vitu ambavyo tulivipigia kelele enzi za JPM Leo hii ndio mmepata akili ya kugundua. Nyie kwenu watu Walikuwa wakitekwa kwenu ni sawa tu , wakiuawa, kubambikwa kesi, udanganyifu kwenye uchaguzi kwanu mlifumba macho na masikio.

Wakulima enzi za JPM soko lilikuwa bovu Sana mazao tuliuza kwa Bei ya hasara lakini hamkunyanyua mdomo kuwatetea wakulima, zaidi mliishia kuwambia wafanye kazi ilihali kazi wamefanya lakini soko bovu mkawaita wakulima wanatumiwa na mabeberu kuchafua nchi ilihali wanadai haki zao
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom