Kwa hili, Wizara ya Elimu izingatie

dustless

JF-Expert Member
Oct 21, 2016
796
712
Habari wakuu, moja kwa moja kwenye mada.

Suala la nafasi za uongozi kwenye ngazi za Elimu litazamwe upya namna zinavyopatikana. Shule nyingi zimekuwa na changamoto lukuki kwa sababu tu ya menejimenti mbovu ya wasimamizi wa vitengo husika.

Hii ni kwa sababu viongozi wanapewa nafasi hizo pengine kwa kuwa karibu na mkubwa fulani ama kwa udahaifu walionao ili watumike kunufaisha waliowaweka.

Ukweli ni kwamba, mkuu wa shule mzuri siku zote anafahamika katika staff husika. Hivyo basi, shule ingepewa mamlaka ya kuchagua mkuu wake wa shule mwenye uwezo wa kusimamia na kuongoza shule bila kuwa na ubaguzi wala upendeleo wowote.

Na awe mstari wa mbele kusikiliza kero na kutatua changamoto mbalimbali zilizo chini ya uwezo wake kuliko ilivyo sasa kwa wakuu wengi waliopo.

Wengi wamekuwa vibaraka wa halmashauri huku wakiacha jopo kubwa la walio chini yao wakiishi bila matumaini huku haki zao zikiminywa na baadhi ya wakurugenzi wasio na mapenzi mema na nguvu kazi ya taifa hili.

Kwa hiyo nafikiri kada hii ingepewa meno kujiendesha kwa maana ya kuwa na uwezo wa kumchagua, kumthibitisha na pengine kumwajibisha mkuu wa shule anaeshindwa kusimamia majukumu yake sawasawa.

Vivyo hivyo ifanyike kwa ngazi zingine kama vile uafisa Elimu wilaya, nafasi hiyo ipatikane baada ya kushindanisha ubora wa wakuu wa shule katika wilaya husika, atakae ibuka ndiye awe kiongozi wa nafasi hiyo.

Hali kadhalika kwa maafisa Elimu mikoa wapatikane kwa kwa kushindanishwa maafisa Elimu wa wilaya wote katika mkoa husika na kiwepo kipindi maalumu cha kutathimini utendaji wake ili inapotokea kashindwa kusimamia nafasi yake awajibishwe au aondoshe kabisa kwenye nafasi hiyo.

Hii itafanya watu wawajibike katika nafasi wanazopewa na kukuza kama si kuimarisha mfumo wetu wa Elimu nchini kuliko ilivyo sasa ambapo wenye vyeo hivi wanajifanya miungu watu kwa kuwa wanakiburi chini ya vivuli vya waliowaweka.

Wengi wao hawasimamii vyema nafasi zao, wanaficha matatizo ya waalimu wenzao na mbaya zaidi wanatumiwa na baadhi ya wakurugenzi kukandamizi haki za watumishi kwa manufaa yao binafsi.

Na inafikia wakati halmashauri fulani fulani jina kapuni zimeshindwa kulipa fedha za likizo kwa baadhi ya waalimu kwa kisingizio cha umbali wa waliko zaliwa, watumishi watakuwa wamenielewa. Maana umbali wa mtumishi alikozaliwa una determine kiasi cha pesa atakachopewa.

Hili ni tatizo moja kati ya mengi yanayodhorotesha ufanisi wa kazi katika kada hii kutokana na upatikanaji mbovu wa viongozi wao.
Ni hayo tu kwa leo.
 
umeongea kweli kabisa hii sms wangeipata watu wa Manispaa Ya Mtwara Mikindani ingekuwa nzuri zaidi maana kuna akina maproo huko hawana vigezo zaidi ya rushwa na ujanja ujanja tu.
 
Lindi manispaa inawahusu....walimu wanaodai malipo kwa likizo za miaka kedekede jibu wanalopewa ni rahis....wanaletewa fedha kidogo....
 
umeongea kweli kabisa hii sms wangeipata watu wa Manispaa Ya Mtwara Mikindani ingekuwa nzuri zaidi maana kuna akina maproo huko hawana vigezo zaidi ya rushwa na ujanja ujanja tu.
Ukweli lazima tuuseme. Tupaze sauti kwa pamoja.
 
Lindi manispaa inawahusu....walimu wanaodai malipo kwa likizo za miaka kedekede jibu wanalopewa ni rahis....wanaletewa fedha kidogo....
Halmashauri nyingi viongozi hawa ni tatizo kubwa. Nimekaa pengi nimeshuhudia uozo huu.

