========================
"Mh Raisi niache niseme na unisikilize ukinipeleka hivyo sitoweza kujibu" John Heche. Nyamongo.========================
KWAMBA; Rais anatakiwa kuwasikiliza wasaidizi wake wa chini kabla ya kutoa maamuzi ya ghafula.
KWAMBA; Rais atambue kuwa kuna maswali mengine yanahitaji maelezo kabla ya kujibu Ndiyo au Hapana hasa yahusuyo pesa.
KWAMBA; Rais atambue kuwa Mbunge hawajibiki kwake angeamua hata kutojibu, mbunge anawajibika kwa Wananchi, Spika na Bunge, na kuna kamati za bunge na kamati za majimbo zinazohusika na mfuko wa jimbo.
KWAMBA; Rais akubali kusikiliza mawazo mbadala hata kama yatatolewa na mpinzani wake kisiasa, na anapouliza au kuhoji awe rational kwa wabunge wote.
KWAMBA; Rais atambue kuwa sio kila mtu anaweza kupelekeshwa kuna wengine wana misimamo isiyo yumbishwa.
KWAMBA; kwa style ya maswali ya kushtukiza rais anayouliza hadharani, asitarajie kupata majibu ya uhakika na anayotaka yeye au kusikia alichotarajia kuna majibu mengine yanaweza kumfedhehesha.
KWAMBA; Rais atambue kuna baadhi ya sehemu, mikoa na makabila yana ujasiri wa asili, maeneo kama Tarime, Mbeya, kwa hiyo akitembelea maeneo hayo awe amejiandaa kisaikolojia na kiusalama kama tulivyoona ulinzi wake ulivyoimarishwa alipoingia mkoa wa Mara.
SISI WANANCHI NA VIJANA TUMEJIFUNZA NINI:
KWAMBA; tusiwe waoga pindi tunapoongea na viongozi wetu wakuu, tujiamini, lkn tuwaheshimu, kuna mwingine anapoulizwa kitu na rais anapoteza kumbukumbu kabisa anashindwa hata kutaja cheo chake.
KWAMBA; heshima inazo pande mbili kama shilingi 'it's a two way traffic' heshimu uheshimiwe.
NI FUNDISHO pia kwa wabunge wa CCM na baadhi ya Wabunge wa Upinzani wanaopenda kuonyesha heshima ya kinafiki wawapo mbele ya Rais huku wananchi wao wakikosa huduma za msingi, utawasikia wakisema, jimboni kwangu watoto wote wana madawati, dawa zimejaa hospitalini na maji yanapatikana kwa asilimia 95.
Asante sana John Heche kwa kutoa shule hii ya bure kabisa ni matumaini yangu kuwa, pande zote mbili za viongozi/watawala na upande wa wananchi zimejifunza vya kutosha.