Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau amani iwe kwenu.
Kama kuna wabunge ambao wanapata shida sana wanapochangia bungeni basi bila shaka kwenye orodha hiyo hakosekani Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea. Kabla hajawa mbunge, Watanzania wengi na hasa wafuasi wa CHADEMA waliaminishwa kuwa Kubenea ni mtu makini na amekuwa akiandika kwenye gazeti lake la Mwanahalisi taarifa za kiuchunguzi ambazo zimefanyiwa utafiti wa kina. Naamini pia ni kutokana na kuaminishwa huko, ndio maana wananchi wa Ubungo wakampa kura nyingi ili awe mbunge wao.
Muda mfupi tu baada ya kuchaguliwa kwake, hakika sura halisi ya Kubenea inaanza kuonekana. Kubenea kwa sasa anaonekana ni mwanasiasa mkurupukaji na asiye na uwezo wa kupangilia hoja anapoongea. Miongoni mwa mambo ambayo hakika yamemuumbua sana Kubenea ni lile sakata la wabunge kuvuliwa shanga na chupi. Hakika tukio hilo lilimwachia Kubenea aibu kubwa sana kwani alishambulwa mpaka wabunge wa UKAWA.
Tukio jingine ni hili la juzi ambaye alisema kuwa JWTZ ilitoa ardhi kwa kampuni ya Hennang Guiging Industry Investment kwa ajili ya kufanya ujenzi wa nyumba kwa miaka 40. Waziri wa Ulinzi amekanusha madai hayo na ndipo Naibu Spika Tulia Akson alipotoa siku nne kwa Kubenea kuthibitisha madai yake vinginevyo atachukuliwa hatua kali za kisheria. Siku alizopewa zinaisha Jumanne na endapo atashindwa kuthibitisha hakika si tu kuwa atakabiliwa na adhabu kali bali pia atakuwa ameendeleza kujidhalilisha.
Wadau, kwa sisi tunaomwelewa Kubenea, hatushangazwi hata kidogo na haya yanayomkuta Bungeni. Siku zote amekuwa mkurupukaji na mpika majungu na amekuwa akitumia vyombo vyake vya Mwanahalisi na Mwanahalisi Online kutekeleza azma yake.