Mamlaka husika walitazame hili kwa jicho la tatu, kama kweli nao wana nia ya dhati na taiga hili. Kwa maana tunaoongea haya tumo jikoni tunajua ukweli uliopo.
 
Mamlaka husika wanaingia humu? Jitahidi kuwasilisha hija panapohusika umeona jambo kubwa na ninaamini hili sio kada ya Elimu tu Bali inawezekana ni maeneo mengi
 
Mamlaka husika wanaingia humu? Jitahidi kuwasilisha hija panapohusika umeona jambo kubwa na ninaamini hili sio kada ya Elimu tu Bali inawezekana ni maeneo mengi
Tatizo lililopo unaweza toa wazo lako wakalidump. Ndo maana tunaona bora tutumie mitandao ya jamii tu. Naamini watasoma wakubwa, tunao humu...
 
Tatizo lililopo unaweza toa wazo lako wakalidump. Ndo maana tunaona bora tutumie mitandao ya jamii tu. Naamini watasoma wakubwa, tunao humu...
Hapana huo ni mtizamo wako usiogope jaribu then utaleta mrejesho Siku chache zijazo
 
Hongera kwa wazo zuri ila navyuojua hawawezi kuufanyia kazi kwa sababu watawala/walimu wakuu wengi huchaguliwa na wakubwa ili wapige dili kama ulivyosema wewe hapo juu........wakitumia mapendekezo yako watakosa ulaji!!
 
Hapana huo ni mtizamo wako usiogope jaribu then utaleta mrejesho Siku chache zijazo
Mkuu umewahi fanikiwa kwa approach hiyo ili nami nijaribu? Unipe na hiyo trik ili nmuadress muhusika moja kwa moja.
 
Hongera kwa wazo zuri ila navyuojua hawawezi kuufanyia kazi kwa sababu watawala/walimu wakuu wengi huchaguliwa na wakubwa ili wapige dili kama ulivyosema wewe hapo juu........wakitumia mapendekezo yako watakosa ulaji!!
Hakuna kitu kibaya kama kuwa na kiongozi au msimamizi wa taasisi fulani halafu awe kivuli au daraja la wajanja wachache.

Maendeleo halisi itakuwa ni ndoto na kikubwa hapo itakuwa ni kutimiza matakwa ya hao wajanja...
 
Haki ya mungu serikali ingeamua kuwatumia walimu sawasawa juu ya mwenendo na maamuzi ya wakuu wa shule wengi hawatasalimika, wapo wanaoongoza kukwanyua mahindi ya shule(kulala na wanafunzi), wakiona mwl. fulani anakerwa na tabia hiyo hapo fitina zitaanza hadi uhame!
 
Wakuu wa shule hasa hizi za kata waondolewe maana wengi waliingia kwa tiketi ya uzoefu tu.Elimu zao hazitoshi hizo nafasi ndiyo maana kila siku porojo na kutetemekea waliowateua.Vitu vingine serikali inafanya maksudi kuzalisha migogoro.Hivi mwl wa cheti unamlipa posho wakati hapohapo wapo degree wengi,ufanisi utakuwepo kweli.mwanafunzi kuongoza walimu wake! Only in Tz.
 
Viva Tanzania,,, kumbe bado tuna watu wanawaza vizuri namna hii? Barikiwa Sana
 
Haki ya mungu serikali ingeamua kuwatumia walimu sawasawa juu ya mwenendo na maamuzi ya wakuu wa shule wengi hawatasalimika, wapo wanaoongoza kukwanyua mahindi ya shule(kulala na wanafunzi), wakiona mwl. fulani anakerwa na tabia hiyo hapo fitina zitaanza hadi uhame!
Kuna matatizo chungu nzima, uwezo wa wengi wao ni mdogo sana katika kuongoza..
 
Wakuu wa shule hasa hizi za kata waondolewe maana wengi waliingia kwa tiketi ya uzoefu tu.Elimu zao hazitoshi hizo nafasi ndiyo maana kila siku porojo na kutetemekea waliowateua.Vitu vingine serikali inafanya maksudi kuzalisha migogoro.Hivi mwl wa cheti unamlipa posho wakati hapohapo wapo degree wengi,ufanisi utakuwepo kweli.mwanafunzi kuongoza walimu wake! Only in Tz.
Kuna baadhi ya halmashauri wameanza kuwaondoa wenye Elimu ndogo, sema zingine kwa maslahi binafsi ya wakurugenzi bado wamewakumbatia watu hawa. It's shame!
 
Back
Top Bottom