Kwa imani yako!

Kwa imani yako!

Huo ni msaada wa kubahatisha. Nenda ukaombe msaada kwa Wizara ya Elimu.
 
Pole sana kwa yote ni changamoto tu za kidunia watakaoguswa watakusaidia !binafsi nitafanya hivyo Jipe moyo utayashinda...!
 
Nashukuru kaka issa. Si haba naiman nitapata kwengine pia
 
hela za mb kuingia huku umetoa wapi? ndugu zako wanafanya kazi gani? kwanin usifanye vikao vya ukoo ukachangiwa pesa pamoja na mambo mengine maana unaweza ugua pia? unasali dhehebu gani? kwa nini usizungumze na kiongozi wa kanisa kwa hali uliyonayo ili uwekwe kwenye kundi la watoto yatima ufaidike na misaada hata kanisani unaweza changiwa vizuri tu? unaishi kijiji gani ,kata gani,jimbo gani na wilaya gani? diwani wako ni nani na mbunge wako ni nani maana kuna pesa za maendeleo ya jimbo huwa wanapata pia kikao cha madiwani kinaweza anzisha miradi eneo husika ili kuwasaidia nyinyi kama mtakuwa wawazi kwao.

Mtazamo wangu uko kwenye kutafuta suluhu ya kudumu sio ya muda mfupi, kama uko kwenye hali ngumu sana huna hiyo 65 maana yake hata chakula ni tabu, unanunuaje mafuta ya kupika na kulipia umeme na kununua vitabu ,pamflet na madaftari? ili kupata suluhu ya kudumu fanya hayo hapo niliyoandika
 
Pole sana kwa matatizo yanayokukuta kaika umri wako huu mdogo.

Naomba kwanza nikushauri kitu. Katika mmaisha yako yote, kwanza jifunze uvumilivu hasa wakati wa shida. Usipende kutafta suluhu za muda mfupi katika matatizo yako maana mwisho wake siku zote huwa mbaya.

Yes hauna baba lakini nina imani unao ndugu wa baba au mama au hata ndugu zako wa tumbo moja. Je, umeshaongea nao hao kwanza? Pili, kama webgine walivyokuuliza, unaishi wapi kwa sasa? Je umeshauona uongozi wa eneo unaloishi? Ni rahisi sana kupata msaada katika eneo unaloishi kuliko kuja kuomba msaada humu ambapo humfahamu mtu yeyote. Ninaelewa kuwa baadhi ya koo/familia/ndugu hawajaliani, ila kuna sehemu nyingi unaweza kupata msaada.

Kama wewe ni mkristo, natumaini unafahamu kuwa kuna jumuiya kila mtaa. Hebu uone uongozi wa jumuiya yako nina hakika WATAKUSAIDIA! Ninaongea hayo nikiwa na uhakika kwa sababu mimi ktk jumuiya yangu tunasomesha vijana 2 waliofiwa na wazazi wao, ambao walikuwa wanajumuiya wenzetu. Tulianza nao wakiwa kidato cha pili na mwaka huu wanamaliza kidato cha nne! Anza hapo nina hakika utapata msaada as msaada usiokuwa na masharti!!
 
Kwa ushauli naomba uwanze kuuza iyo smart phone unayo tumia

sikuingia hapa kwaajili ya kubishana! Kama ulikuwa hauna la maana la kuweza mfariji mtu ni vyema ungetulia ndugu yangu. Haukuzingatia katika somaji wako! Ila ahsante kwa ulichokinena!! Mungu akubariki.
 
Ahsanten kwa nyoote mliohusika kwa namna moja ama nyingine. Mungu awe nanyi milele. Kwa wenye kauli njema na thabiti awazidishie na kwa wale wenye kauli chafu nao pia awaongezee.
 
sikuingia hapa kwaajili ya kubishana! Kama ulikuwa hauna la maana la kuweza mfariji mtu ni vyema ungetulia ndugu yangu. Haukuzingatia katika somaji wako! Ila ahsante kwa ulichokinena!! Mungu akubariki.

Kwani amebishana na wewe au kakushauri? Kupanga ni kuchagua, au umiliki simu usifanye mtihani au uuze simu ufanye mtihani.

Omba msaada pale ambapo hauna machaguo kabisa. 70,000 sio nyingi kihivyo kiasi cha kushindwa kuraise. Tena waweza fanya vibarua weekend na kutengeneza hiyo pesa badala ya kujidhalilisha na mwisho kutukanana na watu usio wajua.

Utamaduni wa kuomba naona ni cancer nyingine Tanzania, we have learned from the best and the FIRST.
 
Watz ndio mko hvyo hvyo mmelaumu sana diaspora kumbe 65,000 tu hamtoi, sa lawama za nini au roho mbaya tu🙉🙉

We usitake mjadala na Mimi kama hiyo mada unitaka sana rudi kule kule
 
Ahsanten kwa nyoote mliohusika kwa namna moja ama nyingine. Mungu awe nanyi milele. Kwa wenye kauli njema na thabiti awazidishie na kwa wale wenye kauli chafu nao pia awaongezee.

Daah mkuu kauli yako imenivunja maini kabisa duh haya mkuu kila la heri
 
Back
Top Bottom