Kwa Jicho la Tatu: Majibu ya John Heche kwa Rais yana fundisho kubwa kwa watawala na wananchi

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,272
========================​
"Mh Raisi niache niseme na unisikilize ukinipeleka hivyo sitoweza kujibu" John Heche. Nyamongo.
========================​

KWAMBA; Rais anatakiwa kuwasikiliza wasaidizi wake wa chini kabla ya kutoa maamuzi ya ghafula.

KWAMBA; Rais atambue kuwa kuna maswali mengine yanahitaji maelezo kabla ya kujibu Ndiyo au Hapana hasa yahusuyo pesa.

KWAMBA; Rais atambue kuwa Mbunge hawajibiki kwake angeamua hata kutojibu, mbunge anawajibika kwa Wananchi, Spika na Bunge, na kuna kamati za bunge na kamati za majimbo zinazohusika na mfuko wa jimbo.

KWAMBA; Rais akubali kusikiliza mawazo mbadala hata kama yatatolewa na mpinzani wake kisiasa, na anapouliza au kuhoji awe rational kwa wabunge wote.

KWAMBA; Rais atambue kuwa sio kila mtu anaweza kupelekeshwa kuna wengine wana misimamo isiyo yumbishwa.

KWAMBA; kwa style ya maswali ya kushtukiza rais anayouliza hadharani, asitarajie kupata majibu ya uhakika na anayotaka yeye au kusikia alichotarajia kuna majibu mengine yanaweza kumfedhehesha.

KWAMBA; Rais atambue kuna baadhi ya sehemu, mikoa na makabila yana ujasiri wa asili, maeneo kama Tarime, Mbeya, kwa hiyo akitembelea maeneo hayo awe amejiandaa kisaikolojia na kiusalama kama tulivyoona ulinzi wake ulivyoimarishwa alipoingia mkoa wa Mara.

SISI WANANCHI NA VIJANA TUMEJIFUNZA NINI:

KWAMBA; tusiwe waoga pindi tunapoongea na viongozi wetu wakuu, tujiamini, lkn tuwaheshimu, kuna mwingine anapoulizwa kitu na rais anapoteza kumbukumbu kabisa anashindwa hata kutaja cheo chake.

KWAMBA; heshima inazo pande mbili kama shilingi 'it's a two way traffic' heshimu uheshimiwe.

NI FUNDISHO pia kwa wabunge wa CCM na baadhi ya Wabunge wa Upinzani wanaopenda kuonyesha heshima ya kinafiki wawapo mbele ya Rais huku wananchi wao wakikosa huduma za msingi, utawasikia wakisema, jimboni kwangu watoto wote wana madawati, dawa zimejaa hospitalini na maji yanapatikana kwa asilimia 95.

Asante sana John Heche kwa kutoa shule hii ya bure kabisa ni matumaini yangu kuwa, pande zote mbili za viongozi/watawala na upande wa wananchi zimejifunza vya kutosha.
 
Mzee baba apo ni kua huyo 'self-declared' Kichaa alitaka kuabudiwa once again.....

Ila kwanini mtu uuze utu na roho yako kisa cheo au mamlaka fulani ilihali mwisho wa siku unakufa....

Yani mtu unajijua kabisa wewe sio milima tuseme kwamba utaishi milele, yet unakubali kuuza utu wako eti kisa mkono uende kinywani!....pathetic!

Lucky Dube katika wimbo wa "Respect" alisema ".......I Got No Time to Worship Humankind".

I still dont get it....and probably never will I!
 
Heche alifanya vizuri sana, yule mzee anajiona yeye ni mungu, anataka kila mtu amtetemekee. Anafurahi pale anapowadhalilisha viongozi wa chini yake mbele ya halaiki ili ashangiliwe. Anatakiwa ajifunze kuheshimu viongozi wenzake wa chini.

Hongera Heche John.
 
========================​
"Mh Raisi niache niseme na unisikilize ukinipeleka hivyo sitoweza kujibu" John Heche. Nyamongo.
========================​

KWAMBA; Rais anatakiwa kuwasikiliza wasaidizi wake wa chini kabla ya kutoa maamuzi ya ghafula.

KWAMBA; Rais atambue kuwa kuna maswali mengine yanahitaji maelezo kabla ya kujibu Ndiyo au Hapana hasa yahusuyo pesa.

KWAMBA; Rais atambue kuwa Mbunge hawajibiki kwake angeamua hata kutojibu, mbunge anawajibika kwa Wananchi, Spika na Bunge, na kuna kamati za bunge na kamati za majimbo zinazohusika na mfuko wa jimbo.

KWAMBA; Rais atambue kuwa sio kila mtu anaweza kupelekeshwa kuna wengine wana misimamo isiyo yumbishwa.

KWAMBA; kwa style ya maswali ya kushtukiza rais anayouliza hadharani, asitarajie kupata majibu ya uhakika na anayotaka yeye au kusikia alichotarajia kuna majibu mengine yanaweza kumfedhehesha.

KWAMBA; Rais atambue kuna baadhi ya sehemu, mikoa na makabila yana ujasiri wa asili, maeneo kama Tarime, Mbeya, kwa hiyo akitembelea maeneo hayo awe amejiandaa kisaikolojia na kiusalama kama tulivyoona ulinzi wake ulivyoimarishwa alipoingia mkoa wa Mara.

SISI WANANCHI NA VIJANA TUMEJIFUNZA NINI:

KWAMBA; tusiwe waoga pindi tunapoongea na viongozi wetu wakuu, tujiamini, lkn tuwaheshimu, kuna mwingine anapoulizwa kitu na rais anapoteza kumbukumbu kabisa anashindwa hata kutaja cheo chake.

KWAMBA; heshima inazo pande mbili kama shilingi 'it's a two way traffic' heshimu uheshimiwe.

Asante sana John Heche kwa kutoa shule hii ya bure kabisa ni matumaini yangu kuwa, pande zote mbili za viongozi/watawala na upande wa wananchi zimejifunza vya kutosha.
hapo siyo ujuaji na mbwebwe ajibu swali, Maelezo ya nini?
 
Heche alifanya vizuri sana, yule mzee anajiona yeye ni mungu, anataka kila mtu amtetemekee. Anafurahi pale anapowadhalilisha viongozi wa chini yake mbele ya halaiki ili ashangiliwe. Anatakiwa ajifunze kuheshimu viongozi wenzake wa chini.

Hongera Heche John.
Na huko katika chama chao hakuna mtu mwenye uthubutu wa kufanya kama alivyofanya Heche??
 
Heche alifanya vizuri sana, yule mzee anajiona yeye ni mungu, anataka kila mtu amtetemekee. Anafurahi pale anapowadhalilisha viongozi wa chini yake mbele ya halaiki ili ashangiliwe. Anatakiwa ajifunze kuheshimu viongozi wenzake wa chini.

Hongera Heche John.
hahahaha Heche maneno mengi akiwa mbali na Rais alipokutana nae anabaki kujichekesha tuuuu
 
Mimi nafikiri Mh Rais wala haitaji majibu fulani bali ndio namna yake yakuwadhalilisha viongozi wenzake. Mbona haruhusu wananchi wamuulize maswali kulingana na uongozi wake??

Hotuba zake kwa sasa zimeshapoteza mvuto kwa wananchi. Na hili nikutokana na lugha zake za maudhi. Anapaswa kuchagua maneno yakusema kulingana na hadhi ya kiti chake. Lugha yake ile ingetafsiriwa na kurushwa kwa marais wenzake duniani sijui ingekuaje??
 
"KWAMBA; Rais atambue kuna baadhi ya sehemu, mikoa na makabila yana ujasiri wa asili, maeneo kama Tarime, Mbeya, kwa hiyo akitembelea maeneo hayo awe amejiandaa kisaikolojia na kiusalama kama tulivyoona ulinzi wake ulivyoimarishwa alipoingia mkoa wa Mara"

Hahahahah Kama kujifariji kungekuwa kuna wapeleka watu ikulu hakika chadema ingetawala milele kabisa
 
Back
Top Bottom